JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Amos Nyang'waji (25), Mkazi wa Kijiji cha Matui Wilayani Kiteto Mkoani Manyara amehukumiwa kifungo cha miaka minne gerezani kwa kosa la kumcharaza viboko Karani wa Sensa na kuharibu kishikwambi chake wakati akitekeleza majukumu yake mnamo Agosti 25, 2022.
Imeelezwa mtuhumiwa akiwa nyumbani kwa kaka yake, ghafla alimvamia Karani wa Sensa, Cecilia Paul na kumshambulia, alipotakiwa kujitetea mtuhumiwa huyo alisema yeye ana tatizo la akili lililomfanya atende kosa hilo.
Akisoma hukumu, Hakimu Mosi Sasy wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Kiteto alisema mtuhumiwa ametenda makosa mawili kinyume cha Kifungu cha 241 Sura ya Kanuni ya Adhabu Sura ya 16 na Kifungu cha 326 Kifungu Kidogo cha Kwanza Sheria ya Kanuni ya Adhabu Sura ya 16.
Kosa la kwanza la shambulio la mwili hukumu yake ni miaka mitano jela, kosa la pili kuharibu mali hukumu yake ni miaka 7 jela lakini kwa kuwa aliomba kupunguziwa adhabu akampa hukumu hiyo pamoja na faini Tsh. 700,000 na fidia Tsh. 500,000.
Source: EATV