Aua Mke na Mkwe wake

Mjanja M1

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2018
Posts
4,058
Reaction score
14,382
FESTO Maganga Mkazi wa Seguchini, Kata ya Nala, Wilaya ya Dodoma Mjini, anadaiwa kumuua mkewe na mama mkwe wake, kisha na yeye kuuawa na wananchi. Tukio hilo limetokea jana Jumapili Januari 28, 2024 majira ya saa 10 :30 jioni katika Mtaa wa Seguchini.

Akizungumza na chombo kimoja cha habari, mmoja wa ndugu za marehemu hao, Samwel Lengole amesema wiki iliyopita mama mkwe, ambaye ni mama wa mke wa mtuhumiwa, Anna Ngalai alikwenda kwa mwanaye Maria Joseph kusalimia.

Hata hivyo, amesema (jana saa 10.30 kuelekea saa 12 jioni) pasipo kufahamu ni nini kilitokea, ilikutwa miili ya mama na mtoto wake jikoni ikiwa imechomwa na kitu chenye ncha kali shingoni.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Martin Otieno amethibitisha tukio hilo akisema taarifa atazitoa baadaye.

Source - Nipashe
 

Safari hii Dodoma wamewajibu Geita na sio njombe Tena,mara wametulia
mara hatuui wanawake
 
tulia basi uje na kisa kamili ikiwemo sababu
 
Kesi kama hizi mara nyingi chanzo huwa ni mama wakwe kutaka kuongoza ndoa za watoto zao refer tukio la yule mwandishi na mume aliyeuwa mama yake na kujiuwa.
 
Ugonjwa wa akili is really.. tusipuuze dalili ndogondogo..!
 
Kina mama mwanao akiolewa muacheni aishi kwa amani na mumewe.

Kama hukubahatika kuolewa au maisha yako yote umekua singo maza usimuonee gere mwanao akiolewa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…