Friday Malafyale
JF-Expert Member
- Jan 18, 2017
- 1,811
- 2,916
Raia mmoja ambaye hajatambulika kwa haraka amekutwa amekufa kwa kuuliwa na kuchomwa moto hadi kufa. Kwa mujibu wa mtoa taarifa hii, tukio hili limetokea kijiji cha Luchelegwa Ruangwa Lindi njia inayoelekea Nachingwea kuna mwizi ameuawa na kuchomwa moto na wananchi wenye hasira kali usiku wa kuamkia leo asubuhi ambapo chanzo inadaiwa ni wizi wa mihogo.
Inadaiwa pia mmiliki wa shamba la mihogo alikuwa akilalamika mara kadhaa kuibiwa shambani mwake, hadi akaamua kuvizia wezi wa mihogo ndipo ikatokea mpambano mkubwa kati ya mwizi na mwenye shamba, ambapo mwenye shamba amejeruhiwa vibaya. Lakini pia mwizi ameuawa na kuchomwa moto.
Chanzo mwenyeji wa Luchelegwa Ruangwa Lindi.