Muuza Kangala
JF-Expert Member
- Jul 21, 2021
- 1,242
- 4,813
Inasikitisha sana. Labda ndio maana tunatakiwa kupata Gas za kupikia hadi vijijini
======
Kamanda Mwaibambe alimtaja marehemu aliyepigwa risasi wakati akiokota kuni ni Athumani Ramadhani ambaye baada ya kupigwa risasi ya kifuani alifariki dunia papo hapo.
"Kwa kweli hili ni tukio la kusikitisha na hivi sasa Jeshi la Polisi tunamshikilia mtuhumiwa ili kujibu tuhuma zinazomkabili za kufanya mauaji kwa raia," alisema Kamanda Mwaibambe.
Kiongozi huyo alisema kuwa maelezo ya mtuhumiwa ni kwamba alimpiga risasi ikiwa ni sehemu ya kujihami baada ya kumkamata kwa kuingia kwenye shamba hilo kinyume cha taratibu.
Alisema mtuhumiwa huyo katika maelezo yake kwa polisi, alidai wakati akijaribu kumtia nguvuni, alitaka kumvamia na ndiye alifyetua risasi.
Kamanda huyo alitoa wito kwa wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi kwa kuwa iwapo kunatokea vitendo vya uhalifu, wanapaswa waripoti kwenye mamlaka husika ili zichukue hatua.
Ibara ya 14 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania toleo la mwaka 1977, inaeleza: "Kila mtu anayo haki ya kuishi na kupata kutoka kwa jamii hifadhi ya maisha yake, kwa mujibu wa sheria".
Chanzo: IPP Media