Aubameyang ametia saini mkataba wa kuichezea Arsenal kwa miaka 3 na nusu

Aubameyang ametia saini mkataba wa kuichezea Arsenal kwa miaka 3 na nusu

real G

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2013
Posts
5,227
Reaction score
5,299
LONDON, UINGEREZA: Uhamisho wa mshambuliaji Pierre- Emerick Aubameyang kutoka Klabu ya Borussia Dortmund kwenda Arsenal umekamilika baada ya mchezaji huyo kusaini mkataba wa miaka mitatu na nusu kwa ada ya Pauni milioni 52.7.

Klabu ya Borussia Dortmund imethibitisha uhamisho huo kupitia mkurugenzi wake wa michezo, Michael Zorc aliyesema anamshukuru mchezaji huyo kwa mafanikio aliyoyaleta Dortmund licha ya matukio yasiyofurahisha yaliyotokea siku za karibuni

Aubameyang anafika katika klabu hiyo ya London akiwa katika kiwango cha kutisha cha kupachika magoli, akiwa amefunga magoli 100 katika mechi 119 alizochezea Dortimund kuanzia msimu wa 2015/2016

aubameyang3101ag.jpg
 
Back
Top Bottom