Aucho Vs Chama nani zaidi?

Christopher Wallace

JF-Expert Member
Joined
Dec 8, 2015
Posts
1,479
Reaction score
3,788
Tuweke ushabiki pembeni, japo wanacheza nafasi tofauti, Dr. Aucho wa Yanga na Chama yule wa kipindi akiwa Simba yupi ni mchezaji hatari zaidi akiwa na mpira?
 
Tuweke ushabiki pembeni, japo wanacheza nafasi tofauti, Dr. Aucho wa Yanga na Chama yule wa kipindi akiwa Simba yupi ni mchezaji hatari zaidi akiwa na mpira?
Ni ngumu kuwalinganisha wachezaji wanaocheza nafasi mbili tofauti. Majukumu ya chama Aucho hayawezi kuyafanya. Na pia majukumu ya Aucho, chama hayawezi kuyafanya.
 
Uwezi kuwafananisha kwakua wanacheza nafasi tofauti, Ila Chama ilimchukua muda kufanikiwa pale Simba.
Aucho nimchezaji mzoefu na amecheza nchi nyingi na timu nyingi amesha cheza mbaka timu za ulaya. Uku Kwetu Tanzania ni Kama karudi kijijini, Chama kwenye uzoefu ana mengi ya kujifunza kwa Aucho.
 
Nyani bwana!!ni kawaida yenu kurukaruka
 
Ni ngumu kuwalinganisha wachezaji wanaocheza nafasi mbili tofauti. Majukumu ya chama Aucho hayawezi kuyafanya. Na pia majukumu ya Aucho, chama hayawezi kuyafanya.
No! Unaweza kushindanisha watu wa nafasi mbili tofauti ila kumlinganisha chama na aucho ni kumkosea chama mno, chama ameipa simba vikombe, ameipeleka simba robo fainaili sasa aucho kaifanyia nini yanga?
 
Narudia tena ni ngumu kulinganisha wachezaji wenye majukumu mawili tofauti, sana sana mtaenda kwenye matokeo ya ujumla (mafanikio) lakini hautoweza kuwalinganisha kiufundi mpira hauko hivyo, je unawezaje kumlinganisha Neymar na De Gea? Zaidi tu ya mtaenda kwenye mafanikio ya mmoja mmoja na kushindwa kuwachambua kwa kiufundi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…