Audi A4 vs Toyota Crown nipe maoni yako

Ni kweli
ndio maana zinauzwa bei ghali kuliko Audi huko kwenye soko la mitumba.
Crown za zamani kidogo, zina body ( sijui ndio mnaita mabati ), ni magumu kishenzi, unaeza pigwa na anaekupiga ndio anaumia. Labda crown hizi latest ndio zina body nyepesi, na hii ni kwa magari mengi ya kisasa, sio yamekuwa body utopolo
 
Crown za zamani kidogo, zina body ( sijui ndio mnaita mabati ), ni magumu kishenzi, unaeza pigwa na anaekupiga ndio anaumia. Labda crown hizi latest ndio zina body nyepesi, na hii ni kwa magari mengi ya kisasa, sio yamekuwa body utopolo
body za zamani zilikuga gauge za mapipa zile 😁😁😁 ukigongwa na gari lazma ufe! Ila sikuhizi majeruhi kibao 😁😁😁
 
body za zamani zilikuga gauge za mapipa zile 😁😁😁 ukigongwa na gari lazma ufe! Ila sikuhizi majeruhi kibao 😁😁😁
😀😀😀 sasa hivi body zote zimekuwa soft sana, si ulaya , america wala japan. Body zimekuwa nyanya tu, wanacho jaribu ni kuongeza electronics safety features kwa kiasi kikubwa sana kwenye gari. Kama hata ukiangalia Features kama za Lexus Ls 500h au MerdezBenz Maybach S650.. utaona mwenyewe security imeamia kwenye electronics zaidi na sio mechanical
 
Watu kwakisikia machine ya Mjerumani wanapagawa kweli. Hizo Bmw 3 series na huyo Audi A4 kwenye soko la used cars wanabei za kawaida sana kuliko hata gari za TOYOTA .
Sababu ni zile zile IST inauzwa bei kuliko Crown zikishatumika Bongo. Used market wanaangalia bei poa, isile mafuta na isiwe na usumbufu. Kumbuka tunaonunua used ni wa hali ya kawaida. Pia watu wanaangalia uwepo wa mafundi wa bei rahisi
 
Nahisi pia na utunzaji wa muhusika. Crown zipo chini, kama mtumiaji yupo hovyo hovyo haichukui mda kukaa kwenye hali yake ya upya. Hii ni kwa gari yoyote ile hata ulaya pia. Matunzo muhimu sana
Leo nimeona Alphard namba DUP.. bampa la chini linaning'inia.

Vigari vya toyota nyanya sana.
 
Leo nimeona Alphard namba DUP.. bampa la chini linaning'inia.

Vigari vya toyota nyanya sana.
Inawezekana kabisa, ila sio Toyota zote na utunzaji pia ni muhimu. Kuna Merced Benz na kuna BMW zipo hoi body zao, ni kutokana na utunzaji wao mkuu.
 
Kwa kifupi tu:

Audi ni Slayqueen mrembo sana mbwembwe nyingi na gharama za hali ya juu. Havumili shida hata kidogo.

Crown ni wife material ila mrembo asilia au natural. Anavumilia hata wakati wa shida.

Ni hayo tu...kama una akili utajiongeza.
Ongeza Sauti Mkuu huku Backbenchers bado hatujakupata vizuri
 
Msitishe wtu nyie ,nilitaka kumiliki Subru nilitishwa sana,ila gari ni matunzo tu,ndugu yangu anyo mwaka wa 12 huu sijawahi kumuona akilia lia na zaidi ni kuisifia tu ila anazingatia sevice tu
 
Leo nimeona Alphard namba DUP.. bampa la chini linaning'inia.

Vigari vya toyota nyanya sana.
Mkuu wangu mara nyingi unakuta tatizo hata siyo gari bali ni mkono wa mtu, kuna watu wanaendesha magari rough sana. European cars especially hz sedan siyo rafiki sana wa rough driving kwenye barabara zetu. Kama Audi ukiiendesha barabara za kimara zilivyo mbovu unaweza pata pressure.
 
Sio kwa nia mbaya ila watumiaji wengi wa gari za mjapan wanatabia ya "sitaki mbichi hizi"
Wengi ambao wamekuwa wakitoa comments za kukatisha wengine tamaa unakuta kiuhalisia hajawahi kumiliki european car.

Mtu anaingia mtandaoni akikutana na comments 20 mbaya kuhusu aina fulani ya gari basi anahitimisha kwamba gari fulani ni mbovu, swali la kujiuliza je ni watu wangapi wanaomiliki hayo magari?? Je kila mtu ambae gari yake haimsumbui huwa anapeleka comment yake mtandaoni?

Ingia playstore au app store nenda katafute application yoyote ambayo wewe unaipenda na haijawahi kukusumbua kisha kaangalie comments za wadau uone kama hautakutana na comments mbaya.

Tuache kutishana kwa vitu ambavyo kiuhalisia hatujawahi kumiliki au kutumia.

Kama una experience ya toyota pekee ni vyema ukamshauri mtu mazuri ya toyota na mapungufu yake, anayemiliki audi naye atakuja kumshauri mazuri na mapungufu yake.

Muda mwingine baadhi ya watu huwa wanawasimulia story za kutisha kuhusu magari yao ili mpunguze kuazima, nyie mkitoka huko mnaibebelea story kama vile kweli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…