U Heard leo Soudy Brown kampata msichana ambae ametoka Mkoani kuja Dar kwa ajili ya kukutana na Aslay wa Yamoto Band.. Msichana huyo anadai ametoka Geita kuja Dar kukutana na Aslay.
Dada mwenyewe amesema walikuwa wakiwasiliana na Aslay kupitia Facebook wakabadilishana namba za simu, baadae anasema Aslay alimwambia aje Dar kwa na atapokelewa na ndugu yake kwa kuwa yeye yuko South Africa.
Msichana huyo amesema yuko Dar kafikia kwa mtu, ila anasubiri Aslay arudi kutoka Afrika Kusini, kingine ambacho anadai kwamba aliongea nae ni ishu ya kumtafutia kazi na yuko tayari kufanya kazi yoyote.
- SAUTI YAKE HII HAPA
Chanzo: MillardAyo