Audio: Dada kafunga safari hadi Dar kumfuata Aslay, walikutana Facebook

Audio: Dada kafunga safari hadi Dar kumfuata Aslay, walikutana Facebook

Lugano5

R I P
Joined
Jul 15, 2010
Posts
4,520
Reaction score
757
asl.jpg


U Heard leo Soudy Brown kampata msichana ambae ametoka Mkoani kuja Dar kwa ajili ya kukutana na Aslay wa Yamoto Band.. Msichana huyo anadai ametoka Geita kuja Dar kukutana na Aslay.

Dada mwenyewe amesema walikuwa wakiwasiliana na Aslay kupitia Facebook wakabadilishana namba za simu, baadae anasema Aslay alimwambia aje Dar kwa na atapokelewa na ndugu yake kwa kuwa yeye yuko South Africa.

Msichana huyo amesema yuko Dar kafikia kwa mtu, ila anasubiri Aslay arudi kutoka Afrika Kusini, kingine ambacho anadai kwamba aliongea nae ni ishu ya kumtafutia kazi na yuko tayari kufanya kazi yoyote.

- SAUTI YAKE HII HAPA

Chanzo: MillardAyo
 
Anahitaji kazi ni jasiri ameona kuna fursa.
 
Hako katoto kamepinda. kanasema kaliacha shule kwa sabau life ilizingua!!! Hapo hakuna kitu.
 
Huyu hana tofauti na yule baby_ake ....vischana vya siku hizi sijui vikoje ujinga ujinga mwingi
 
Huyu mtoto sijui kama atarudi kwao salama
 
huyo Aslay ana kasichana kake kanajiita tessychocolate IG siku hizi hakapi airtime sijui ndo kakatosa mwee watoto hawa
 
huyo mwanamke memory card nahisi imecheza, haiwezekani mtu mwenye akili timamu akatoka kote huko kuja kumfuata mtu asiemjua, nilimsikia alipoulizwa vipi unampenda Asley! ............akashindwa kujibu anajiumauma tu.
 
Back
Top Bottom