Mchokonozi
Member
- Nov 17, 2009
- 15
- 0
Mimi ni mgeni hapa, lakini nimeona nianze post yangu ya kwanza kwa habari hizi njema kwenu.
Nimepata habari kwa mtu ambaye alikuwa karibu sana na Mhe. Augustine Lyatonga Mrema, kwamba, Mrema bado ni MWANACHAMA HAI wa CCM.
Sababu iliyotolewa na mtu huyo, ambaye ni shuhuda, ni kwamba, siku Mrema alipoleleka barua yake ya "kujiuzulu" uanachama wake ndani ya CCM, barua hiyo - kama ilivyo desturi - HAIKUAMBATANA na kadi ya uanachama wa CCM. Kimsingi, kadi haikurejeshwa CCM.
Mtu huyo ambaye alinieleza mambo mengi, aliniambia kwamba, Mrema alifanya hivyo baada ya kuafikiana na uliokuwa uongozi wa wakati huo wa chama cha NCCR-Mageuzi, kwamba, pindi "atakapojiuzulu" kutoka CCM, atapokelewa ndani ya NCCR-Mageuzi kama Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho cha upinzani.
Nyote mmekuwa mashuhuda wa jinsi Mrema alivyokivuruga CCM, na kurukia TLP, ambako mpaka leo, chama hicho kiko TAABANI!
Kimsingi, Mrema ni MAMLUKI wa CCM, aliyetumwa kufanya kazi ya KUUVURUGA UPINZANI akiwa ndani ya vyama hivyo, si nje yake.
Nitaendelea kuchokonoa pindi itakapowekezekana.
---> Mchokonozi
A luta continua!