Augustine Lyatonga Mrema BADO ni Mwanachama Hai wa CCM

Augustine Lyatonga Mrema BADO ni Mwanachama Hai wa CCM

Mchokonozi

Member
Joined
Nov 17, 2009
Posts
15
Reaction score
0
Mimi ni mgeni hapa, lakini nimeona nianze post yangu ya kwanza kwa habari hizi njema kwenu.

Nimepata habari kwa mtu ambaye alikuwa karibu sana na Mhe. Augustine Lyatonga Mrema, kwamba, Mrema bado ni MWANACHAMA HAI wa CCM.

Sababu iliyotolewa na mtu huyo, ambaye ni shuhuda, ni kwamba, siku Mrema alipoleleka barua yake ya "kujiuzulu" uanachama wake ndani ya CCM, barua hiyo - kama ilivyo desturi - HAIKUAMBATANA na kadi ya uanachama wa CCM. Kimsingi, kadi haikurejeshwa CCM.

Mtu huyo ambaye alinieleza mambo mengi, aliniambia kwamba, Mrema alifanya hivyo baada ya kuafikiana na uliokuwa uongozi wa wakati huo wa chama cha NCCR-Mageuzi, kwamba, pindi "atakapojiuzulu" kutoka CCM, atapokelewa ndani ya NCCR-Mageuzi kama Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho cha upinzani.

Nyote mmekuwa mashuhuda wa jinsi Mrema alivyokivuruga CCM, na kurukia TLP, ambako mpaka leo, chama hicho kiko TAABANI!

Kimsingi, Mrema ni MAMLUKI wa CCM, aliyetumwa kufanya kazi ya KUUVURUGA UPINZANI akiwa ndani ya vyama hivyo, si nje yake.

Nitaendelea kuchokonoa pindi itakapowekezekana.

---> Mchokonozi

A luta continua!
 
Mchokonozi Junior Member
red_left.png
red.png
red_right.png
green_left.png

green.png

green_right.png
Join Date: Tue Nov 2009
Posts: 5
Thanks: 0
Thanked 1 Time in 1 Post
Umetumwa na nani ?.
 
Hivi mtu ukihama chama kadi unarudisha au unaipeleka kule kwenye chama chako kipya..kisha nauliza nitajie kiongozi gani wa upinzani uliyerudisha kadi yake CCM
 
Una maana gani unaposema bado ni mwanachama hai? Ni wakati gani mwanachama anatangazwa kuwa sio hai? Naomba majibu tafadhali.
 
Mchokonozi Junior Member

red_left.png
red.png
red_right.png
green_left.png

green.png

green_right.png
Join Date: Tue Nov 2009
Posts: 5
Thanks: 0
Thanked 1 Time in 1 Post
Umetumwa na nani ?.

Mkuu Ngongo uliposema kwenye thread nyingine kuwa wako wengi humu sikukuelewa, duh
 
Hata Mzee Liundi, Msajili wa zamani wa vyama vya siasa, amewahi kukaririwa hivi karibuni alisema CCM ilikuwa inapandikiza mamluki ndani ya vyama vya upinzani, na kwamba anawafahamu wengi. Bila shaka Lyatonga ni mmojawapo. Sitashangaa.
 
Makamba , naye ni CHADEMA alitumwa CCM kufanya kazi maalum na ikimalizika atarejea CHADEMA.
 
Hata Mzee Liundi, Msajili wa zamani wa vyama vya siasa, amewahi kukaririwa hivi karibuni alisema CCM ilikuwa inapandikiza mamluki ndani ya vyama vya upinzani, na kwamba anawafahamu wengi. Bila shaka Lyatonga ni mmojawapo. Sitashangaa.

Kumbe bado unamashaka baki na mashaka yako yatakusaidia siku za usoni.Mnapokosa mambo ya kusema mnakimbilia ohoo huyu CCM mara bado hajarusha kadi,hata Kafulila bado hajarudisha kadi lakini si mwanachama wa Chadema.

L A Mrema kawapeleka puta mnaanza kelele na bado subirini 2010 mtajua yeye ni nani.
 
kurudisha kadi ya chama sio ishu..mbona wengi mimi sijaona wakirudisha kadi,makongoro,lamwai bagenda na kadhalika hawajarudisha kadi.kimaro mwenyewe hajarudisha kadi ya nccr.siku nyingine fikiria hoja zako kama ni za kipuuzi usiziweke huku ambzzo hazina msingi,
 
Mchokonozi Junior Member

red_left.png
red.png
red_right.png
green_left.png

green.png

green_right.png
Join Date: Tue Nov 2009
Posts: 5
Thanks: 0
Thanked 1 Time in 1 Post
Umetumwa na nani ?.

why everytime you guys are discriminating junior/new members?

You need to answer his/her post accordingly, if his wrong,just educate him.You do not have time, read other threads.

People think differently, is not everytime that new post(ideas) means katumwa.Doing this we are scaring other member to start new threads.

There are many people outthere whom we need their ideas, and they may have the best ones than anybody here(for teaching us) they may the worst ones( to teach them)
 
Tunaelekea kupigwa bao na mafisadi tumebaki na mizaha tu!
 
Ni haki yake mbona wapo wengi wa aina hiyo,wana kadi mbili mbili,wengi za cuf na ccm- siasa za nchi hii wizi mtupu????
 
Hizza Tambwe,Naila Jidawi,Dr Rutta,Guninita,Salim Msabaha na hivi juzi Kafulila wametangazwa wapi kama walirudisha kadi ya chama pindi walipohama?Guninita,Tambwe na Msabaha sasa ni maafisa wakubwa wa chama cha CCM waliohamia kutoka CHADEMA na CUF;je kwa sababu na wao hawakurudisha kadi za vyama walipohama basi wao sio CCM?

Upupu mwingine wa kijiweni uliokuja JF;kaazi kweli kweli na mwaka huu tutayaona mengi!point yangu ya kukujibu kuwa;mtu akihama chama kurudisha kadi sio suala la msingi!
 
Mnakumbuka kwamba Mrema alihama CCM kwa "mbwembwe na kebehi nyingi...". Tulitarajia angerudisha kadi. Wangapi wanahamia CCM, kwenye mikutano ya hadhara, na wanaonekana kwenye luninga, wakikabidhi kadi zao za upinzani kwa wanaowapokea CCM? Usiporejesha kadi yako, basi wewe si mwanachama HALISI... ina maana, uko mguu mmoja ndani, mguu mmoja nje. Ama huamini unachokifanya, ama UMETUMWA kufanya kazi maalum. Tathmini yangu!

./Mwana wa Haki
 
Kama hilo lilikuwa ni deal kwani kulikuwa na shida gani mrema angerudisha kadi na alafu angegeuka nyuma kuichukua, kwa CCM na serikali yao wala sio shida,
mbona Balali amekufa lakini hajafa?
 
Mchokonozi Junior Member

Join Date: Tue Nov 2009
Posts: 5
Thanks: 0
Thanked 1 Time in 1 Post
Umetumwa na nani ?.

Nashindwa kukuelewa. Jee Junior member hana haki au hana uwezo wa ku-post thread? Kuna watu wamejoin June mwaka huu lakini wana thread nyingi na za maana kuliko member wa 2007. Tuwape moyo Junior members
 
Back
Top Bottom