Hivi mnajua CCM ilipewa kikatiba na kisheria njia nyepesi ya kuwa Chama cha Kisiasa kuliko chama kingine? CCM haikupewa masharti ambayo leo mtu anayetaka kuaznisha chama anapewa.
Lowassa, Karamagi na Chenge wakija wakakiri makosa ya Uzembe, itabidi tuwaulize, tutawaaminije?
Mfano, kila mmoja wao ana makosa lukuki ya uzembe, hivyo wao ni Wazembe period. Iweje wakitubu kwa kosa la Richmond, Buzwagi na Rada tuwasamehe? Je yale mengine ya Uzembe kama IPTL kwa Chenge tusemeje?
Mrema hakuwa na haja ya kuanzisha chama, ni pupa kutokana na mfumo wa kijamaa na kushindwa kuelewa mfumo mpya wa vyama vingi, ndio ulimfanya akakimbilia NCCR kwa ahadi ya kuwa Mwenyekiti wa NCCR na mgombea Urais kupitia NCCR.
Kama angekuwa anashaurika au kuwa na washauri wazuri wasio na pupa, leo hii tungeona Upinzani ukiwa umeshika madaraka ya nchi.
Mrema alipoondoka CCM, alipaswa kuuongeza nguvu na mshikamano ndani ya Upinzani. Tayari mwana CCM mwingine Sefu Hamadi alikuwa na Chama chake na malengo yake na hawa wawili hawafungamani.
Mrema kama angejiunga chama chochote, na kujijenga taratibu ndani ya chama kama Malecela alivyojijenga ndani ya CCM na kuijenga CCM, ingekuwa rahisi sana kwa yeye Mrema kushawishi wanachama wa chama chake kuwa anastahili kuwa mgombea urais kwa chama chao as long as chama hicho hakina mikingamo kama CCM na yaliyowapata kina Msuya, Malecela, Salim na Dr. Bilali.
Bado tuna nafasi ya kumtafuta mgombea Urais kutoka kambi ya Upinzani, alimradi kuwe na nia ya kweli ya kuleta muungano na kufanikisha azma ya kuing'oa CCM madarakani.