Augustine Lyatonga Mrema: Mpiganaji!

Augustine Lyatonga Mrema: Mpiganaji!

Mimi nami huyu ni shujaa wangu katika siasa za Tanzania. Tatizo kubwa la wanasiasa tanzania wenye majina ni woga na kukosa ujasiri wa kuthubutu kutoka CCM; ni Mrema pekee katika wanasiasa wenye majina aliyeweza hili. Tazama hata sasa hivi mtu atapiga kelele weee lakini akiamua kugombea anaishia kugombea kupitia CCM. Ukimuuliza vipi tena atakupa sababu lukuki-lakini ukiangalia kwa makini ni WOGA.

Hatujawahi kumuenzi Mrema sawasawa inavyotakiwa. It is good kwamba kuna mtu kalileta hili hapa.
 
Mkuu Kitila,

Je unafikiri Mrema anaweza kuanzisha chama kipya chenye nguvu na kikafanikiwa?
 
Mimi nami huyu ni shujaa wangu katika siasa za Tanzania. Tatizo kubwa la wanasiasa tanzania wenye majina ni woga na kukosa ujasiri wa kuthubutu kutoka CCM; ni Mrema pekee katika wanasiasa wenye majina aliyeweza hili. Tazama hata sasa hivi mtu atapiga kelele weee lakini akiamua kugombea anaishia kugombea kupitia CCM. Ukimuuliza vipi tena atakupa sababu lukuki-lakini ukiangalia kwa makini ni WOGA.

Hatujawahi kumuenzi Mrema sawasawa inavyotakiwa. It is good kwamba kuna mtu kalileta hili hapa.

Hili li CCM ni dude la ajabu sana. Wanalitukana wanalisema, lakini wapi bwana wamo tu.

Lakini nina wazo, hata katika dini zetu tuna toba, yaani mtu akikosa ama hata akiona amewakera wenzake ama Mungu analazimika kutubu na akitubu kwa dhati anasamehewa na Mungu japo kwa sisi binadamu tunashindwa kutoa msamaha wa dhati kwa kutokuwa na uelewa wa udhati wa mtu.

Baada ya utangulizi huo nina swali;

Je, Lowassa, Chenge na Karamagi wakitangaza hadharani kwamba wametubu kwa mapungufu yao ya kibinadamu na kwamba baadhi ya maamuzi yao walishinikizwa na vikao vya CCM na sasa wameona hawatakuwa wasafi kwa kuendelea kuwa ndani ya CCM na wakaondoka na kujiunga na upinzani, WATAPOKELEWA, WATASHINDA chaguzi zao?
 
Mimi nami huyu ni shujaa wangu katika siasa za Tanzania. Tatizo kubwa la wanasiasa tanzania wenye majina ni woga na kukosa ujasiri wa kuthubutu kutoka CCM; ni Mrema pekee katika wanasiasa wenye majina aliyeweza hili. Tazama hata sasa hivi mtu atapiga kelele weee lakini akiamua kugombea anaishia kugombea kupitia CCM. Ukimuuliza vipi tena atakupa sababu lukuki-lakini ukiangalia kwa makini ni WOGA.

Hatujawahi kumuenzi Mrema sawasawa inavyotakiwa. It is good kwamba kuna mtu kalileta hili hapa.

Mkuu ni kweli tupu kwa Mrema ,na kosa lake kubwa inaelekea kugombea urais ktk chama kilichoanzishwa na wenyewe.

Sasa mwalimu ktk hoja hoja yako ya ziada ya woga, sasa kila mtu anapoamua kugombea aanzishe chama chake ama ni chama kipi kinachostaili ili mgombea anayepiga kelele akagombee.

mimi nafikiri tuache ushabiki tuangalie ukweli wa mambo na hali halisi.
 
Mkuu, kwa maoni yangu hakuna sababu ya kuanzisha chama, hiyo itatupotezea muda mwingi sana. Chama mbadala tunacho tayari ni kukipa nguvu tu za hali na mali, na hasa raslimali watu-nacho ni chama cha demokrasia na maendeleo, kwa kifupi CHADEMA. Karibu(ni) sana.
 
Sawa mkuu,

Je Mrema anaweza kukubali kuwa labda tuseme mratibu wa shughuli za CHADEMA badala ya kushika nafasi za juu?
 
Sawa mkuu,

Lakini ukweli huo wa mambo ni upi na hali halisi ni ipi, unaweza kufafanua?

Ukweli halisi ni kuwa hakuna chama tawala wala pinzani kilicho na demokrasia ya kweli ndani yake nawala kilicho na nia madhubuti ya kweli ya kuwaondolea wananchi kero zao hapa nasema CHAMA kama CHAMA. na sio mtu binafsi.

Ukweli wa mambo ni kuwa ukipitishwa na chama cha ccm unakuwa na asilimia 65 ya kuwa mbunge hasa ktk majimbo mengi na hatimaye MTU kama MTU /Mbunge kama Mbunge kuwatetea wananchi.

Haya ya chama mimi simo ktk imani hiyo.
 
Hivi mnajua CCM ilipewa kikatiba na kisheria njia nyepesi ya kuwa Chama cha Kisiasa kuliko chama kingine? CCM haikupewa masharti ambayo leo mtu anayetaka kuaznisha chama anapewa.

Lowassa, Karamagi na Chenge wakija wakakiri makosa ya Uzembe, itabidi tuwaulize, tutawaaminije?

Mfano, kila mmoja wao ana makosa lukuki ya uzembe, hivyo wao ni Wazembe period. Iweje wakitubu kwa kosa la Richmond, Buzwagi na Rada tuwasamehe? Je yale mengine ya Uzembe kama IPTL kwa Chenge tusemeje?

Mrema hakuwa na haja ya kuanzisha chama, ni pupa kutokana na mfumo wa kijamaa na kushindwa kuelewa mfumo mpya wa vyama vingi, ndio ulimfanya akakimbilia NCCR kwa ahadi ya kuwa Mwenyekiti wa NCCR na mgombea Urais kupitia NCCR.

Kama angekuwa anashaurika au kuwa na washauri wazuri wasio na pupa, leo hii tungeona Upinzani ukiwa umeshika madaraka ya nchi.

Mrema alipoondoka CCM, alipaswa kuuongeza nguvu na mshikamano ndani ya Upinzani. Tayari mwana CCM mwingine Sefu Hamadi alikuwa na Chama chake na malengo yake na hawa wawili hawafungamani.

Mrema kama angejiunga chama chochote, na kujijenga taratibu ndani ya chama kama Malecela alivyojijenga ndani ya CCM na kuijenga CCM, ingekuwa rahisi sana kwa yeye Mrema kushawishi wanachama wa chama chake kuwa anastahili kuwa mgombea urais kwa chama chao as long as chama hicho hakina mikingamo kama CCM na yaliyowapata kina Msuya, Malecela, Salim na Dr. Bilali.

Bado tuna nafasi ya kumtafuta mgombea Urais kutoka kambi ya Upinzani, alimradi kuwe na nia ya kweli ya kuleta muungano na kufanikisha azma ya kuing'oa CCM madarakani.
 
Hivi wakulu mimi naomba kuuliza swali, je ni nani wanaunda "political establishment" ya Tanzania?

Kwa uzoefu wangu na nchi zenye demokrasia ya kweli nnaona kwamba ili chama mbadala kiweze kupewa ridhaa ya kuongoza na wapiga kura "provided" kwamba chama tawala kimelegalega, political establishment ni lazima pia wapitishe chama hicho na kipewe kuongoza nchi.

Je kwa Tanzania ni nani anaweza kuamua kwamba chama mbadala ni lazima kwa mfano-uchaguzi wa 2010 ukiachilia wapiga kura?
 
Richard,

Tanzania hakuna Political Establishment. Kama tungekuwa nayo, ungeona unyoofu wa vyama na kupungua kwa utitiri wa vyama.

CCM ni wajanja, waliweka masharti rahisi kuruhusu uundwaji wa vyama badala ya kuweka masharti magumu ambayo yangekuwa ndiyo msingi wa Political Establishment.

Leo hii, mtu akikasirika kuwa haelewani na Mrema, Lipumba au Kikwete, ni rahisi kwenda kuanzisha chama na anahitaji watu kadhaa na shahada (sugnature) kadhaa ili apewe hati ya kuwa chama cha siasa.

Hii inasababisha kuchuja (dilute) kwa mfumo wa kisiasa ambao huzaa vyama utitiri visivyo na muelekeo na kuvunja nguvu za kuwa na strong political establishment.

CCM wamefanikiwa kwa kuwa manipulative kwa hili na hasa ugawaji wa ruzuku.

Ukiondoa vyama vichache vikubwa kama CUF na CHADEMA, vyama vingine ni dhaifu na havieleweki vina sera gani zaidi ya kuwa na watu wenye majina. Na hili ndio kosa la Mrema alipotoka NCCR na kukimbilia TLP.

Vyama kama DP, UDP, TLP, NCCR, NRA na vinginewe, vinapaswa ama kujifuta au kuungana na kuwa chama kimoja kama si kujiunga na CUF na CHADEMA kama vina nia ya kuwa wapinzani wa CCM na sera zake.
 
Rev.Kishoka,

Nimekuelewa lakini mimi nafikiri "political establishment" ya Tanzania ipo ila ipo "detached" na jamii ya watanzania ambao ndio wapiga kura.

Uwezo wake wa kuleta mabadiliko ambayo ndio Raisi Kikwete akisema ya Kasi Mpya, nguvu Mpya na Ari Mpya haupo na haiwezekani kufanya hivyo kwa sababu kuna "high degrees of endogamy," na hii inaonekana katika jamii nzima ya watanzania.

Nikitumia neno hili la "endogamy" nnaliweka katika jamii yetu sisi watanzania ambapo utakuta mambo hayaendi mbele interms of maendeleo kwa sababu za UFISADI, RUSHWA na kadhalika- yaani kunakuwa hakuna social mobility na badala yake ni watoto wa wachache ndio wanasonga mbele kwenye ulaji na kuwaacha wengi wakiishia elimu ya sekondari.

Kwenye zile familia za wale "Elite" ndio utaona biashara, mitandao na mambo mengine yanashika tama na kuzuia jitihada za kuleta maendeleo kwa demokrasia ya kweli kwa watanzania wengi maskini na wapiga kura.

Kwa hio mfumo wa siasa uliotengenezwa na "political establishment" ndio umekuwa co-opted na wale elites na kutokana na low levels ya wananchi kujishirikisha na kuwa active kwenye siasa matokeo yake ndio tunayaona.
 
Kuna Vacuum kubwa sana katika katiba ya Tanzania ndio maana huwezi kuona kuwa Demokrasia ya kweli na pia hata kama watu kama wakina Mrema but CCm watajaribu kuona kuwa vyama Makini na watu makini wahajiungi na vyama, Tazama hata mswada wa sheria ambayo inakataza siasa kwenye vyuo Vikuu, Je viongozi wa taifa letu kesho wataanzia wapi kama sio Vyuoni?? Kuna Ulazima wa hawa Jamaa wanajiita Makamanda wa Ufisadi kutoka ndani ya chama Chao na kujiunga na Upinzania
 
Richard,

Jana nikilonga na Mzee Mwanakijiji, tuliongelea mizizi ya Rushwa na Ufisadi ilivyokomaa Tanzania na ni jinsi gani itakuwa ni vigumu kuondoa Ufisadi kwanza ili kuleta maendeleo .

Tanzania kuna kile kitu tulichozoea cha kuulizana " Una kiasi gani? unahitaji kiasi gani? zungumza basi! " kama salamu ya mtu kupata haki yake au mahitaji.Naye anayeulizwa swali hilo, hulijibu bila woga au aibu.

Sasa ni kutokana na kukomaa kwa mfumo huu, ni rahisi kwa Political Establishment ikawa selective na kurithishana kwa manufaa yao.
 
Mimi nafikiri hiyo rushwa ni tatizo dogo sana hasa akipatikana Rais mwenye dhamira ya kweli na aliye na huruma mbele ya wananchi wake.Nafikiri hivyo vingine ni viungo tu.

Mimi nafikiri pia hapa hatuhitaji chama ila tunachohitaji ni maisha bora, wengi wanaokomaa na vyama japo si wote wanafanya hivyo hivyo kulazimisha chama maana watanufaika moja kwa moja wao binafsi na kubadili kutoka FISADI wa ccm na kuingia FISADI wa chama XX
 
Wakuu,

Kama mnakumbuka uchaguzi wa raisi nchini Marekani, walianza na kura za maoni ambapo Republicans na Democrats ndio wanajulikana zaidi.

Mimi kwa upande wangu nilkuwa naangalia ni jinsi gani political establishment itaamua kupata raisi mwingine mbadala wa George Bush.

Ndio tukaona "Obama surge" ambapo mwanasiasa huyu alionekana na political establishment kuwa na uwezo wa kubadili upepo. Lakini hali hii unaweza kuichambua katika sehemu mbili ya kwanza, kwamba watu na wapiga kura wote wanaelewa umuhimu wa matatizo yaliyopo kwenye political system na kuwa tayari kubadili mawazo.

Pili ni kwamba sera za maendeleo zimekaaje na zinashughulikiwa vipi na zinashabihiana vipi na mfurukuto ndani ya "political establishment."

Sasa kutokana na mambo hayo mawili ndio tukaona kwamba Obama ana sera ya kuleta mabadiliko na sera hio ikakubalika katika Marekani nzima na mamilioni ya wapiga kura wakajitokeza katika kampeni na hasa vijana wakawa na "desire" au mshawasha wa kutaka mabadiliko muhimu ya kijamii na kisiasa.

Kwahio "political establishment" ianweza kuamua kubadili mfumo wa siasa Tanzania na kusema kwamba sasa tunataka mtu wa kuleta mabadiliko na yakatokea na ikawa kuweka sura mpya kwenye fundamentally reactionary policies na institutions kama mahakama, polisi na zingine zinazofanana na hizo.
 
mie nafikiri mambo makubwa mawili yaliofanya wananchi wapoteza imani na mrema ni tamaa yake ya madaraka japo kuwa angekuwa kiongozi mzuri sana na pia propaganda ya kwamba bado alikuwa ccm kaja kubomoa upinzani.na kuhusu kuja kubomoa upinzani kuna matukio yake mengi ambayo yalikuwa yanafanya hilo swala kwamba bado yuko ccm kuonekana kweli.
sasa hivi ni too late tumepoteza kiongozi mzuri sana namshauri agombee ubunge.
 
Ninauhakika Mrema bado ana nafasi ya pekee sana. Katika Project X mojawapo ya mambo tunayoangalia ni nani atampinga JK mwakani kwa ufanisi mkubwa. Huyu tutamtengeneza na mojawapo ya majina matatu tunayoyaangalia ni la Mrema.
 
Kwanini?? mzee wangu Mwanakijiji?? Mrema labda kwa kuwa haiba yake katika jamii imepungua sana katika machoni kwa Watanzania lakini kuna maneno ya street kuwa ni Pandikizi toka CCM!! Hayo mengine ni Wakina nani??
 
haiba ya Mrema imepungua kwa jamii kwa sababu tumeamini uongo juu yake; tumekuwa kama wale wote waliopewa uchaguzi kati ya Baraba au Yesu...
 
Back
Top Bottom