Augustine Lyatonga Mrema: Mpiganaji!

kamakabuzi said:
Si utoroshaji ulikuwa na vibali vya wakubwa wake? Kumbuka wanyama waliosafirishwa hai kwenda uarabuni, si aliwakamata lakini wakawa wa vibali toka ikulu?
Maovu kama hayo ndiyo yalimsukuma kukataa collective responsibility na kutoka serikalini!

kamakabuzi,

..Mrema hakuelewana na wenzake ktk suala la Chavda, lakini zaidi inaelekea hakufurahia kile kitendo cha kuvuliwa "Unaibu Waziri Mkuu" na pia kuhamishiwa wizara ya Kazi.

..lakini pia najiuliza hivi kwa akili zake yeye aliona ni lazima lazima lazima awe Waziri wa Mambo ya Ndani? mbona wizara ya Kazi ina matatizo mengi na hatukumsikia akishughulikia suala lolote lile?

..vilevile kule kwao maeneo ya Moshi ni kati ya mipaka iliyokithiri kwa kuingiza bidhaa za kimagendo bila kulipa ushuru. hatukuwahi kusikia Mrema amekwenda kuzuia magendo yaliyokuwa yakipitishwa mkoani kwake na hata jimboni kwake mwenyewe.

..Mrema kazi yake ilikuwa ni kuwasumbua wahindi wa mjini ambao kwa kweli ni easy targets.

..halafu wale wafanyabiashara aliokuwa akienda kumalizana nao kuhusu masuala ya kodi kule Kiraracha ilikuwa namna gani? hivi hawakuwa wakimpa kitu chochote kweli? hivi ni nani alimpa madaraka ya kupindisha sheria zetu za kodi kiasi kile?
 
fmes

mrema hakusoma lakini ameweza kuweka vituo vya polisi karibu na wananchi, na wakati wa mrema vituo vingi vya polisi vilijengwa nchini...

naomba unitajie mawaziri waliosoma waliopita baada ya mrema na impact zao katika TZ, sio lazima wawe kwenye wizara ya mambo ya ndani..

mrema ameacha makucha yake au legacy (vituo vya polisi karibu na wananchi), je hao waliosoma wameacha legacy gani????????

kinachoitajika ni mtu ambaye ni mtendaji na mwenye dhamira ya kutenda kwa manufaa ya waTZ, hata kama akiwa na ajenda yake ya kuadvance politicallly ilimradi waTZ wanufaike. By the way kila mwanasiasa huwa anataka kuendelea kisiasa, kuna wanataka kuendelea on merits na kuna wanatoka kuendelea kwa mtandao(hii ndiyo iliyoko TZ, hamna merits).

note: prof/dr sio kipimo cha utendaji, hawa ni ma academics, hata ukiangalia cabinet nyingi za nchi za nje utakuta hamna ma prof/dr wengi kama ilivyo TZ. TZ imekuwa na tabia ya kujaza ma prof/dr wengi ambao hawana policy zozote zile na hawajaleta mabadiliko yeyote yale.
 
 
 
 
 
 


..Joka kuu inabidi uache story za vijiweni ili watu tuendelee kusoma unachoandika la sivyo next time tutakuwa tunakupita tuu!
 

Big up Bro; Alitaka kuwepo na wenye mtizamo kama yeye lakini hakuna hata mmoja aliyejitokeza, uoga na unafiki pia uzindaki wabunge wetu walionao.
 
-
- Assumption kwamba an-ignorant man like Mrema anaweza kutuokoa as a nation na kwamba we need a man of his ignorance level, ni an insult kwetu wananchi wote wa Tanzania,
FMEs!

...mlionao nao sasa AKA smart CCM mafisadi wamewafikisha wapi? zaidi ya kuwaongezea njaa,ujinga,umaskini wa kutupa,foleni na magonjwa yanayotibika yakiua mamilioni kila mwaka.....viongozi walioshindwa hata kusign mkataba wa kuzalisha umeme unaona ni bora kuliko Mrema? viongozi wanaogawa dhahabu ya mabilioni kwa upumbavu wa kutoelewa nini maana ya free market...................................
 

ni kweli mwambie MKULU FMES..

UKWELI ni kuwa kuna tofauti kubwa sana kati ya elimu na busara ya uongozi....

kwanza lazima mjuwe hofu ya mrema kuwa rais ndio iliwafanya ccm waweke kipengele cha degree kwenye kazi ya urais...kalini hicho kipengele hakina maana yeyote!!!

mrema alikuwa very charismatic na tishio...alikuwa ana damu ya kupendwa ....nakumbuka enzi zile tulienda uwanja wa ndege wakati mzee mwinyi rais na mrema ni naibu waziri mkuu..unaweza hata kucheka,ukipangwa msafara kuelekea ikulu kwenye gari la wazi na rais mgeni...ukipita maeneo ya mkusanyiko ...vingunguti,buguruni ....uhuru...ilikuwa inawashangaza hata viongozi wageni kwani wananchi walikuwa hawawashangilii...lakini wakishapita ...wanasikia kelele nzito nyuma[nadhani walikuwa wakifikiri watanzania wanachukua dakika moja kufanya utambuzi kichwani na kuanza kushangilia]....kifupi baadaye ilibidi mrema awe gari lake linapangwa nyuma kidogo ya gari la rais ....ili kuondoa hisia za yeye kushangiliwa na rais kuachwa...mzeee mwinyi hakuwa na tabu hata kidogo na umaarufu wa mrema ..na alimkubali ...isitoshe aliposimamishwa kazi miaka ile walikuwa na mrema....ambaye umaarufu wa mrema ulikuwa ukimkera ni waziri mkuu cleopa msuya....kwani wananchi hawakujuwa hata kama yeye yupo...na hata aliye engneer kwa kiasi kikubwa mrema kuondolewa unaibu ni cleopa baada ya kumlalamikia mwinyi kuwa hawezi kufanya kazi naye[nadhani zilikuwa siasa za urais wa 1995].

Wakuu tukirudi kwenye elimu..dunia imeshuudia viongozi wazuri tu wenye elimu za kawaida..tukianza na hapa nyumbani ..mzee mwinyi hakuwa graduate[ana diploma ya uwalimu wa kingereza], mrema ana diploma ya uwalimu [ ana diploma ya masuala ya ujasusi na propaganda ya east europe,huwa haitajwi sana].., ,ukienda hapo kenya MOI ana diploma ya ualimu tu ..na walimuita profesa wa siasa[alimudu kuishika nchi pamoja kuliko mchumi kibaki]

nenda uingereza ...john major ...hakuwa msomi[kwenye nchi ya wasomi],marekani regan [one of favourites presidents-hakuwa msomi]..and the list is long....,tuache hapo south africa ambapo Zuma ..zaidi ya elimu ya uzoefu kazini ya kijasusi [russia] -only field training ..hana elimu ya kawaida ya darasani....

tofauti waliyonayo viongozi wenye elimu ndogo ambayo inawasaidia ni usikivu....wanawasikiliza wananchi na washauri kuliko hisia zao...na mara nyingi huwasaidia kuliko wasomi ambao hujiona wanajuwa !!
 
philemon u r right,ujue angalia let say entrepreneur aliefanikiwa ukiambiwa chanzo chake unaweza toa machozi,wengi wao si wasomi,but wanafight kupata kile wanachotaka.Msomi akiongoza hata mabo yasiyohitaji analyisis utakuwa unaanalyse kwa saanaaaa hatimaye unaishia ktk makaratasi bila kutenda,risk assesment utaambiwa,au hakuna tija,but moderate elimu aningia kichwa kichwa unakuta mabo yanaenda mbele!watu wa aina hii wanatakiwa wawe top then chini yao wawepo wasomi!! huko nchi zilizoendelea sijasikia mwnasiasa pasee ati Prof,Dr, High proffesionals!! kama wapo ni wachache sana,na utakuta ni ps or military scholars, sio huku daktari,engineer,mwalimu,mjeshi woote ni wanasiasa
 
Wasomi wengi wa tz, (sio wote) wanakariri vitabu vya wenzao tu na kuiba mitihani lakini hawajaelimika. Fuatilia wanachoongea viongozi wanajiita Dr utashangaa hizo Phd walipataje.

Mrema anaweza kuwa hajasoma kwa sababu tu alikosa nafasi lakini uwezo wake kuongoza ni mkubwa. Unakumbuka ubunifu wake kupambana na majambazi, vituo vya polisi alivyojenga kwa kumobilze nguvu za wananchi ndivyo vinatumika hadi leo na hata serikali haijaweza kuongeza. Mauaji na ujambazi mkoani Mara vilikua vimekithiri lakini mrema alitoa siku saba kurejesha silaha vituo vya polisi na wakuria wakasalimu amri bila ubishi. toka hapo uhalifu ulipungua mpaka unapoanza tena sasa hivi.
 

PM:

Elimu ni neno pana sana. Elimu ya form six pekee yake ni sawa elimu ya mwaka wa kwanza chuo kikuo. Na katika nchi zingine ni sawa na elimu ya mwaka wa kwanza na wapili.

Hivyo diploma za Mzee Mwinyi, Moi, Odinga, na hata ya hile Nyerere aliyotoka nayo Makerere zilikuwa na kiwango ambacho kiko kati elimu ya kidato cha sita na digrii ya kwanza.

Pamoja na hayo wapo wanaopenda kujisomea, kujiendeleza na kujifunza kutoka kwa wenzao.

Sifa hizi Mrema hana. Nafasi alizopewa wakati wa Mwinyi na umaarufu aliokuwa nao, angejifunza mengi. Lakini hakuonyesha hilo.

Kwanza hakujifunza umuhimu wa sheria. Maamuzi yake yalitokana na emotions zake.

Na washabiki wake wengi aliotupa kipindi kile, tulikuwa hatujuhi sheria au umuhimu wa kupiga kura.
 
- Mkulu Semilong, naona this time tutajadili ishus tu, haya Mrema alijenga hivyo vituo wapi hasa mkuu hebu angalau vitaje kumi tu mkuu? Halafu hivyo vituo vimefanya nini hasa katika kupunguza uhalifu nchini under Mrema na sasa?
FMEs!
unataka nianze kukuhesabia vituo (kwa kweli huu utakuwa ni ubishi, na ninashangaa sana mtu kama wewe kujidai hujui kuwa mrema alijenga vituo)
kuhusiana na uhalifu uliopo sasa mrema ametoka kwenye system siku nyingi sana, matatizo ya kina zombe, masha, kapuya,mwema unataka kumletea mrema


- If that is the case si Muungwana ametoa mabillioni, eti hebu niambie effective yake kwa maisha ya kila siku kwa wananchi masikini?
hayo ni matatizo ya muungwana siyo ya mrema, kipindi cha mrema ujambazi ulipungua kwa kasi sana, tokea mrema aondoke miaka mingi sana imepita


kuhusu kusoma sina haja ya kuyarudia aliyoyasema mikaeli hapo juu zuma regan et al
ingekuwa ulaya mrema asingeingilia kwa ajili mahakama ingewashuhulikia, mahakama za ulaya zinaendeshwa kwa sheria na haki, kesi kubwa kwenye mahakama za bongo zinaendeshwa na viongozi, mfano kikwete alivyoliambia taifa juzi kuwa vigogo wengine watafikishwa mahakamani - ni kielelezo tosha kuwa kigogo hawezi kuguswa bila kikwete ku-approve.


note: usifananishe mahakama/kesi za bongo na za ulaya, katika mahakama/kesi za bongo viongozi wanainfluence kubwa sana
 

Mkuu PM uchambuzi mzuri sana ingawa naelewa kuna wachangiaji wanakuelewa sana sema watapenda kuweka ligi tu ilimradi wanataka waonekane wanachangia.

Ronald Reggan alikuwa mcheza picha wakawaida,John Major wa Uk alikuwa Bank teller,wote wanatoka katika nchi zenye wasomi wengi.Tukija Africa Mzee Moi na Mzee ruksa.

Hizi habari sijui diploma ya Mwl ilikuwa juu kuliko aliyosoma Mrema bila shaka ni sehemu ya propaganda tulizolishwa ktk uchaguzi wa mwaka 1995.

Tanzania inahitaji kiongozi anayetoa maamuzi mazito kwaajili ya maendeleo ya nchi na si kuuza sura na kulea mafisadi kwa kisingizio chochote.
 
Last edited:
Ukiachia baba wa taifa, vongozi wengine waliojituma kutimiza wajibu wao kwa faida ya Mtanzania ni Sokoine na Mrema.

Tatizo la Watanzania huwa ni wivu na kila mwenye mafanikio kidogo tunampaka matope.

Mashujaa wangu Tanzania ni Nyerere, Sokoine na kisha Mrema, mawaziri wakuu wengine wote walikuwa wahuni tu.
 
Mkuu FM
Kati ya wanajamvi wanaonivutia kwa hoja zilizo simama wewe ni mmoja wapo.
Bilashaka kuna jamaa kaiba password yako,umekuwa chini ya viwango katika hii hoja kwa kiwango cha kutisha.
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…