jmushi1
Platinum Member
- Nov 2, 2007
- 26,329
- 25,263
ni kweli mwambie MKULU FMES..
UKWELI ni kuwa kuna tofauti kubwa sana kati ya elimu na busara ya uongozi....
kwanza lazima mjuwe hofu ya mrema kuwa rais ndio iliwafanya ccm waweke kipengele cha degree kwenye kazi ya urais...kalini hicho kipengele hakina maana yeyote!!!
mrema alikuwa very charismatic na tishio...alikuwa ana damu ya kupendwa ....nakumbuka enzi zile tulienda uwanja wa ndege wakati mzee mwinyi rais na mrema ni naibu waziri mkuu..unaweza hata kucheka,ukipangwa msafara kuelekea ikulu kwenye gari la wazi na rais mgeni...ukipita maeneo ya mkusanyiko ...vingunguti,buguruni ....uhuru...ilikuwa inawashangaza hata viongozi wageni kwani wananchi walikuwa hawawashangilii...lakini wakishapita ...wanasikia kelele nzito nyuma[nadhani walikuwa wakifikiri watanzania wanachukua dakika moja kufanya utambuzi kichwani na kuanza kushangilia]....kifupi baadaye ilibidi mrema awe gari lake linapangwa nyuma kidogo ya gari la rais ....ili kuondoa hisia za yeye kushangiliwa na rais kuachwa...mzeee mwinyi hakuwa na tabu hata kidogo na umaarufu wa mrema ..na alimkubali ...isitoshe aliposimamishwa kazi miaka ile walikuwa na mrema....ambaye umaarufu wa mrema ulikuwa ukimkera ni waziri mkuu cleopa msuya....kwani wananchi hawakujuwa hata kama yeye yupo...na hata aliye engneer kwa kiasi kikubwa mrema kuondolewa unaibu ni cleopa baada ya kumlalamikia mwinyi kuwa hawezi kufanya kazi naye[nadhani zilikuwa siasa za urais wa 1995].
Wakuu tukirudi kwenye elimu..dunia imeshuudia viongozi wazuri tu wenye elimu za kawaida..tukianza na hapa nyumbani ..mzee mwinyi hakuwa graduate[ana diploma ya uwalimu wa kingereza], mrema ana diploma ya uwalimu [ ana diploma ya masuala ya ujasusi na propaganda ya east europe,huwa haitajwi sana].., ,ukienda hapo kenya MOI ana diploma ya ualimu tu ..na walimuita profesa wa siasa[alimudu kuishika nchi pamoja kuliko mchumi kibaki]
nenda uingereza ...john major ...hakuwa msomi[kwenye nchi ya wasomi],marekani regan [one of favourites presidents-hakuwa msomi]..and the list is long....,tuache hapo south africa ambapo Zuma ..zaidi ya elimu ya uzoefu kazini ya kijasusi [russia] -only field training ..hana elimu ya kawaida ya darasani....
tofauti waliyonayo viongozi wenye elimu ndogo ambayo inawasaidia ni usikivu....wanawasikiliza wananchi na washauri kuliko hisia zao...na mara nyingi huwasaidia kuliko wasomi ambao hujiona wanajuwa !!
Mkuu uwezo wako wa kupambana na propaganda ni mkubwa,yote uliyoyasema ni kweli tupu!Mrema si tu kuwa ni mpiganaji,bali mpiganaji halisi,na CCM naona bado wakimfikiria hawapati usingizi,tumepata fagio jipya ila la zamani kamwe hatutalitupa maana linajua kona zote za nyuma...Long live Lyatonga mzee wa inji hii...!Na muencourage kuwa mapambano yanaendeleaa!