Augustine Okrah, winga bora zaidi katika soka la Tanzania kwa sasa

Augustine Okrah, winga bora zaidi katika soka la Tanzania kwa sasa

Execute

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2022
Posts
3,000
Reaction score
7,336
Huyu jamaa alisajiliwa kimyakimya na hata gharama za ujio wake hazikuwekwa wazi.

Ameonesha kuwa ni winga mwenye makali ya kimataifa. Ana kasi, pasi za upendo, anaona nafasi katikati ya msitu wa mabeki na ni mpambanaji.

Katika muda mfupi aliopo Simba amefanya wachezaji wengi sana waliopita hapo kusahaulika kwa haraka.

Nuru inaangaza kwa siku zijazo.
 
Kwangu sipendezwi na Mgunda anavyomtumia, kumchezesha kule winga ya kushoot anamfanya asiweze kufanya baadhi ya mambo, kule hawezi kukata kuingia ndani, mguu wake unamfanya akimbie pembeni apige krosi tu, kule ni mwendo wa kupiga krosi tu. Ila angekuwa upande wa kulia anaweza kuingia ndani, kucurve, kushoot na options kibao.
 
George job aliwahi kusema pale wasafi.

"Okrah ni mchezaji wa daraja la juu kidogo ya Miquissone"

Though hajatupa kile Miquissone alitupa uwanjani ila anaonekana ni mchezaji haswa. Mind you tarehe 23 utopolo lazima afe.
Tar 23/10/2022

Kwa nijuavyo mashabiki wa Simba mtaanza kutukana humu jamvini, hapo mshaloa si chini ya 3
 
Kwangu sipendezwi na mgunda anavyomtumia, kumchezesha kule winga ya kushoot anamfanya asiweze kufanya baadhi ya mambo, kule hawezi kukata kuingia ndani, mguu wake unamfanya akimbie pembeni apige krosi tu, kule ni mwendo wa kupiga krosi tu. Ila angekuwa upande wa kulia anaweza kuingia ndani, kucurve, kushoot na options kibao.
Very good comment
 
Mpira wa siku hizi anayetumia mguu wa kulia anakaa kushoto na anayetumia mguu wa kushoto anakaa kulia.

Angalia Messi, Salah, Saka au kipindi kile Arjen Robben, wote wanacheza kulia. Halafu Ronaldo au Henry wanakaa kushoto enzi zile wanacheza kama winga.

Pengine baada ya muda Okrah pia atazoea.
 
Luis akija sakho ndio atatakiwa kumpisha jumla.
Nakubaliana nawe mkuu, dogo katukosesha goli la pili la wazi jana, alipenetrate vizuri akashindwa kutoa pass kwa mwenzake aliyekuwa na nafasi nzuri zaidi yakushinda
 
Mpira wa siku hizi anayetumia mguu wa kulia anakaa kushoto na anayetumia mguu wa kushoto anakaa kulia.

Angalia Messi, Salah, Saka au kipindi kile Arjen Robben, wote wanacheza kulia. Halafu Ronaldo au Henry wanakaa kushoto enzi zile wanacheza kama winga.

Pengine baada ya muda Okrah pia atazoea.
Kwa hiyo umekubaliana na mtoa maoni au haujakubaliana na mapendekezo yake? Sio kwa ubaya
 
Tar 23/10/2022

Kwa nijuavyo mashabiki wa Simba mtaanza kutukana humu jamvini, hapo mshaloa si chini ya 3
Kama kawaida yao mburula, watapigwa na yanga ,tar 23 ndio watajua Wana mzoga uliopata faida ya kucheza na viwete, bullets na agost iliyofungwa 6 na namungo
Yanga imekutana na timu ngumu Al hilal ilitingwa fainali 3 za club bingwa na CAF
Tar 23 Kuna dhahma inaenda kutokea
 
Kwa hiyo umekubaliana na mtoa maoni au haujakubaliana na mapendekezo yake? Sio kwa ubaya
Mkuu mimi nimeelezea fact iliyopo kwenye soka la kimataifa. Itapendeza endapo Okrah atawekwa kwenye nafasi inayomfanya aisaidie timu kwa mafanikio zaidi. Sasa hapo tunamwachia kocha.
 
Kama kawaida yao mburula, watapigwa na yanga ,tar 23 ndio watajua Wana mzoga uliopata faida ya kucheza na viwete, bullets na agost iliyofungwa 6 na namungo
Yanga imekutana na timu ngumu Al hilal ilitingwa fainali 3 za club bingwa na CAF
Tar 23 Kuna dhahma inaenda kutokea
Badala ya kushughulikia matatizo kwenye timu yenu mnaleta visingizio na sababu za kitoto. Mtaendelea kuishia hatua za awali maana ni wapumbavu msiotaka kujifunza kwa waliofanikiwa.
 
Mkuu mimi nimeelezea fact iliyopo kwenye soka la kimataifa. Itapendeza endapo Okrah atawekwa kwenye nafasi inayomfanya aisaidie timu kwa mafanikio zaidi. Sasa hapo tunamwachia kocha.
Nimekupata,kweli jamaa kwa Uwezo alio nao nikuwa hatuja mfaidi,hatujavuna Uwezo wake,hatujaexploit potential. Ni kama ununue bus halafu ulipeleke route zisizo na wateja,hutalifaidi.

Kwa hisia zangu kuna wakay ukimuangalia ni kama anawaza kuwa "sio mimi huyu,hawanijui hawa, mashabiki wasijehisi ndio Uwezo wangu"

Kama ile mechi ya Haaland vs Liverpool Community shield alikosa makosa mpaka akawa anatikisa kichwa kuwa "dah kuna watu wanahisi ndio Uwezo wangu".

Hivyo Kama ulivyosema itafutwe namba ambayo tutamfaidi
 
Back
Top Bottom