Aunty Ezekeil anasa mimba nje ya ndoa

Aunty Ezekeil anasa mimba nje ya ndoa

John Okello

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2014
Posts
459
Reaction score
207
attachment.php


Stori: waandishi wetu
Madai mazito! Pamoja na kutumia nguvu kubwa kukanusha kwa miezi kadhaa, bado staa wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel Grayson, anaendelea kugandwa na madai kwamba, amenasa mimba nje ya ndoa, Ijumaa lina mkanda kamili.

Habari hizo zilishika kasi mithili ya moto wa kifuu baada ya Aunt kunaswa Klabu ya New Maisha iliyopo Masaki jijini Dar, Jumapili iliyopita akiwa ameshiba yaani kitumbo ndi huku akishindwa kukificha baada ya kila kitu kuonekana waziwazi kwa macho yasiyohitaki miwani.

KIGAUNI CHAANIKA KILA KITU
Aunt, akiwa ukumbini humo na mastaa wenzake waliohudhuria kwenye shoo ya msanii wa Bongo Fleva aitwaye Mirrow anayesimamiwa na kampuni ya muigizaji, Wema Isaac Sepetu na Meneja Petit Man, alitinga akiwa amevaa kigauni cha drafti nyeupe na nyeusi ambacho kilionesha vilivyo tumbo lake.

WEMA ADAIWA KUMSINDIKIZA KLINIKI
Kwa mujibu wa mpenda ubuyu wetu ambaye naye alikuwemo ukumbini humo, kwa kumtazama Aunt anaonekana kuwa na ujauzito wa si chini ya miezi minne sasa na kwamba Wema ambaye ni shosti wake anadaiwa kuwa huwa anamsindikiza kliniki lakini staa huyo ameendelea kusisitiza kuwa hana.

UJAUZITO MIEZI MINNE
"Mimi najua muda mrefu na jinsi anavyoonekana kwa sasa hakuna ubishi kwani ujauzito wake una kama miezi minne hivi," kilisema chanzo chetu na kuongeza:

"Mwanamke mjamzito anajulikana kabisa. Hebu mcheki usoni alivyobadilika. Yaani kawa mweupe wakati Aunt huwa ana rangi ya chokuleti. Ukweli ni kwamba ana dalili zote za kubeba mimba."

MAKE-UP YAMKATAA
Chanzo hicho kilizidi kuweka wazi kwamba, siku hiyo, Aunt hakuwa amechangamka kama alivyozoeleka siku zote na uso wake ulionekana kama mtu aliyechoka na hata ‘make-up' aliyoweka haikuwa ikionekana vizuri.

NDUGU WAANZA MANENOMANENO
Habari zaidi zilidai kwamba, baadhi ya ndugu na mawifi wa staa huyo wameanza kucharuka wakidai kwamba Aunt atakuwa amepata ujauzito huo nje ya ndoa kwa kuwa muda mrefu hajaonana na mumewe, Sunday Demonte anayedaiwa kuwa gerezani huko Dubai."Tangu mumewe apate matatizo Dubai hawajaonana hivyo Aunt hawezi kusema ni ya mumewe," kiliendelea kudai chanzo chetu.

VITABU VYA DINI
Baadhi ya ndugu hao wametaka vitabu vya Dini ya Kiislam viweke wazi kama ni sahihi kwa Aunt kubeba ujauzito nje ya ndoa kwani kwa upande wao wanapinga kitendo hicho na kwamba ni udhalilishaji kwa ndugu yao ambaye alifuata taratibu zote za kumuoa staa huyo.

Aunt Ezekiel wakati wa kufunga ndoa.

MNENGUAJI WA DIAMOND AHUSISHWA
Sosi huyo alidai kwamba ujauzito wa Aunt unahusishwa na mnenguaji wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz', Moze Iyobo ambaye kwa sasa wamegandana kama kumbikumbi wakisemekana kuwa kwenye mahaba niue.

SHEHE ANASEMAJE?
Ili kuondoa utata huku likijiridhisha kuwa Aunt anakaribia miaka miwili bila kukutana na mumewe, gazeti hili lilizungumza na Shehe Kaima wa jijini Dar ambaye analijua vizuri sakata la staa huyo ambapo alikuwa na haya ya kusema:
"Kwa kawaida mwanamke ambaye hajakutana na mumewe kwa miezi 6 au zaidi baada ya ndoa, hupaswa kwenda mara moja Baraza Kuu la Waislam Tanzania (Bakwata) kulalamika na hatimaye kudai talaka.

"Ikiwa mwanamke ameridhika na hali hiyo, naye akaamua kukaa kimya huku akifanya mambo yake na kuanzisha uhusiano na wanaume wengine maana yake amejitoa mwenyewe kwenye mamlaka ya mumewe, hivyo hapo kunakuwa hakuna ndoa tena."

AUNT ANASEMA?
Kama alivyojitetea siku ya bethidei yake oktoba, mwaka huu baada ya kuvaa kigauni cha pinki kilichoonesha kitumbo kikianza kuchomoza, katika tukio hilo la Jumapili iliyopita, Aunt ameendelea kusisitiza kuwa ni aina ya magauni anayovaa ndiyo yanayomuonesha na kitumbo lakini hana mimba.
"Sina huo ujauzito, labda ni kwa sababu ya aina ya magauni ninayovaa," alisema Aunt kwa kifupi.

MIAKA MIWILI ILIYOPITA
Oktoba 18, 2012, Aunt alifunga ndoa na Sunday ambapo mwigizaji huyo alibaki huku mumewe akitimkia Dubai kabla ya baadaye kupata matatizo na kutupwa jela.


CHANZO: GPL
 

Attachments

  • DSC06554.jpg
    DSC06554.jpg
    53.2 KB · Views: 3,888
acheni kumchafua Waziri kwa skendo za uswazi
Hebu nipe namba ya simu ya anti ezekiel ili tumuulize mwenyewe aseme ukweli
 
Kwani Nyalandu ni shetani asiyestahili kuzaa na mabinti kama Aunt Ezekiel? acheni hizo, mlitaka akili kuwa alienda marekani na akampa mimba Aunt?

Acheni hayo bhana, Nyalandu ni binadamu mwenzetu na mtanzania mwenzetu,acheni mambo hayo
 
acheni kumchafua Waziri kwa skendo za uswazi
Hebu nipe namba ya simu ya anti ezekiel ili tumuulize mwenyewe aseme ukweli

wew amakweli hauishi dunia yetu , nahisi si mtanzania hata hili la baraka pia walikataa, subiri uitwe uncle...
 
Kwani Nyalandu ni shetani asiyestahili kuzaa na mabinti kama Aunt Ezekiel? acheni hizo, mlitaka akili kuwa alienda marekani na akampa mimba Aunt?

Acheni hayo bhana, Nyalandu ni binadamu mwenzetu na mtanzania mwenzetu,acheni mambo hayo
naona mapungufu ya kwako subiri kutwa mjomba ,.... nyalandu ameteleza kwa hili....
 
View attachment 208234
hakuna lililo la kificho kama ijumaa lilivyo ripoti, matumizi mabaya ya ofisi ya umma yaliyofanya na Nyalandu katika kile alicho kiita kutangaza utalii huku kumbe ni kula uroda wa binti wa kibantu Anty Ezekiel HUKO Marekani kumetoa matunda kwani binti huyo amedaka ujauzito, macho na masikio ya watanzania yanasubiri kuona toto la kitalii likiletwa duniani kupitia binti huyo, sasa ni wajibu wake kukataa ila ukweli umedhihiri.

Jamani mambo mengine sasa ni umbea! kuzaa nako ni dhambi au ni baraka!?
 
Jamani mambo mengine sasa ni umbea! kuzaa nako ni dhambi au ni baraka!?

si dhambi ni jambo la kupongezwa ila mazingira ya ubebaji mimba yana zibana kodi za wa TZ ni kweli na binti huyo alikiri kwenda na mh.....
 
si dhambi ni jambo la kupongezwa ila mazingira ya ubebaji mimba yana zibana kodi za wa TZ ni kweli na binti huyo alikiri kwenda na mh.....

Hakukiri hivyo unavyosema wewe, alisema kuwa, alienda marekani kwa mwaliko, hakujua kuwa Nyalandu yupo huko, na alionana naye ukumbini, na wakati Nyalandu anaondoka ukumbini hakujua, sasa unataka nini? mimi sipendi tuingize mambo binafsi hapa kabisa.
 
Niliwahi kusikia Nyalandu jongoo wake hapandi mtungi!!! au kesharekebishwa?
 
Kwani yule waziri wa wazungu si nasikia sio ridhiki?
 
Si ndio matunda ya kutangaza utalii jamani!!!!
 
Ni ujinga kumchafua mtu kwa sababu za makundi yenu huko CCM. Lowassa atakua mtu wa ajabu kama ana watu wa aina hii ya mleta mada kwenye timu yake
 
Back
Top Bottom