Aunty Ezekiel: Nataka niwakomeshe wabaya wangu

Aunty Ezekiel: Nataka niwakomeshe wabaya wangu

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
MWIGIZAJI nguli katika tasnia ya filamu Bongo , Aunt Ezekiel aka cheusi dawa anadaiwa kuanza kusaka mtoto ikiwa ni miaka miwili tangu afunge ndoa na Sunday Dimonte .

Kwa mujibu wa rafiki wa karibu wa Aunt, siku si nyingi staa huyo atakwenda kuweka makazi ya muda kwa mumewe Dubai hadi atakapopata ujauzito. Akizungumza na Amani hivi karibuni, rafiki huyo ambaye aliomba jina lake lihifadhiwe kwa kuogopa kusutwa na ' matarumbeta ' , alisema wengi wanadai
mume wa Aunt yuko jela kwa hiyo ili kuwahakikishia kuwa kitu hicho hakipo ameamua aende kuishi Dubai kwa muda hadi atakaponasa ujauzito .

Aunt Ezekiel "Kama mipango yake itakwenda vizuri, baada ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kupita ataondoka na safari hii atakaa sana Dubai hadi Mungu atakapomjalia kupata mimba ndipo atarejea Bongo . Lakini baadaye ataondoka tena kwani hata kujifungua amependa akajifungulie Dubai , " alisema rafiki huyo . Baada ya kupata nyepesinyepesi hizo, Amani lilimtafuta Aunt na kufanikiwa kukutana naye uso kwa uso alipoulizwa alisema hapendi kuweka hadharani mambo yake na mumewe lakini kuhusiana na ishu ya kwenda kuishi Dubai , muda si mrefu ataondoka . "Nadhani unajua kuwa mke na mume Mungu akiwajalia
afya njema ni muhimu ndoa ijibu kwa kupata mtoto, sasa kuhusu kwenda kuishi Dubai ndiyo mipango yangu.
"Nataka kuwakomesha wale wanaodai kuwa mume wangu amefungwa ! Sitaki kuwajibu kwa maneno , nataka kuwajibu kwa vitendo , " alitamba Aunt .

Chanzo: Jipange101
 
Huyu anaishi ili watu waone jinsi anavyoishi?
Ina maana watu wakigoma kuona jinsi anavyoishi basi thamani ya maisha kwake inapotea?
R.I.P Me....🙁
 
Hapo anawakomoa au anajikomoa mwenyewe badala aishi life lake mwenyewe
 
Sasa kama mumewe hajafungwa kwa nini anatokwa povu hivyo? Ukijisikia kuzaa we zaa tu, sio kuzaa ili kukomesha watu.... Aunt jembe langu ila ananiangusha siku hizi, sijui kisa anashinda sana kwenye vigodoro hahahaha

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
tunasubir atukomeshe maana achelew kesho kuja na lingine
 
Mzushi hana lolote kafungwa kweli,yeye mwenyewe akiwa dubai anaishi kwa rafiki wa mumewe vichochoroni asizuge bure,
kama yupo nje na misifa alokua nayo mbona huyo bwana hamleti wakamuona watu? anyamaze tumsitiri.... Ramadhan ishakwisha aende tena akavae vichupi ma disco asijitie anakwenda kwa mume,hanae mume yuko kwenye senyege....
 
wabaya wake ndio watakaobeba mimba au ndio watakaomtunzia watoto??
 
wabaya wake ndio watakaobeba mimba au ndio watakaomtunzia watoto??

Labda watamsaidia kubeba tumbo na kujifungua labor, mwache awakomeshe abebe mimba akajifungulie Dubai ,nadhan ndo maana yake , ataenda kujifungulia Dubai awakomeshe wachawi wake
 
huyu naye limbukeni kweli, kubeba abebe yeye kukoma wakome wengine, huyu kabaki tu kuugua ukichaa wa kuvua nguo barabarani apelekwe milembe
 
Mtoto wake yeye na mume wake,.anawakomeshaje watu hapo....huyu mwanamke hamnazo kweli
 
Labda watamsaidia kubeba tumbo na kujifungua labor, mwache awakomeshe abebe mimba akajifungulie Dubai ,nadhan ndo maana yake , ataenda kujifungulia Dubai awakomeshe wachawi wake

Huyo mumewe mbna yuko mchelemchele bwabwa dizaini hii dunia ina mambo kwel
 
Back
Top Bottom