Australia: Serikali kupiga marufuku watoto chini ya 18 kuwa na Insta, X, Facebook na Tiktok?

Australia: Serikali kupiga marufuku watoto chini ya 18 kuwa na Insta, X, Facebook na Tiktok?

Jaji Mfawidhi

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2016
Posts
15,835
Reaction score
23,776
Serikali ya Australia imeonyesha njia baada ya kupiga marufuku mtoto chini ya miaka 16 kuwa na akaunti ya. mitandao ya kijamii ili kulinda maadili.

Nimezungumza na maelfu ya wazazi, babu na nyanya, shangazi na wajomba. Wao, kama mimi, wana wasiwasi kuhusu usalama wa watoto wetu mtandaoni, Albanese alisema.

Pendekezo hilo linakuja huku serikali kote ulimwenguni zikipambana na jinsi ya kusimamia matumizi ya vijana ya teknolojia kama simu mahiri na mitandao ya kijamii.

Majukwaa ya mitandao ya kijamii yataadhibiwa kwa kukiuka kikomo cha umri, lakini watoto wa chini ya umri na wazazi wao hawangefanya hivyo.

Jukumu litakuwa kwenye majukwaa ya mitandao ya kijamii kuonyesha wanachukua hatua zinazofaa kuzuia ufikiaji. Jukumu halitakuwa kwa wazazi au vijana," Albanese alisema.

Antigone Davis, mkuu wa usalama wa Meta, ambayo inamiliki Facebook na Instagram, alisema kampuni hiyo itaheshimu vikwazo vyovyote vya umri ambavyo serikali inataka kuanzisha.

"Hata hivyo, kinachokosekana ni mjadala wa kina kuhusu jinsi tunavyotekeleza ulinzi, vinginevyo tunahatarisha kujihisi bora, kama tumechukua hatua, lakini vijana na wazazi hawatajikuta katika mahali pazuri," Davis alisema katika taarifa.

Aliongeza kuwa zana zenye nguvu zaidi katika duka za programu na mifumo ya uendeshaji kwa wazazi kudhibiti programu ambazo watoto wao wanaweza kutumia zitakuwa "suluhisho rahisi na faafu."

X[tweeter] hakujibu mara moja ombi la maoni mnamo Alhamisi. TikTok ilikataa kutoa maoni

TANZANIA.
Serikali ya Tanzania inaweza kuzuia watoto, iwe sharti ukitaka kujiunga lazma uweke true credential zako.
 
Australia ndio nchi pekee duniani inayoheshimu jaki za kijamii.

Last week wamepitisha sheria ni marufuku kwa Maboss wote kuwapigia simu wafanyakazi waliopo chini yao baada ya saa za kazi au siku za mapumziko na hasa wanawake.
 
Kumbe Australia wajinga Ile haki sawa wanayoihubiria hapa iko wapi ila sheria yao nili ielewa sana lakini pia wazungu nawaelewa sana kwenye kujiekea mazingira mazuri hata kama jambo litakua baya wakiamua kulisimamia wanaliekea sheria zao za uongo na kweli jambo linanyooka nenda kwetu sisi sasa
 
H

Haki sawa Kwa watoto??
Hivi umeelewa kweli mkuu kilichoandikwa au ndo kujibu kwa kurupuka
 
Back
Top Bottom