Hizo ni taaluma za watu bora waachie wenye taaluma zao wafanyie kazi na wewe jiendeleze katika taaluma yako sio mtaka kujua mengi huo ndio ushauri wangu
hiyo ni profesional ya watu wengine
Shy,
AutoCAD siyo taaluma ya watu. Ni kitu ambacho kila mtu kama una nafasi basi waweza kujifunza hata ile basic tu. Ndani ya hii program kuna matumizi katika fani nyingi sana za Engineering na hata nje ya hiyo. Ila nafikiri kwa wale wote wenye michoro isiyohitaji freehand drawing, basi waweza kujifunza hii. Ndiyo maana wanasema CAD yaani 'Computer Aided Design'.
Kwa wale ambao unasema ni taaluma yao, hii program na Microstation huwa wanazitumia kama platform tu ya program nyingine. Yaani tuseme wanawasha computer na wanafungua kwanza Windows. Baadaye wanafungua AutoCAD au Microstation. Baada ya hapo ndipo wanafungua tena kiprogram kingine wanachotumia katika kazi zao. Nikisemea ambayo nilishawahi ifanya ni kuwa hapo nawasha program iitwayo INROADS. Ila sasa Inroads (inayotumika katika kuchora barabara) inaweza hata kufanya kazi ndani ya Autocad.
Hizi program ziko nyingi kwa sasa. Kuna za Madaraja, Reli, Sewage system, Structures, nk. Ukitaka ziona basi waweza watembelea hawa jamaa wa BENTLEY wa USA.
Hivyo Wandugu, hata kama wewe ni mtu wa electronics, hizo resistance zenu mnaweza kutumia AUTOCAD kuzichora. Na kwa kuwa kuna ZOOM kubwa sana, unaweza kuwa una ZOOM na kuchora hivyo vipande vidogovidogo saana. Pia unaweza kusoma kwa FUN. Uzuri mkubwa wa hii AUTOCAD ni kuwa kuna zile tools na symbol zake ambazo unaweza kuwa unaangalia picha na kujua harakaharaka kuwa wana maana gani.
Pia waweza kujitengenezea Maktaba ya hiso symbol. Hizi maktaba huwa zinaleta wakati mwingine ugomvi kazini kwani unaweza kujitengenezea na mtu akaja kukuibia. Wengine wanaziuza hizi symbol. Wewe badala ya kuchora, unachukua tu hizo symbo au kwa jina la kitaaluma wanasema "cell" na kuzibandika.
NB: Naona INVISIBLE KAWEZA tayari link:
https://www.jamiiforums.com/educati...94-autocad-2009-essential-training-video.html