Automatic gearbox/ transmission

Automatic gearbox/ transmission

Styvo254

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
246
Reaction score
227
WanaJamii mko poa?

Leo nimeona niwajuze kidogo kuhusu hii mitambo, automatic gearbox. Kwanza gearbox ni nini? Gearbox in mashine ya kubadilisha(kupunguza ua kuongeza) nguvu inayohitajika kufanya kazi flani, hufanya hivyo kwa kubadilisha mzunguko wa meno yanayotoa nguvu - au pia waeza sema kasi ya mzunguko kwa vile kuongeza kasi ni kupunguza nguvu.

Kwa kueleza zaidi; tuchukue gearbox yetu kama kapu lililowekwa chumvi(nguvu/power) na sukari(kasi/speed) zote jumla kilo kumi, masharti ni waweza punguza au uongeze yeyote bora jumla owe kilo kumi kwa hivyo ukiweka chumvi kilo tisa, sukari itabidi iwe kilo moja tu. Ukitaka kasi basi nguvu itokayo kwa mashine itakua chino, ndio sababu gari hungoa kw namba moja au mbili, na sio tano.

Hapo basi twaona kua gearbox ufanya kazi kwa kubadilisha mzunguko wa meno unayotoa nguvu ili kutoa nguvu au kasi kadri inavoitajika kuendesha chombo bila kuichosha engine kw kuipeleka kwa mwendo wa kasi zaidi au pole pole zaidi. Ubadilishaji wa gear waweza fanywa 'manually' na dereva au 'automatically'. Leo tunaangazia automatic.

Gearbox automatic zimekua nasi tangu miaka ya mapema ishirini karne iliopita. Matumizi yake kwa magari ya mauzo ya kawaida hapo kwanza yalikua nadra sana, labda kwa 'special order' sababu hii ilichikuliwa kama starehe ya kifahari. Lakini haya yamebadilika miaka thelathini - ishirini iliyopita tukiona magari ya kawaida yakija automatic na sio manual tena.

Kwa kweli watengeneza magari wana sababu ya kufanya hivi. Gearbox automatic ikitunzwa vizuri (service na mafuta yake halisi) utoa huduma kwa miaka zaidi ya ishirini bila tatizo, service ya kwanza kawaida hufanywa miaka mama kumi na baada ya kuanzia matumizi. Ukiangalia mwenzake wa manual, clutch assembly (clutch plate, pressure plate na release bearing) ni vitu vya kuisha kwa matumizi kama kawaida. Clutch plate ngumu sana kwenda zaidi ya miaka saba hasaa kw matumizi ya foleni za sasa.

Automatic gearbox ziko za aina tofauti, kama vile:

I) Epicyclic/hydraulic transmission
Hii ndio ya kawaida kupata kwa magari. Hutumia mafuta ya hydraulic kutenda kazi kwake, kupooza na kulainisha. Utenda kazi wake utumia misingi(principle) za mskumo wa mafuta(fluid pressure) kubadili mzunguko wa memo kwa kushika au kuachilia mizunguko ndani ya mfumo kupitia clutch plates na steel discs. Muundo wake hutimia meno yalioshikana kwa ndani na nje pia - yaani meno mengine yanazunguka ndani ya mzunguko wa mengine, ndio wanaita 'epicyclic geartrain'.

Kiungo msingi cha mfumo huu ua ni mafuta. Gearbox ziko tofauti kukingana na mwaka wa toleo, nguvu/size ya engine itakayotumika, nguvu inayohitajika kw chombo, matumizi, maamuzi ya muunda gari n. k. Tofauti hizi ubadili mifumo ndani ya mashine na kuhitaji mafuta ya aina flani ili kuiwezesha mashine kufanya kazi vyema.

II) CVT - Continuously Variable Transmission
Hii ni aina ya gearbox ambayo hutumia meno mawili ya muundo kama wa 'cone' na yaliowekwa mbadala - upande mkubwa wa moja uko na mdogo wa wapili, na kushikaniswa na nyororo ambayo utembea juu ya meno hayo toka mwisho mmoja hadi mwingine. Kumbuka kw upande mmoja jino la kwanza ni ndogo na lingine kubwa na ule mwisho mwingine aliyekua mdogo ndiye mkubwa na mwenzie mdogo. Ile nyororo inapotembea pale mzunguko unabadilika.

Utembezaji wa ile nyororo kwa miundo mingine hasaa ile ya kwanza unategemea kasi ya mwendo na kusongeshwa na uzito(centrifugal weight) unaotembea kulingana na kasi ile. Kwingine mskumo wa mafuta utumika pamoja na kupooza na kulainisha mfumo.
Kwa miundo ya kisasa mama kwa Nissan, kuna eCVT ambayo ni ya halo ya juu na hutumia umeme kuboresha utendakazi wake.

III) Automated Gearbox
Gearbox hii nayo ni ya manual ila ubadilishaji na clutch ni automatic. Meno ya ndani na utendakazi ni manual transmission kabisa na pia yatumia clutch kama ile ya kawaida.

Inapatikana hata kwa malori ya DAF na MAN kwa jina Astronic, Toyota MR2 pia inatumia hiyo design ya transmission na sasa hats Ford Focus, Mazda na wengine wameijaribu pia. Kwenye magari makubwa wanatumia mskumo wa hewa kubadili na kukanyanga clutch kw magari madogo ni mskumo wa mafuta au motor za umeme zatumika.

Muundo huu unasifika kwa kutunza clutch kw mda mrefu zaidi ya pale dereva anapoikanyanga mwenyewe, na pia uchaguaji wa gear ni mzuri zaidi na uinusuru engine majanga mengi.

Bila shaka kuna miundo mingine mingi lakini hizo hapo ndizo tunazozipata humu kwetu kwa sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom