Auwawa kwa kukojoa hadharani!

Msongoru

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2008
Posts
306
Reaction score
24
na Ramadhani Siwayombe, Arusha



JESHI la Polisi mkoani Arusha linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kumuua kwa kumpiga risasi, Rafael Lesika (35), baada ya kukojoa katika kituo cha kuuzia mafuta.

Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Robert Boaz, aliwataja wanaoshikiliwa kuwa ni Rafael Ebeneza (32) na Loshiye Moses (65).

Alisema tukio hilo lilitokea juzi, saa 1:30 usiku, maeneo ya Manispaa ya Arusha baada ya Lesika, aliyekuwa akifanya kazi ya upishi katika kampuni ya ulinzi ya Kili Warriors ya mjini hapa, akiwa na wenzake sita kufika katika kituo hicho cha mafuta cha Oil Com kwa lengo la kujaza mafuta katika gari lao.

Kaimu Kamanda huyo alisema baada ya kufika katika kituo hicho cha mafuta, Lesika alishuka katika gari na kukojoa chini, ndipo watuhumiwa hao ambao ni walinzi walikwenda eneo hilo kwa lengo la kumchukulia hatua kwa kosa hilo.

Kamanda Boaz alisema wakati wakimuhoji Lesika, kulitokea kutokuelewana kati yao, ndipo Mosses akamshika na mlinzi mwenzake Ebeneza akamfyatulia risasi na kufariki dunia papo hapo.

Alisema baada ya tukio hilo, walinzi hao walikamatwa na kufikishwa polisi katika eneo hilo. Watuhumiwa hao wapo rumande wakisubiri kupelekwa mahakamani kukabiliana na kesi ya mauaji hayo.

Kaimu kamanda huyo alisema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru, ukisubiri taratibu za mazishi.
 
Hiyo ni kuua bila kukusudia

Ni kweli kuwa muuaji aliua bila kukusudia, labda wawe walikuwa na ugonvi hapo awali / siku za nyuma.
Mungu wetu mtakatifu apokee roho ya marehemu kwenye raha yake ya milele. Amen.
 
Nadhani maelezo hayajakamilika ili tuweze kuhukumu kwa haki. Ila matatizo haya ya kuuana sisi wadanganyika kwa mambo yasiyokuwa na kichwa wala miguu yamezidi sana ktk miradi ya WATU wanaoitwa wawekezaji.

Nchi inakwenda siko kwa minajili ya kulinda mali za MAGABACHOLI. Sijui kama tutasalimika!!!!
 
Kitendo cha kumuua huyo kijana ni cha kinyama. Kwani kukojoa tu haiwezi kumpa mtu adhabu ya kifo. Ninakubali kwamba alifanya kosa. Alistahili kupelekwa mbele ya vyombo vya sheria. Sheria ndiyo ingemhukumu.
 
kusema kweli tabia ya kukojoa hovyo imepitiliza kusema ule ukweli inanikera mno ... ila hukumu ya kuua mbona kubwa sana
 
Nafikiri risasi lilifyatuka bila kutegemea. Sidhani kama mlinzi huyo alidhamiria kuua. Nao huu uhuni wa kukojoa hovyo kila mahali inabidi uachwe. We fikiria mtu kukojoa kwenye kituo cha mafuta!!!!! Mbona vituo vingi vya mafuta vina sehemu ya kujisaidia? Tuwape pole wafiwa.
 
Pengine marehemu alikuwa ameshapitia kambi ya fisi kabla ya kufika hapo kituo cha mafuta,

Poleni sana Wafiwa
 
Hiyo ni kuua bila kukusudia

Nashindwa kuelewa...! Hiyo bunduki ilikuwa ya aina gani...!? Ninavyo fahamu mimi risasi haiwezi kwenda chemba bila ya kuipeleka (tunaita kukoki), kisha unatakiwa ufunguwe kile kidude cha usalama pale karibu na kifyatulio. Sasa huyu mlinzi kwa bahati mbaya (!?) Kwa kweli nashindwa kuelewa... Kama sikusei bunduki yake hiyo inapitia hatua zote hizo. Risasi kaipeleka chemba... kisha... kafungua usalama... then anakurupukushana na kikojozi wa barabarani! Hivi alitegemea kitu gani? Je hakimu hakiamuwa kuwa ni uzembe...!
 
Haya ni madhara ya kujichukulia hatua mikononi. Mwanachi=sheria+mahakama=hukumu(KIFO).
 
kusema kweli tabia ya kukojoa hovyo imepitiliza kusema ule ukweli inanikera mno ... ila hukumu ya kuua mbona kubwa sana
...Sidhani hata huyo mlizi kama alidhamilia kumlima risasi lakini ndio hiyo muda ukifika lazima zigo limuangukie mtu.....Poleni wafiwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…