Msongoru
JF-Expert Member
- Apr 16, 2008
- 306
- 24
na Ramadhani Siwayombe, Arusha
JESHI la Polisi mkoani Arusha linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kumuua kwa kumpiga risasi, Rafael Lesika (35), baada ya kukojoa katika kituo cha kuuzia mafuta.
Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Robert Boaz, aliwataja wanaoshikiliwa kuwa ni Rafael Ebeneza (32) na Loshiye Moses (65).
Alisema tukio hilo lilitokea juzi, saa 1:30 usiku, maeneo ya Manispaa ya Arusha baada ya Lesika, aliyekuwa akifanya kazi ya upishi katika kampuni ya ulinzi ya Kili Warriors ya mjini hapa, akiwa na wenzake sita kufika katika kituo hicho cha mafuta cha Oil Com kwa lengo la kujaza mafuta katika gari lao.
Kaimu Kamanda huyo alisema baada ya kufika katika kituo hicho cha mafuta, Lesika alishuka katika gari na kukojoa chini, ndipo watuhumiwa hao ambao ni walinzi walikwenda eneo hilo kwa lengo la kumchukulia hatua kwa kosa hilo.
Kamanda Boaz alisema wakati wakimuhoji Lesika, kulitokea kutokuelewana kati yao, ndipo Mosses akamshika na mlinzi mwenzake Ebeneza akamfyatulia risasi na kufariki dunia papo hapo.
Alisema baada ya tukio hilo, walinzi hao walikamatwa na kufikishwa polisi katika eneo hilo. Watuhumiwa hao wapo rumande wakisubiri kupelekwa mahakamani kukabiliana na kesi ya mauaji hayo.
Kaimu kamanda huyo alisema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru, ukisubiri taratibu za mazishi.