Awamu na 6 na mbinu ya kuwainua Wakulima

Awamu na 6 na mbinu ya kuwainua Wakulima

Rashda Zunde

JF-Expert Member
Joined
May 28, 2022
Posts
204
Reaction score
231
Wakati Serikali ikitarajia kuanza kutoa ruzuku katika pembejeo za kilimo ikiwemo mbolea, wakulima wametakia kufuata utaratibu ulioweka ikiwemo kujisajili ili kufaidika na fursa hiyo itakayopungizia gharama za uzalishaji.

Kupitia mpango huo wa ruzuku, mbolea zote za kupandia zinazofahamika kama NPK zilizokuwa zikiuzwa kwa Sh122, 695 zitauzwa kwa Sh70 000 huku ruzuku ya Serikali ikiwa Sh52,695.

Pia UREA (ya kukuzia) iliyokuwa inauzwa kwa Sh124,734 wakulima wataenda kuinunua kwa Sh70,000.

Wakati akifunga Sherehe za Wakulima za Nane Nane Agosti 8 mwaka huu, Rais Samia aliagiza mpango huoa uanze Agosti 15 ili kuwawezesha wakulima kujianda vema na msimu wa kilimo unaokuja.

Waziri wa Kilimo Hussein Bashe aliyekuwa akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Saba Saba mkoani Njombe Agosti 10, 2022 amesema zipo hatua kadhaa ambazo mkulima anatakiwa kufuata ili apate punguzo la bei ya mbolea.

Hatua ya kwanza, wakulima wahakikishe wamejisajili ili waweze kupata mbolea kwa bei ya punguzo iliyotolewa na Serikali.

“Mkulima ukienda dukani swali la kwanza utakaloulizwa umejisajili? Hata kama hujajisajili mwambie ukweli sijajiajili,” amesema Bashe.

Kama mkulima hujajisajili, wakala wa mauzo atakuelekeza mahali pa kujisajili ambapo atachukua taarifa za mkulima ikiwemo majina kamili, kukupiga picha, kuchukua alama ya kidole gumba na namba ya simu.

“Ni muhimu uweke namba yako ya simu ili sisi ili tujiridhishe kama umenunua huo mfuko,” amesema Bashe.

Hatua ya pili mkulima ni lazima ahakikishe mfuko anaonunua una nembo ya ruzuku pamoja na msimbo wa majibu ya haraka (QR code) ambayo itakuwepo kwenye kila mfuko kuthibitisha kwamba huo mfuko wa mbolea umelipiwa ruzuku na Serikali.

“Utaona kidude pembeni ambacho kina na stika ukiona na mbolea haina hicho kitu toa taarifa kwa viongozi wa Serikali waliopo jirani hiyo ni mbolea ya usaniii iliyobanduliwa neno ruzuku,” ameongeza Bashe.

Amesema hatua hizo zikifuatwa vizuri zitapunguza wizi wa fedha kutoka kwa wakulima kuuziwa mbolea kwa bei ya juu ambayo tayari imelipiwa ruzuku.
 
HUWEZI KUWAINUA WAKULIMA KWA KILIMO CHA JEMBE LA MKONO
ARDHI IMECHOKA SANA KILIMO KINACHOTAKIWA NI CHA KUTUMIA ZANA ZA KISASA KUWAPA PEMBEJEO TU HAITASAIDIA
 
Serikali inamaanisha kuwa hivi vibanda vya kujisajilia vitafunguliwa pembezoni mwa maduka ya pembejeo?au hapohapo dukani nitasajiliwa?

Tarehe 15 hiyo yaja na tamko limeanza kuwekwa vizuri😄😄
 
Elimu ya ukulima wa kisasa yahitajika
 
Back
Top Bottom