Mwinyi, Mkapa na Kikwete wamewahi kutoa majibu ya hili swala na naamini hayo majibu yalitoka mioyoni mwao. Kuna wakati ambapo jina Tanzania lilikuwa la heshima na la kujivunia na waliokuwapo enzi hizo ni mashahidi. Kuna wakati Tanzania ilitazamwa kwa macho ya husuda na majirani zake na msimamo wake kwa maswali mbali mbali uliheshimiwa. Hivi sasa jina Tanzania linahusishwa kwa namna fulani na nchi ya mataahira na ni aibu wakati mwingine kujitambulisha hivyo.
Tanzania imewahi kuwa Maraisi wa aina nne tofauti kabisa na wenye misimamo na uwezo tofauti kabisa.
1. Mwenye nguvu, mvuto na mpiganaji ambaye yuko tayari kuutetea msimamo wake kwa nguvu ya hoja - Uraisi aliupigania mwenyewe.
2. Yupo yupo na mpole asiyejua jukumu la kiongozi wa nchi wala heshima inayoendana nayo, kila kitu rukhsa - Uraisi aliukwaa kama ngekewa.
3. Asiye na mvuto lakini hutumia nguvu kutetea hoja na kusimamia malengo hata kama hayana manufaa kwa taifa - Uraisi alipakatwa.
4. Asiyejua kwa nini aliutaka Uraisi ni kama mtoto anayelilia wembe na akapewa ! Uraisi wake ni feki - anachezeshwa kama "puppet"
Uchambuzi wako umekuwa wa kina sana na wenye hoja mahsusi. Lakini tukizichambua hizo hoja No1 hadi 4, zinaweza kuzaa hoja kubwa nyingine. Na kwa maana hiyo zinaweza kupata upinzani na kuungwa mkono kwa wkati mmoja.
Hoja namba 2, Yupo yupo na mpole ambaye ni Mwinyi. Kumbuka ndiye aliyesimamia mabadiliko toka ujamaa mpaka ubepari. Utaifishaji ndio ilikuwa kazi kubwa mno. Na hapa si utaifishaji tu, bali kubadilisha vichwa (idiolojia ) ya watanzania 35 mil. idiolojia ikiwa pamoja na ueleo wa maneno kinyume nyume, badala ya Mnyonyaji tumwite Muwekezaji, Nyapara mpaka kiongozi au msimamizi n.k. Kazi hii si rahisi, na aliifanya akiwa na upinzani mkali wa wafuasi wa Nyerere. Waziri hatekelezi agizo lolote la rais mpaka akaulize Butiama.
Tunaweza tukamwita mpole, lakini kama angekuwa mkali sana na mwenye kushikilia misimamo yake, Tanzania ingeweza kuingia katika vita. Maana tamaa ya mzee kifimbo katika uongozi ilikuwa kubwa kuliko tulivyofikiria, hasa ukizingatia umaarufu wake nchini. Kuwa Mzee haambiliki alikuwa alikuwa akiongoza awmu ya 2 kwa distance control, sio siri kwa watanzania wote. Jaribu kuwa katika hali hiyo mwenyewe, kuwa wewe ni bosi lakini umbo tu mwendeshaji ni mwingine. Kwa upande wangu Mwinyi alikuwa smart sana, kutawala serikali na serikali ndani ya serikali na bado tukapata amani. Uwezo huo wanao wachache sana, na ni viongozi wale walioweka maslahi ya Taifa mbele ndio wanaweza kufanya hivyo japo ya kuwa na jeshi.
Namba 3, hutumia nguvu kutetea hoja na kusimamia malengo hata kama hayana manufaa kwa taifa - Uraisi alipakatwa. Hapa umepatia, na ninakuunga mkono. Tumpe nafasi ya ngapi,, fikiria kama tamaa yake ya kuendelea baada ya miaka 10 ingefanikiwa na akakaa miaka 20. Je nchi ingekuwa wapi? Piga picha hiyo, na utoe nafasi.
Namba 4, Asiyejua kwa nini aliutaka Uraisi ni kama mtoto anayelilia wembe na akapewa ! Uraisi wake ni feki - anachezeshwa kama "puppet. Sijui anachezeshwa au ndio mbinu za kisiasa hizo. Kuna mifano ya marais wengi, hutumia mbinu hizo na kufanya vizuri katika maendeleo. Aliposhindwa katika uchaguzi kiongozi wa chama cha KADIMA (Israel), alisema maneno yafuatayo: Kuna wanasiasa wanaoamini kuwa maneno na vitendo ni tofauti. Akimaanisha kuwa hawatatekeleza yale wanayoahidi. Na ni kweli, katika utawala wa Nitanyau Palestine imetulia kuliko alivyoahidi vita tu na HAMAS, na kwamba atakifuta chama hicho. Kitu ambacho hakijatokea.
Naona mchezo bado mgumu, watoa hoja wameogopa sana kutaja moja kwa moja jina la Rais aliyeshinda. Lakini maelezo ya kila mmoja yanaashira sana kuwa Nyerere yu karibu zaidi kushinda tuzo.