Awamu ya 6: Tusije zembea ujenzi wa Bwawa la uzalishaji umeme Stieglers Gorge

Mimi naamini kabisa Magufuli angeweka shilingi 3t. Kwenye umeme wa gas tungepata hizo 2,115mg ambazo kawekeza 6.5t kwenye SG. Kuna watu wanaosema umeme wa maji ni rahisi na kuwa eti tumejenga kwa fedha zetu za ndani.
Hivi unajua bei ya gesi kwenye soko la dunia ni dola ngapi last month?
Kuna makampuni mengi ya gesi ya energy supply yamekufa Ulaya kutoka na bei ya gesi kuwa juu!

Bei ya gesi imekuwa ina fluctuate sana. Bei ikipanda gharama zinamuhusu mtumiaji!!

Halafu haya makampuni ya gasi yakishaua vyanzo vingine vya umeme. Kazi yao ni moja, fanya wanavyotaka. Ukileta ubishi wana turn off supply tap kwa kisingizio cha matengenezo!
Tukizubaa haya makampuni ya gesi ndio yatakuwa “King Maker” miaka hijayo. Mkileta ubishi mtakaa gizani mpaka msalimu amri!!
 
Ona Huyu na Ma gas yake ambayo Tunanunua kwa Wazungu kwa bei ghali wanatuuzia halafu tunauchakata ndipo Tanesco anauziwa...
Acha Hizo bana...
Kama unataka Kufaidika Na Gas tafuta namna nyingine waache watu wengi wafaidike na Umeme wa Nafuu wa Maji!

Tulikuwa tunatumia umeme wa maji toka zamani, mbona bado umeme haukuwa bei rahisi? Mkaa ulikuwa bei rahisi kuliko umeme.

Ndege ni za kwetu na sio za mkopo, mbona nauli ni bei ghali kuliko ilivyokuwa fastjet? Amka unaingizwa mjini bro.
 

Gas ni yetu boss. Huenda hauko hapa nchini. Ni hivi kuna bomba la gas toka mtwara hadi hapo kinyerezi na uzalishaji wa mg 450 mpaka sasa unaendelea. Jikite hapo badala ya hizo post zako za kiingereza hapo juu bro.
 
Tulikuwa tunatumia umeme wa maji toka zamani, mbona bado umeme haukuwa bei rahisi? Mkaa ulikuwa bei rahisi kuliko umeme.

Ndege ni za kwetu na sio za mkopo, mbona nauli ni bei ghali kuliko ilivyokuwa fastjet? Amka unaingizwa mjini bro.
Umeme siyo maji tu na ni kujidanganya kufikiri hivyo.
Umeme kunageneration, transmission na hatimaye retail.
Kwenye generation ndiyo tunaingelea sasa.
Infrastructure ya umeme wa maji ni kubwa lakini maintainance ni very low, wakati umeme kama wa gesi infraatructure ya priduction gharama si za juu sana lakini maintdinance ni VERY HIGH.

Tukija kwenye transmission, kuna maintainance ya lunes na ma trasformer mazito na madogo ma switches. Hapa maintainance ndito gharama isiyokwepukika.

Mwisho ni uuzaji wa umeme kwa viwango tofauti , na hapakuna gharama zake.

Hivyo kusema umeme wa maji ulitakiwa kuwa rahisi hivo ni only comparetive terms kwa long term analysis.
 
Safi mkuu , umelielezea vizuri hadi raha!
 
Nguvu zimeelekezwa kwenye bandari ya Msoga gang,bwawa si kipaumbele,Labda kwa vile kivuri Cha Magufuli bado kinawatesa kuutosa mradi wa bwawa.
 

Bila kubisha hiyo hoja yako kwani ina ushawishi wa kimantiki. Tulikuwa na umeme wa hydro, tulihamishwa huko kwakuwa tatizo lilikuwa mabadiliko ya tabia nchi. Na waliosema hivyo hadi kufikia 2015, ndio hao hao walianza kusifia umeme wa maji kuwa ni wa gharama nafuu! Wakati tunatumia umeme wa maji, bado nchi yetu haikuwa nchi yenye umeme nafuu kama nchi nyingine za Afrika mashariki. Nilitaka iwe hivi, wote tunajua gharama za nishati. Anayetumia petroli anajua tofauti ya diseli nk. Anayetumia gas anajua tofauti ya gharama za mkaa, umeme nk. Sasa nilichotaka nijue tofauti ya hawa wanaotumia umeme wa gas, na maji wapi kuna nafuu, ama ungeweka mfano kuwa wakati wa umeme wa hydro mkaa ulikuwa juu kuliko umeme, lakini tulipoanza kutumia gas mkaa ukawa chino.

Ukinitajia hizo terminologies za umeme, sijui distribution, transmission, infrastructure nk, kwangu naona ni mbwembwe tu zisizo na maana yoyote. Nafananisha na hili debe la ndege zetu, lakini gharama ni juu kuliko fastjet jet. Usishangae hizi porojo zote lakini huo umeme wa maji ukianza bei zikawa hizihiz za juu, na ukiuliza zikianza story hizi hiI za maneno ya kiingereza sijui factor, mara tarrifs yaani ni vurugu tupu.
 
Nguvu zimeelekezwa kwenye bandari ya Msoga gang,bwawa si kipaumbele,Labda kwa vile kivuri Cha Magufuli bado kinawatesa kuutosa mradi wa bwawa.

Tuombe tu huo mradi wa maji utekelezwa lakini hakuna anayeogopa hicho kivuli cha Magufuli. Kama yeye alitosa miradi aliyoikuta tena kwa kuibeza, usitegemee hawa wengine wana cha kumuogopa. Ingekuwa wananchi wana nguvu hapo sawa wangeogopa. Lakini huyo Magufuli ndio aliyepora nguvu za wananchi na kuzipeleka kwenye genge la chama chake na vyombo vya dola.
 

Mkuu kwa kifupi umeme wa gesi ni ghali kuliko wa maji….habari zingine hizo ni siasa..maana wapanga bei za umeme sio maengineer…

Tuzidi kupambana kwa nguvu zote bwawa likamilike ndio maana JPM alipambana lianze mapema iwezekanavyo…vita ni kubwa maadui ni wengi ndani na nje…wabaya zaidi ni wa ndani…unaeza ukawa mmoja wa adui wa ndani bila kujijua…
 

Ni kweli kabisa usemacho, je wakati tunatumia umeme wa maji gharama ilikuwa nafuu? Mimi sio engineer nitaamini vipi hiki usemacho? Au niamini tu ili nipone?
 
Ni kweli kabisa usemacho, je wakati tunatumia umeme wa maji gharama ilikuwa nafuu? Mimi sio engineer nitaamini vipi hiki usemacho? Au niamini tu ili nipone?

Mkuu umejibiwa vizuri na Maso.
Mbona suala liko clear sasa.
 
Mkuu umejibiwa vizuri na Maso.
Mbona suala liko clear sasa.

Sina popote nilipokataa hoja zake, bali nimekuwa na mtazamo tofauti kidogo na ukweli wake wote aliousema. Rejea post yangu namba 52.
 
Mkuu imebidi nirudi nyuma kusima posti yako no 52.
Inawezekana kabisa wewe ni mtu wa imani, zaidi kuliko kudadavua mada yenyewe.
Sioni hata jinsi ya kulipa miundombinu ya umeme wa maji ndani yamiaka 10, pamoja na unafuu wake kiujumla.

Suala la teknolojia tusiligeuze kuwa la imani, kama unavyo fanya.
 
Wahujumu wa nchi hii tutawajua vyema kutokana na yatakayoendelea kupitia kwenye miradi hii. Hawa ni 'wapigaji', wanachoweka mbele ni maslahi ya upigaji wao.
Tutatumia kila njia iwezekanayo kuwafunua mbele za wananchi wawwajue ni akina nani hawa wanaoiuza nchi yetu kwa maslahi yao binafsi.

Hata wakilembalemba hizo gesi zionekane zinafaa zaidi, tutawaeleza wananchi maana yao ya kukimbilia huko mara hii na kuucha mradi mkakati zaidi ukisuasua. Januari anakimbila nyimbo za Jua na upepo ili apate pa kupigia. Tutamfunua, hana akili ya ziada kuziba akili za wengine.
 
Mtalijaza kwa mate? Ukame ndio huo na hauishi kesho.

Amandla...
 
Gas ni yetu boss. Huenda hauko hapa nchini. Ni hivi kuna bomba la gas toka mtwara hadi hapo kinyerezi na uzalishaji wa mg 450 mpaka sasa unaendelea. Jikite hapo badala ya hizo post zako za kiingereza hapo juu bro.
Mkuu,
Mimi ni nipo hapa Tanzania ni mkulima na mfugaji.

Bei za umeme unaozalishwa kwa maji zinakuwa hazibadiliki kama bei ya umeme unaozalishwa kwa gesi au petrol.

Angalia kwa wenzetu wanaotegemea umeme wa gesi wanavyoteseka na bei

Wenzetu wnaotegemea umeme wa gesi bei zimeongezeka si chini ya mara 4 kwa mwaka huu peke yake!
Ndio, gesi inazalishwa uko Mtwara lakini na makampuni ya nje. Mikataba yetu na wao inasemaje gesi ikipanda kwenye soko la dunia? Mfano sasa bei za gasi na demand zipo juu Europe. Hao bado wataendelea ku supply kwa bei ile ile na supply bila kupungua?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…