Elections 2010 Awamu ya Kwanza Kampeni ya Dr. Slaa kuelekea Ikulu

Elections 2010 Awamu ya Kwanza Kampeni ya Dr. Slaa kuelekea Ikulu

Nawashauri Chadema walinde kura zao . Maana jitihada zote za kufanya kampeni hazitakuwa na manufaa kama hatutalinda kura zetu. Maana Mtaji wa CCM ni kuiba kura ndio maaana wanatumia umasikini wa mawakala na wasimamizi wa chaguzi kwa kuwarubuni kwa Tshs 10,000 mpaka laki moja na wanjizolea mamia ya kura ambozo mpinzani amezitafuta kwa jitihada kubwa. Chaedema lindeni kura na mengine yote yanawezekana

Hapo ndugu yangu unapotea maana mimi binafsi nimesimamia uchaguzi na sikuona hilo nililoliona ni kura nyingi kwa CCM.Na mfumo wa upigaji kura sasa hivi ni tofauti maana kura zinahesabiwa vituoni mbele ya mawakala wa vyama vyote.Zinazopelekwa Katani ni figures na mabox ya kura zilizofungwa. Hapo hakuna wizi kwa sababu matokeo yanakuwa kuanzia kwenye kituo cha kupigia kura mpaka juu.Tusilaumuvitu ambavyo havipo.
 
Dr Slaa anatisha! Ni kama vile amekwishashinda uchaguzi... Sasa ni wazi upepo wa siasa umegeuka Tanzania. Tutegemee mabadiliko ya uongozi na chama tawala mwaka huu.
 
.nimependa hiyo..."hatukubebwa na magari ..tumekuja wenyewe"..........maana namna JK alivyokosa soko siku hizi ...ili watu wafike kwenye mikutano yake hutuma malori na mabasi vijijini na mijini mbali .....kukusanya wasikilizaji.....kwa ujira wa tzs 2,000 HADI 10,000 kutegemea na kiwango cha uchumi cha eneo analopita......na mkataba ni kuwa advance wakati wa kupanda basi au lori na malipo ya mwisho wakati wa kuwarudisha nyumbani....kazi kweli kweli sijui PCB wapo wapi????..

.....siku hizi bila posho na usafiri CCM mikutano yake haipati watu....tabia mbaaya sana!!


Na hiyo ndo rushwa nyingine na ni njia mojawapo ya kuimarisha ufisadi na kuupanda kwenye mioyo ya Watanzania; usione ajabu Watanzania kuja na misemo ya ajabu ajabu kama vule; "hapendwi mtu, ni pochi tu, nk, nk".

I HATE THIS BEHAVIOUR YA KUDANGANYA-DANGAYA WATANZANIA WAKATI WAO WANANYONYA DAMU ZETU HATA NA WATOTO WETU AMBAO HAWAJAZALIWA!
 
Eee MUngu ibariki Tanzania yetu, weka mkono wako wenye nguvu juu ya watawala, hao wanaotafuta nafasi ya kutuongoza, tunaomba utume malaika wako walinzi waizunguke masanduku yote ya kura kusiwe na uwizi wa aina yoyote, maana uwizi si asili yako e mungu wetu, wapofushe wenye nia mbaya ya kutaka kubadilisha matokeo ya kura ili haki iweze kudendeka, Eee mungu tuhurumie sie wa Tanzania tumenyonywa vyakutosha, tumenyanyaswa vyakutosha, tumepigika vya kutosha, fungua akili zetu baba tuweze kutambua, kila kitu ndani ya nchi yetu kimebinafsishwa, lakini hatuoni matunda ya ubinafsishaji huo, kilicho baki nikubinafsishwa roho na watoto wetu, Eee mungu tunusuru na hili,
Mungu mwinue mtumishi wako Dr Wilbrod Slaa kama ulivyo mwinua Daudi kutoka mchanga kondoo hadi kwenye kiti cha ufalme. Amen

Watanzania hatuna chuki na kiongozi yeyote, ila tunaomba pia nawao waheshimu maamuzi yetu, haiwezekani sisi tumchague mtu serikali ituwekee huyu, basi awaongoze hao waliomweka.

hivi kuna haja gani ya kuwa na vyama vingi vya siasa kama chama kimoja ndo king'ang'anie uongozi, hawaoni hata nchi za wenzetu wanaotusaidia pesa za kuiongoza nchi wanafanyaje! ila shida iko kwetu wananchi,kwanini hatushangai kwanini viongozi hao wasiasa wakati uchagizi ukikaribia wanakuwa wako karibu na wananchi lakini akisha pata kura yako, basi hata kukuita mbayuwayu haoni shida, hatakama unashida ya kufa hauwezi kumwona, na ukijitahidi kumwona jibu atakalo kupa utatamani umwambie nirudishie kura yangu! hivi usipo chafuka utajifutaje? mwaka huu tuchague chama kingine kituongoze ila siyo ccm, waache wajifunze kuheshimu watu,
 
hata kama unasema hayo hatudanganyiki sasa tunaitaji maisha bora na makazi bora kura zetu kwa DR Slaa
 
slaa+geita.jpg


dr slaa anakubalika sana kanda ya ziwa, lakini mbona naona watoto wapo wengi? Je hawa ni wapiga kura hapo oct 31?


nimeona channel ten taharifa ya habari yani watu kibao, hao watoto unaosema wewe sijuhi wapi huko!
 
.nimependa hiyo..."hatukubebwa na magari ..tumekuja wenyewe"..........maana namna JK alivyokosa soko siku hizi ...ili watu wafike kwenye mikutano yake hutuma malori na mabasi vijijini na mijini mbali .....kukusanya wasikilizaji.....kwa ujira wa tzs 2,000 HADI 10,000 kutegemea na kiwango cha uchumi cha eneo analopita......na mkataba ni kuwa advance wakati wa kupanda basi au lori na malipo ya mwisho wakati wa kuwarudisha nyumbani....kazi kweli kweli sijui PCB wapo wapi????..

.....siku hizi bila posho na usafiri CCM mikutano yake haipati watu....tabia mbaaya sana!!

Hii safi sana nimeona picha vizuri make kwa michuziblog yeye anaweka picha za wapinzani ambazo zimepigiwa upande ambao hauna watu sana kuonyesha kuwa wapinzani hawapati watu kama picha za kikwete zinavyoonyeshwa, usanii mtupu
 
Mwaka huu ninavyoona hali, lazima Dr. Slaa atashinda. Ili umafia wa CCM uweze kumtangaza JK kuwa ameshinda, wafuatao watapiga kura:-
1. wanajeshi
2. Polisi
3. FFU
4. Wafungwa

Maana kwa hali ya kawaida haiwezekani kufikia hata 20% ya kura zote Tanzania.
Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Mbariki Dr. Slaa😛layball:
 
Hii safi sana nimeona picha vizuri make kwa michuziblog yeye anaweka picha za wapinzani ambazo zimepigiwa upande ambao hauna watu sana kuonyesha kuwa wapinzani hawapati watu kama picha za kikwete zinavyoonyeshwa, usanii mtupu


Hata TBC jioni ya leo wameonyesha picha za kampeni ya dr wa ukweli, Slaa akihutubia watu kiduchu huko Mwanza. Jamaa zangu nilioketi nao, ambao bado hawajaushitukia usanii wa TBC wakasema ah! Slaa hajapata watu wengi huko Mwanza.

Ilibidi niwape shule kidogo.
 
Mwaka huu ninavyoona hali, lazima Dr. Slaa atashinda. Ili umafia wa CCM uweze kumtangaza JK kuwa ameshinda, wafuatao watapiga kura:-
1. wanajeshi
2. Polisi
3. FFU
4. Wafungwa

Maana kwa hali ya kawaida haiwezekani kufikia hata 20% ya kura zote Tanzania.
Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Mbariki Dr. Slaa😛layball:
Wafungwa wana akili. Wakipelekwa kupiga kura watampigia Dr. Slaa kwa sirisiri.
 
buhaaaaaaaaaaaa haaaaaaaaaaa kweli maji shingonii
 
Wafungwa wana akili. Wakipelekwa kupiga kura watampigia Dr. Slaa kwa sirisiri.

Go Slaa, go
ila nina hofu na mabango ya CCM kila mahali huku Dar, CCM hawajapitiliza 50 billion, kiwango kilichowekwa na sheria ndogo ndogo za uchaguzi?
 
go slaa go wakuu kweli 2010 watz ha2danganyiki pamoja na porojo zote bado watu nyomi kwenye kampeni mungu wa pofushe wezi wa kuru tumpate rais chaguo letu.
 
Slaa+Mwanza2.jpg



Slaa+Geita.jpg


Dk Willibrod Slaa amecharuka mkoani Mwanza. Akiwa katika majimbo ya Geita, Buchosa na Nyamagana, mgombea huyo ametoa changamoto kali kwa CCM, hasa mgombea urais Jakaya Kikwete ambaye Dk. Slaa alisema ni "saizi yangu." Halafu akatumia fusa hiyo kumshughulikia, akisema rais huyo wa awamu ya nne hana mpango mkakati wala visheni ya kuwakomboa Watanzania. Badala yake, Kikwete amekuwa akitekeleza maagizo yake (Dk Slaa) katika kipindi cha miaka minne iliyopita, hasa kwa kudai anapigana na ufisadi (ulioibuliwa na Dk. Slaa). Hata katika tukio la juzi la Kikwete kumchukulia hatua Meneja wa kiwanda cha Turiani, Morogoro, Dk. Slaa alisema hatua ya Kikwete ilitokana na msisimko wa siasa za uchaguzi, hasa baada ya Dk Slaa kutembelea Turiani, wiki mbili zilizopita, na kutoa kauli kwamba atashughulikia matatizo yao katika siku 100 za kwanza za utawala wake.

Vile vile, alisema Rais Kikwete amevunja rekodi ya kudanganywa kuliko marais wote duniani katika miaka mitano iliyopita. Alisema mwaka mwaka 2007, JK alifungua mradi hewa wa maji huko Pwaga, Dodoma; mwaka 2009 Rais Kikwete aliletewa Ikulu mkurugenzi wa halmashauri isiyohusika na kukabidhiwa gari la wagonjwa; na alizindua hoteli moja ya kitalii mkoani Arusha, kesho yake ikavunjwa uzio na TANROADS, na mwaka huu alisaini kwa mbwembwe sheria iliyochomekwa vipengele ambavyo havikujadiliwa Bungeni; na kwamba hata baada ya matukio yote hayo, hakuna mtu aliyewajibishwa.

Mwaka huu, siku alipozindua kampeni za CCM mkoani Mwanza, JK aliwaeleza wananchi kwa mbwembwe, kuwa Mbunge wa Nyamagana, Lawrence Masha, alikuwa amepita bila kupingwa; jambo ambalo Dk. Slaa alisema si kweli kwani mgombea wa Chadema alikuwa ameweka pingamizi, ambalo hatimaye limemrejesha ulingoni. "Ama JK alidanganywa na Masha au alijidanganya mwenyewe au hakuwa makini…Kikwete si makini. Awaombe radhi wananchi wa Nyamagana kwa kuwadanganya."

Alisema Kikwete amekuwa rais wa majaribio, na kwamba miaka mitano inatosha. "Imetosha, Kikwete aende akapumzike, muda wake umekwisha, miaka mitano inamtosha. "Hatuwezi kwa miaka mitano kuendelea kuwa na rais mtalii, asiyejua matatizo ya wananchi wake, anayetetea maslahi ya wawekezaji badala ya wananchi, asiye na visheni," alisema.Dk Slaa alidai hata mipango mkakati kama MKURABITA, MKUKUTA na hata MINI-Tiger, hata na barabara anazojivunia JK kujenga ni za awamu ya tatu ya Rais Mstaafu Benjamin Mkapa, si zalo la awamu ya nne.

Akiwa jijini Mwanza, alisisitiza juu ya umuhimu wa viwanda katika kujenga uchumi, ajira na ujira bora; akasema CCM iliua viwanda na makampuni ya umma zaidi ya 450 yaliyoanzishwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, na hivyo kuua ajira na uchumi wa taifa. Alisema Chadema kinadhamiria kuanzisha viwanda vinavyotegemea mazao ya kilimo na mifugo, ili kuimarisha uchumi wa watu maskini, kwani raslimali zipo. Kilichokosekana, hadi sasa, ni ubunifu kwa upande wa watawala. Alisisitiza pia sera za elimu, afya, na makazi bora wa mujibu wa ilani ya Chadema.

Baada ya mkutano alisindikizwakwa maandamano na umati wa watu wazima na vijana, wakisukuma gari alilopanda kutoka uwanja wa Mirongo hadi Hoteli ya Nyumbani - umbali kwa kilometa zipatazo 5. Polisi walijitahidi kuwadhibiti wananchi hao, ikawa kazi bure. Hakukuwa na fujo yoyote. Walikuwa wakiimba, "rais, rais, Slaa; tumechoka mafisadi..." huku baadhi yao wakiwa na mabango yenye maandishi kuwa, "hatukubebwa na magari, tumekuja ejnyewe."

Asilimia kubwa ni underage.
 
Go Slaa, go
ila nina hofu na mabango ya CCM kila mahali huku Dar, CCM hawajapitiliza 50 billion, kiwango kilichowekwa na sheria ndogo ndogo za uchaguzi?
Usiwe na wasiwasi na mabango uchaguzi wa Tanzania hauendeshwi kwa mabango, huku kijiji kwangu hadi leo kuna bango la chagua Mkapa limekuwa kama pambo lakini watu wanajua watakayemchagua, baada ya Slaa kuapishwa hayo mabango ya Kikwete yatabaki kama kumbukumbu ya rais mstaafu.
 
Back
Top Bottom