Awamu ya pili ya HESLB yatoka, lakini waombaji wengi bado wakwama kwenye 'veification passed' shida ni nini?

Awamu ya pili ya HESLB yatoka, lakini waombaji wengi bado wakwama kwenye 'veification passed' shida ni nini?

Atukuzwaye

Senior Member
Joined
Oct 5, 2026
Posts
191
Reaction score
250
Bodi ya mikopo Tanzania imetangaza orodha ya wanufaika iliyotangazwa tarehe 21 Oktoba 2026, inayowajumuisha wanafunzi wa mwaka wa kwanza na wanaendelea na masomo waliodahiliwa katika vyuo mbalimbali vya elimu ya juu na vyuo vya kati.

Wanafunzi 90,235 wapangiwa mikopo na ruzuku ya TZS 284.73 Bilioni awamu ya pili 2026/2027. Katika post hiyo HESLB inawakumbusha waombaji wa mikopo na ruzuku wenye sifa kwa mwaka wa masomo 2026/2027 ambao bado hawajapangiwa mikopo kutembelea akaunti zao za SIPA wakati wa uchambuzi na upangaji wa mikopo na ruzuku zikiendelea.

My take;
Sasa kuna jopo la wanafunzi linalobaki na maswali kuhusu taarifa hiyo hasa ambao bado wakifungua akaunti zao wanakuta tu 'verification passed' kwamba waendelee kufuatilia maombi hayo au ndio tayari wamekosa?

Nadhani bodi ingesema lolote kuhusu hii issue, ili waombaji wapate uelewa zaidi kuhusu jambo hili, kwasababu wanafunzi wengi wanabaki kuulizana wao kwa wao jambo ambalo hata wao hawana uhakika nalo
BODI YA MIKOPO.jpg
 
Sawa pole yao wanafunzi ila hili lijina HESLB libadilishwe
Binafsi mijina isio yalugha yetu inanikera sanaaaaaaa
 
Back
Top Bottom