Abraham Lincolnn
JF-Expert Member
- Apr 12, 2018
- 2,754
- 4,975
Shujaa mashuhuri na kiongozi wa kijeshi na wa kisiasa nchini Ufaransa baada ya mapinduzi ya Kifaransa ,Napoleon Bonapatre aliwahi kutamka maneno haya;
"The world suffers a lot. Not because the violence of bad people, but because of the silence of the good people.”
Akimaanisha kwamba "Dunia inateseka si kwasababu ya uovu wa hao watendao maovu, Bali kwa ukimya wa watu wema"
Miaka mingi na imepita tangu karne ya 18 Baada ya mapinduzi ya Ufaransa,Lakini bado maneno haya yana akisi uhalisia katika jamii zetu.Pia tunafahamu kwamba daima kiongozi bora ni yule anayechukua hatua kuliko yule anayekaa kimya.Kwa maana nyingine ukimya huweza kuleta athari kubwa zaidi kuliko kutoa ufafanuzi na miongozo pamoja na hatua madhubuti katika kudhibiti changamoto na mienendo ya serikali kiujumla.Waswahili husema ni heri kuinuka na kuchukua hatua kuliko kuketi na kusubiri hatari ikukute, Kwa maana nyingine kiongozi anayesimama na kuchukua hatua (yoyote) ni heri kuliko yule asiyejisumbua kuchukua hatua, Kwani kwa kufanya hivyo huleta madhara makubwa kwa wale anaowaongoza.Waswahili husema heri lawama kuliko fedheha pia Lawama ya wazi ni heri, Kuliko upendo uliositirika.
1; Kuna watanzania wengi mno huko vijijini ambao huteseka kwa umasikini uliokithiri, Wengine hawana uwezo wa kupata milo walau miwili kwa siku.Unapokuwa kiongozi hauna budi kujiweka katika viatu vyao na kujua ni kwa namna gani unaweza kusaidia.Kukaa kimya au kutochukua hatua yoyote au kuelekeza matumizi ya fedha na rasilimali za wananchi katika ziara zisizokuwa na tija kwao na Semina,Birthday Party, Posho pamoja na matumizi mengine yasiyo na umuhimu huku wananchi wakifa na kuteseka kwa umasikini ni laana pia ni sawa na mauaji makubwa sana ambapo kama kiongozi hakika utaulizwa siku ya kiama.
2; Kuna wamama wengi wajawazito wanaopoteza watoto wanapokuwa njiani kuwahi huduma za afya kwa ubovu wa miundombinu.Kiongozi anayeona hali hii wala asishtuke wala kutoa viaumbele kwa watu hawa hana tofauti na jambazi au wauaji wengine wa kimbari.Bodaboda wengi hupoteza maisha kwa ubovu wa miundombinu,Ajali zimeua na zinaendelea kuua watu kwa ubovu wa miundombinu.Ukiwa kama kiongozi bila kuwa na jicho la kuyaona haya huku nguvu nyingi ukielekeza katika ziara za kutatua changamoto za gesi ya ukaa! hakika ni kutesa na kuua masikini! Ni laana kubwa.
3; Nchi hii ina wakazi wa madaraja tofauti, Wapo waliomatajiri, Wapo wale wenye uchumi wa kati pia wapo wale walio na uchumi wa chini kabisa wakiishi chini ya dola moja.Kuwa kiongozi anayetazama daraja moja na kuwasahau daraja la chini ambao kwa nchi masikini kama Tanzania ndiyo wengi zaidi ni dhambi kubwa sana! Tunafahamu wapo wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa lakini pia wapo wafanyabiashara ndogondogo wanaolisha na kuendesha familia na maisha yao kiujumla,Kuwatenga,kutowajali na kutokuwapa kipaumbele ni dhambi kubwa! haina tofauti na dhambi ya mauaji!
4; Kuwabebesha wananchi mzigo mkubwa wa kodi na tozo wakati huo nchi ikiwa na rasilimali za kila aina kama bahari,mito,maziwa,ardhi kubwa,madini ya kila aina hata kufikia kuwa miongoni mwa nchi zinazoongoza duniani kwa rasilimali ukiacha Congo DRC pamoja na Brazil huku Bibi masikini aliyepo kijijini kushindwa kunufaika na rasilimali hizo ambazo mara nyingi huishia mikononi mwa wachache na bado akaongezewa mzigo wa tozo ili mawaziri na wabunge waweze kuweka magari yao mafuta na kulipana posho zisizokuwa na umuhimu ni zaidi ya dhambi ya mauaji na ni laana kubwa
5; Lawama za vijana wanaokosa ajira huku serikali haijishughulishi kutafuta namna na njia mbadala ya kuwawezesha na kuwainua kiuchumi ni laana ambayo huimega na kuitafuna serikali hiyo kidogokidogo.
6; Kuruhusu bei ya bidhaa muhimu kwa wananchi kupanda kiholela bila kudhibiti na kuzidi kuongeza machungu na makali kwa wananchi ni dhambi isiyotofautiana na ile ya mauaji ya dikteta mashuhuri wa Ujerumani,Adolf Hitler japo utekelezaji huonekana wa tofauti.
7; Kuruhusu viongozi kujipimia na kula kwa urefu wa kamba,Huku wananchi wakiteseka na huduma mbovu kutoka serikalini haina tofauti na mauaji ya kimbari.Maumivu anayopitia mwananchi masikini mchuuzi wa samaki kwa samaki zake kuharibika baada ya umeme kukatika kisha samaki wote kuharibika na kisha kiongozi kutotoa maelezo yoyote au kujitokeza na kujibu kwa kejeli kisha kiongozi mkuu kukaa kimya bila hatua yoyote kuchukuliwa ni laana! ni zaidi ya jambazi anayeteka na kuua!.Huu ni mfano mmojawapo tu.
8; Kuona wananchi wakipitia nyakati ngumu wakati huo kiongozi kuamua kukaa kimya ni kudhulumu haki na uhai kwa wale waliokupa dhamana hiyo.Wananchi wanapodhulumiwa ardhi kisha kiongozi mkuu kukaa kimya bila kuwajibisha wale wanaohusika ni kutoa baraka ya dhulma! na jambo hili ni laana! haina tofauti na kuua!
9; Kuona mali za watanzania kama vile madini,Viumbe hai n.k zikiibiwa,kutoroshwa au kunufaisha wachache wakati huo kuna watu masikini sana huko vijijini ambao hawaruhusiwi kabisa kugusa rasilimali hizo au kunufaika moja kwa moja tena kufikia hatua wengine kuhamishwa kwa nguvu kupisha wale wenye mabavu kunufaika na rasilimali hizo! hakika hii ni laana kubwa sana! Kiongozi kufumbia macho au walau kuona ukubwa wake na kulitolea ufafanuzi ni dharau na kiburi cha hali ya juu sana!
10; Kiongozi kuona na kuruhusu maovu katika jamii, mfano madawa ya kulevya, wizi, ujambazi n.k bila kujitokeza na kukemea hadharani ni janga! Laana ya ndugu jamaa marafiki na wale ambao kwa namna moja ama nyingine wameathirika na madawa ya kulevya hayatakuacha salama kama kiongozi! na hata mbele ya Mungu utapaswa kujibu! Kwa kuwa ulikuwa na nafasi ya kuzuia au kupigana kuhakikisha unawalinda watu wako dhidi ya hayo lakini kwa bahati mbaya ulichagua upande wa wanufaikaji.