kifupi kirefu
JF-Expert Member
- Oct 29, 2018
- 539
- 3,507
Dunia na Ulimwengu unahitaji miradi endelevu ya maendeleo baada ya
mfumo wa miradii ya maendeleo kuonekana haina tija. (The world is focusing on Sustainable Development projects and programs not development projects). Kwanini miradi endelevu ya maendeleo?
1. Miradi endelevu lazima iwe shirikishi- moja ya hitajio la miradi shirikishi nikuwafanya wananchi na watumiaji wa mradi kuwa sehemu ya mradi na kujipa ile sense ya ownership (umiliki). Miradi mingi inayotekelezwa na awamu ya Tano siyo shirikishi katika ngazi ya siasa, kiserikali na jamii. Upo uwezekano miradi hii ikafa pale mwenye maono atakapoondoka madarakani.
2. Miradi endelevu ina sifa ya uwazi(Transparency). Miradi ya maendeleo ya awamu ya tano imejaa usiri mkubwa watu wakiaminishwa hata fedha za miradi hii ni fedha zetu za ndani huku ukweli ukiwa Ni kwamba tunakopa. Kukosekana kwa uwazi kunawafanya watawala watakaomrithi Magufuli kufanya kazi yakutukua makaburi Kama alivyofanya yeye. Kugukua makaburi kutapelekea tugombane na wakopeshaji wetu na waliotumika kukopa, taifa litaendelea kuishi kwa kufukua makaburi na kutuhumiana huku anayetuhumu akiwa mtuhumiwa ila tu mwenye sifa ya kushika mpini.
3. Miradi inayofanywa haikuzingatia taratibu za nchi- Ipo michakato imewekwa serikali inayoambatana na URASIMU, mfano taratibu za mikataba, manunuzi na upataji wakopeshaji na watekelezaji wa miradi. Urasimu uliowekwa kwenye serikali nyingi Duniani ililenga kuifanya serikali ifanye Jambo lililofanyiwa utafiti na likapita mikononi mwa watu wengi wenye taaluma tofauti ambao wataibua hoja zitakazopelekea kufanyika Jambo lenye maslahi mapana kwa Taifa. Awamu ya Tano kwa kiasi kikubwa imesukumwa na kuona matokeo ya miradi bila kuzingatia mlingano wa maslahi ya Taifa na miradi husika. Namna mradi unavyobuniwa, unavyopembuliwa hadi kuanza kutekelezwa kumekuwa na maelekezo mengi yanayofikia hata kuwatumbua wale wanaopingana na mawazo kutoka juu Jambo lililopoka Uhuru wa watoa maamuzi. Kimchakato mradi unaweza kuonekana umepita hatua zote ila kimantiki aliyeusukuma huo mchakato Ni aliyewateua watoa maamuzi.
4. Miradi endeleo haisukumwi na amri toka juu Wala maamuzi ya vyombo vya dola, miradi endelevu usukumwa na misingi ya sheria. Miradi yetu mingi imesukumwa na dola, nikawaida kabisa kumsikia Waziri aliyesoma economics akimshambulia na kumwondoa kwenye nafasi engineer bila hata kumpa nafasi yakujitetea kitaalam. Hi imewajengea hofu watumishi wa Umma na kuishi maisha ya Bora liende.
Hizi Ni baadhi ya hoja zinaifanya miradi ya maendeleo ya CCM kubaki na sifa ya miradi ya maendeleo na kupoteza sifa ya miradi ya maendeleo endelevu.