Awamu ya Tano na Udhibiti wa Ajali za Barabara I: Semeni Ninyi

Kwani unasikia habari za corona? Je haipo au mtu amekataza kutangaza?
 
Kwani unasikia habari za corona? Je haipo au mtu amekataza kutangaza?
Korona na ajali za barabarani ni vitu viwili tofauti. Ajali Wala huhitaji takwimu, ikitokea tuu hata kabla mamlaka husika hazijatangaza tayari tunakuwa tumeshapata kwenye mitandao ya kijamii. Hivyo usiwe tuu unapinga kila jema linalofanywa, hili la ajali mbona liko wazi na hata wewe ninauhakika unaujua ukweli kuwa ajali za barabarani zimepungua Sana na hii sio bahati tuu, ni mipango thabiti ya serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Magufuli.

Kulinda uhai wa watu wako ni jambo jema sana na la umuhimu mkubwa. Hongera Rais Magufuli, hongera jeshi la polisi, hongera madereva, hongera watumiaji wa barabara. Hongereni watanzania.

Hata hi yo, bado tunalo jukumu kubwa Kama wananchi kuhakikisha tunafuata sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa.

#Maisha yetu, jukumu letu, tuyalinde
 
kwa suala la kupunguza ajali tanzania bado ni safari ndefu saana.

wapo askari (trafic)wengi tuu ambao hawajui kile wasimamiacho barabarani na pia wapo ambao wenye elimu ya kile kisimamiwacho barabarani ila kwa makusudi wanaweka maslahi binafsi mbele

wapo madereva wasio na elimu ya udereva (kulijua gari na sheria za usalama barabarani) weengi tu na wanaendesha magari barabarani pia wapo wenye elimu hiyo ila hawaizingatii na wenye kuzingatia ni wachache saana.

watembea kwa muguu nao wapo katika sehemu ya visababishi vya ajali kwakuwa wengi wao nao hawana elimu ya matumizi salama ya barabara.

TANROAD na TARURA nao humo kuna madudu meeengi mnoo sehemu zenye uhitaji wa alama za kuvukia waenda kwa miguu ni chache mnoo kuko uhitaji halisi sehemu zingine alama zimefutika na pia vibao vya alama kudondoka na hawachukui hatu zozote.

LATRA na JESHI LA POLISI nao wamekuwa wakisingana katika majukumu yao hivyo hapo napo yafaa kiundwe chombo kimoja kitakacho husika katika kusimamia utoaji wa leseni za madereva pia kuhakiki madereva pia kusimami sheria za usalama barabarani pia kutoa leseni za usafirishani na kusimamia kanuni za usafirishaji.

wanasiasa ama viongozi wa nchi waache kutoa matamko ambayo yenye kuonyesha kutaka madereva hasa wa bodaboda waache kukamatwa hata palipo na makosa ya wazi kwani kwa matamko hayo tutaendelea kuona bodaboda wakiendelea kuwa ni katika kundi kubwa lenye kusababisha ajali na pia kutambua kuwa pengine bodaboda wa leo ndio dereva wa semi ama basi wa kesho

ni maoni yangu tu
 
tatizo ulitumia hisia kuandika kuliko takwimu
 
Awamu ya 3 na ya 4 ziikuwa na ajali nyingi na mbaya sana, sijui kwanini haswa.
 
Ujumbe murua
 
Unalinda uhai wa raia huku kukiwa na kundi la WASIOJULIKANA ambalo linateka, linatesa, linapoteza na KUUA raia huku Serikali ikiwa kimya kabisa na hakuna uchunguzi wowote? 😳😳😳
Ni sawa tu linawashughulikia wasaliti wa nchi hii.
 
Kuwa namba 6 duniani kwa ajali ni aibu kubwa kwa nchi hii. Duniani kuna nchi zaidi ya 200. Ukweli ni kwamba magu amefanikiwa zaidi kwenye propaganda hakuna anayemwamini hata marais wa nchi jirani wameanza kumtenga.
 
Fazili ndugu yangu, hakikaaa! Kama ni tabu utapata sana. Wewe ni wale aina ya watu wanaotafuta baya kwenye kila jema. Inshallah baadae leo nikitulia nitaandika uzi juu yenu. Labda itasaidia.
 
Fazili ndugu yangu, hakikaaa! Kama ni tabu utapata sana. Wewe ni wale aina ya watu wanaotafuta baya kwenye kila jema. Inshallah baadae leo nikitulia nitaandika uzi juu yenu. Labda itasaidia.
Mimi ndugu nazungumza ukweli kwa kuchambua mambo, sio kama watu wengi mtaani ambao wanalishwa propaganda. Usipokuwa katika level flani ya juu huwezi jua ukweli wa mambo na hilo ndio tatizo la Watanzania wenzangu. Wanalishwa uongo.
 
Mhhh hawa mabeberu vp jmn🤒
Mbona ajali za mabasi zimepungua sanaa ni kama hazipo kbs siku hizi
Gari binafsi pia kuna afadhali kubwa
Risk ni bodaboda na gari za serikali ambazo hazitaki suala la zima la usalama na 'speed governor'!
 
Kama ajali za mabasi zimepungua kuna ajali nyingi mno za boda boda na pia serikali hii kwa kuficha ukweli ni hodari sana kila kitu kibaya kinafichwa mithili ya takwimu za corona, unafikiri corona imekwenda wapi? Ipo ila tangaza uone.
 
Mimi ndugu nazungumza ukweli kwa kuchambua mambo, sio kama watu wengi mtaani ambao wanalishwa propaganda. Usipokuwa katika level flani ya juu huwezi jua ukweli wa mambo na hilo ndio tatizo la Watanzania wenzangu. Wanalishwa uongo.
Sasa ndio kupinga kila Jambo? Onesha basi uelewa wako
 
Unalinda uhai wa raia huku kukiwa na kundi la WASIOJULIKANA ambalo linateka, linatesa, linapoteza na KUUA raia huku Serikali ikiwa kimya kabisa na hakuna uchunguzi wowote? 😳😳😳
🤣 🤣 🤣 🤣 no comment
 
Reactions: BAK
Kama ajali za mabasi zimepungua kuna ajali nyingi mno za boda boda na pia serikali hii kwa kuficha ukweli ni hodari sana kila kitu kibaya kinafichwa mithili ya takwimu za corona, unafikiri corona imekwenda wapi? Ipo ila tangaza uone.
Hata nchi zilizoendelea zinaficha taarifa mbaya. Kumbuka wale wakimbizi wa Vietnam walioganda katika malori kule Uingereza wakitokea Ubelgiji, mpaka leo hatujui nini kinaendelea. Siungi mkono ufichji wa taarifa mbaya, lakini pia sio busara kuweka wazi kila kitu sometimes.
 
Sasa ndio kupinga kila Jambo? Onesha basi uelewa wako
Kwa mfano watu wanashabikia manunuzi ya ndtege, umewahi kusikia tangu tununue ndege miaka 3 imepita sasa ni faida kiasi gani imeingia? Na hata kama kuna hasara je ni kiasi gani? Hakuna. Tumefanya makosa makubwa kununua midege kwanza kwa cash, pili kuacha serikali ndio ifanye biashara ya ndege. Serikali zote duniani hazifanyi biashara moja kwa moja, zinakuwa na hisa kwenye makampuni na zinabaki zikikusanya kodi. Tumeingia kwenye biashara ya ndege iliyo biashara ngumu zaidi duniani tunaona mashirika mengi sana ya ndege yakipata hasara kubwa kwa mfano Kenya Airways haijaleta faida yoyote toka 2012, South African Airways toka 2011 ni hasara tu na inasemekana sasa shirika limekufa kabisa baada ya corona, n.k. ATCL inaendeshwa kibabe tu na kodi za maskini angalia hapa utaona jinsi ATCL ilivyochini, tena leo afadhali jana hapakuwa na safari kabisa kwa ATCL ni mashirika mengine tu Dar-es-Salaam Julius Nyerere International Airport Arrivals, Dar-es-Salaam DAR Arrivals | Airportia
 
Kwa hiyo wewe kudhibiti ajali ni tosha kabisa kunyamazia udhalimu wa kuteka, kutesa, kupoteza na kuua Watanzania wasio na hatia?
Mkuu kama unaushahidi kwanini huwapi polisi huo ushahidi usiokuwa na mashaka? Tufike mahali tuseme basi weka facts mkuu sio majungu na propaganda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…