Awamu ya tano ni chachu ya uharaka wa Katiba Mpya

Sina haja na nani anatawala nina haja na nani anatawala kwa ridhaa ya wananchi. hata Ulaya na Marekani hakuna chama kinachotawala milele litoke jua inyeshe mvua. Taifa linajiandaa kuhangaika na wakora wanaoiba kura. Taifa lazima lifike huko kwa kumfikisha mahakamani yeyote anaetuibia chochote kwa kutumia ridhaa tuliyompatia.
 
Wacha hizo wao walikuwa wanafanyakazi kwa manufaa ya wote, hata rais akiiba mali ya umma anakatwa shingo, hii ni tofauti na awamu ya tano ambayo chato ndio iliyokuwa inaangaliwa zaidi. Awamu ya tano ilikuwa inakata vichwa watu waliokuwa wanahoji utendaji na kuwaacha wezi. Hakukuwa na utawala wa sheria bali mtu huyohuyo anatuhumu, shitaki na kuhukumu.
 
Japokuwa si lazima kureply lakini naomba kuuliza kwa hiyo awamu ya tano ndio ilikuwa kikwazo cha katiba mpya au nimesoma usi kinyumenyume??
 
Hatari sn
 

🀣🀣🀣🀣 We unajielewa kweli? Au ulichoandika ndo hukielewi??? Kijazi interchange, tanzanite bridge na kijazi zipo chato?
SGR, mwalimu Nyerere, na msalato airport nazo zipo chato?

Acha kukalia akili namna hiyo kaka.... Nani amabye unamfahamu ambaye alikatwa kichwa na serikali ya magu? Dr ulimboka au?πŸ˜‚

Kesi gani ambayo magu alishtaki na kutoa hukumu mwenyewe?

Ukijibu hayo maswali utajigundua kuwa we ni walewale Team ufipa ambao hawana hoja maalumu katika vikao vyao πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†
 
Akili huna hata ya kusaidia kunusa harufu chafu. Dar es salaam, Dodoma, mwanza na chato ni nyumbani kwa JPM, ana nyumba na rasilimali huko. Tanzania Ina mikoa mingapi? Nitajie miradi aliyoipeleka Morogoro, Tanga, Kilimanjaro, Arusha, iringa, mbeya, ruvuma, singida, tabora, kigoma inayofanana na Ile aliyoipeleka chato, dsm, Dodoma na mwanza.
 
Japokuwa si lazima kureply lakini naomba kuuliza kwa hiyo awamu ya tano ndio ilikuwa kikwazo cha katiba mpya au nimesoma usi kinyumenyume??
Awamu ya tano ndio awamu pekee ambayo hata wanaCCM wenyewe waliuona umuhimu wa katiba Mpya kwa kile walichokiona kwa macho yao. awamu ya tano hakukuwa na serikali ya CCM bali kulikuwa na serikali ya makufuli na serikali ya awamu ya tano, mpaka mzee Mkapa rip akaingilia kati. Muulize Nape, January, Mzee Yusuph, Mzee Abdalahamani, mzee Membe, Mzee Sumaye, Mzee Ngoyai, mzee Lugola,.... watakwambia Katiba mpya ni muhimu leo sio kesho, hawakulamba asali hata kidogo, nyuki wote waliingia kwenye mizinga ya sukuma geng. Na jamaa akamka kabisa akisema "wacha niitumie katiba hii kuwanyoosha"
 
🀣🀣🀣🀣 Hivi hiyo mikoa unayoisema ushawahi kwenda kweli?... We jamaa ndo hovyo kabisa!
~Iringa uwanja mkubwa wa ndege unajengwa pale,
~Moro barabara ya njia nane inaenda huko, SGR nayo, na angekuwepo daraja la juu pale junction lingekuwa lishaanza kujengwa....
~Mbeya ndo usiseme...
~Tabora na singida alivuta maji toka ziwa Victoria mpaka pale ili kazi zianze, kwa vile bila maji hakuna kinachowezekana.... Kia kuna rada ya kimataifa na ya maana

Labda nambie wewe unavoanza kujenga nyumba ambayo jiko linajitegemea huwa unajenga kwa pamoja????

Tunavosemaga vijana wa khaki sometimes hamnazo mnaona kama tunawaonea. Sasa ww ndo umekuja kudhihirisha kabisa kuwa kichwa ni cheupe kabisaaaa πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Kwahiyo wewe unaona upigaji uliokuwa unafanywa na hilo genge ulikuwa sawa??? Kweli we akili umekalia sana... Nchi unapoifanyia mageuzi namna ya magu alivofanya lazima wapigaji waumie na wanakuwa na mneno sana....

Mzee kaondoka, mama kupitia waziri wake wa fedha wame suggest kuwe na kodi ya kichwa... Cha ajabu hakuna hata kiongozi mmoja wa upinzani aliyesimama kukemea hili kwa nguvu zote na wala hakuna hata asasi za kiraia au zile za haki za binadamu zilizosimama japo kuhoji tu.... Ila mguse mtu wa upinzani uone, hata km kakutwa na kosa hapo, nchi nzima upinzani na mashirika ya kiraia yatasimamia kidete....

Haya magenge huwaga siyaamini kabisa na ndo toka waukose ubunge ndo ikawa kero huku jf 🀣🀣🀣
 
Utawala wa Hayati Magufuli ulitufunza umuhimu wa Utawala wa kidenokrasia na Katiba Bora.
 
hata huna aibu kulinganisha kile kilichofanywa Iringa na kile kilichofanywa kwenye kijiji komoja tu cha Chato, shame on you. Chato tu peke yake kumejengwa Ikulu, uwanja wa ndege, bENKI, uwanja wa mpira, hospitali kubwa sana, barabara zenye traaffic lights ingawa magari ni 6 tu kijijini pale, na dakika sifuri kingegeuzwa kijiji kiwe Mkoa.

Kwahiyo mama Samia hakupata shida sana kuwashawishi wanaCCM kurejea mchakato wa katiba, ingawa kwenye mchakato huo wa kuandika katiba mpya kuna mambo pia yanayokwaza umalizaji ya kero za Muungano ambayo lazima katiba mpya iandikwe ili Zanzibar ijikomboe kwenye baadhi ya dhuruma za kikatiba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…