Awamu ya tano ya urais wa Hayati Magufuli iliwachelewesha sana vijana

Awamu ya tano ya urais wa Hayati Magufuli iliwachelewesha sana vijana

TheDreamer Thebeliever

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2018
Posts
2,490
Reaction score
3,584
Habari wadau,

Msema kweli ni mpenzi wa Mungu, licha ya mazuri ya awamu ya tano lakini kosa kubwa liliofanyika ktk awamu hiyo ni kuwachelewesha maisha vijana.

Vijana wengi hususa graduates walikuwa wanaishi kama mashetani hakukuwa na ajira wala viwanda vipya vilivyoanzishwa na hata miradi waliyotarajia ilikuwa ya kupika tu kwenye makabrasha. Utakumbuka mradi wa bomba la mafuta watu walifanyishwa mpaka interview wengine wakaenda mpaka Tanga kusubiria mradi waliambiwa utaanza SAP lakini zilikuwa siasa tu.

Mawaziri wa viwanda walidanganya sana uma kujifanya wanazindua viwanda vipya kumbe ni vile vile nadhani Hayati alikuwa hapati taarifa za kutosha au ilikiwa moja ya ajenda kuaminisha uma kwamba kuna viwanda vingi vimeanzishwa wakati vingi vilikuwa ni vile vile.

Ila nashukuru baadaye alikuja kustuka kwamba anachezewa mchezo ndio maana nyakati za mwisho alionekana kama amekata tamaa kuhusu sera ya viwanda maana alitumbua mawaziri wa viwanda mpaka alichoka.

Vijana wengi waliomaliza mavyuo wamejazana mtaani toka awamu ya tano mpaka sasa wapo waliokaa miaka zaidi ya saba bila ajira.

Kiukweli huu ni mzigo mkubwa ambao Rais Samia ameachiwa na mtangulizi wake na anapaswa kuubeba kama anataka 2025 aendelee kuwapo.

Na kiukweli hawa vijana waliokosa ajira wengi ndio wakosoaji na watukanaji wakubwa wa serikali mitandaoni, na kwa sasa nguvu ya mtandao ni kubwa ili mama Rais Samia aepuke kukosolewa mitandaoni inabidi amalize au apunguze tatizo la ajira kwanza ili vijana wawe bize na kazi wasahau kushinda mitandaoni.

Kamwe sitomlaumu Hayati kwa maamuzi yake yalikuwa mazuri ila hayakujari utu kwa kutowajari wahitumu wa vyuo wasio na ajira na kujari miradi (vitu). Wapo viongozi wake walioenda mbali na kuwabeza wahitimu kwa kuwataka wajiajiri wakati wanajua hawa vijana wametumia miaka mingi kugonga desa hawana chochote wanachokijua kuhusu biashara zaidi ya madesa.

Wito wangu kwa mama Rais Samia ajari utu kwanza vitu baadaye, hawa vijana waliokosa ajira miaka zaidi ya mitano kwa sasa wana watoto na wana familia zinazohitaji kuhudumiwa.

Katika awamu hii ya Rais Samia sitarajii kusikia kiongozi akisema vijana wajiajiri kwa kuwabeza, kama serikali itataka vijana wajiajiri basi iandae mpango maarumu wa kijana kujiajiri tangu yupo chuo, ikiwezekana baada ya kumaliza chuo waji organise wapewe elimu ya kujiajiri hata ya mwaka mmoja harafu waunganishwe na ma bank kupata mikopo.

Wasingoje mpaka wafike mtaani na mtaa uwavuruge mpaka wachanganyikiwe na stress za kitaa hatafu ndio waje waseme wajiajiri.
 
Umeongea ukweli mtupu kubwa huru hakuna kutekwa wala kuuwawa !!! Jamaa aliumiza watu sana aisee fikiria mwalimu aliye ajiriwa 2014 mpaka Leo hajawahi ongezwa mishahara wala kupanda daraja hali ni mbaya mno aisee,makato ya mkopo yaka double from 8% to 16% . sukari 2700 per kg,mafuta ya kula 5000 per Lt ,aisee acha tuuu !! Mama Samia okoa watumishi walidhalilishwa sana haijawahi tokea tangu uhuru
 
Ni kweli ametujeruhi na majeraha makubwa sana, hayaponi haraka , na tumefurahi alivyoondoka, apumzike panapostaili,
Kipindi cha miaka hii mitano watu wanatuumiana kwa uchawi, uvivu.nk
 
Back
Top Bottom