Aweso aiweka kikaangoni LUWASA. Aipa mwezi mmoja

Aweso aiweka kikaangoni LUWASA. Aipa mwezi mmoja

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610

Waziri wa Maji, Jumaa Aweso ameiweka katika uangalizi Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira mjini Lindi (Luwasa) kwa kipindi cha mwezi mmoja na kuahidi kuleta timu itakayowasaidia kuandaa mikakati.

Ametoa kauli hiyo jana Januari 26, 2024 akizungumza na bodi, watumishi wa mamlaka hiyo pamoja watumishi kutoka wakala wa maji na usafi wa mazingira vijijini (Ruwasa) Mkoa wa Lindi.

Pia, ametishia kuivunja bodi hiyo endapo haitofanya kazi yake ya kuisaidia mamlaka, kwa kuwasimamia watumishi kufanya kazi kwa weledi na kutoa huduma bora kwa wananchi.
 
Back
Top Bottom