Aweso awataka wakurugenzi wa mamlaka za maji kutobambikia watu bili za maji

Aweso awataka wakurugenzi wa mamlaka za maji kutobambikia watu bili za maji

Binti 1

Member
Joined
Dec 1, 2018
Posts
30
Reaction score
65
Waziri wa maji, Juma Aweso amewataka wakurugenzi wa mamlaka za maji kutoa huduma ya maji kwa wananchi badala ya kuwabambikia watu bili za maji.

Waziri Aweso ameyasema hayo leo mkoani Njombe katika ziara ya Rais Samia Suluhusu Hassan ambaye yupo mkoani humo kikazi.

Aweso amesisitiza kuwa maji ni huduma na sio biashara
 
Mwenye mawasiliano ya waziri tafadhari,naomba msaada mkuu.

Namna ya kumpata yeye mwenyewe nimwambie kitu kuhusu ubambikizaji huu
 
Makonde water supply wanaongoza kwa kubambikia wateja madeni.
 
Mwambieni waziri maji ni biashara vile vile, bila kufanya kama biashara pesa za kufanya maintenance zitatoka wapi
 
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Eng Justin Rujomba Tarehe 7.7.2022 amesaini Mkataba wa Construction of water blending system for FLOURIDE reduction wenye thamani ya TZS 36.3 Bilion na Kampuni ya Sinohdro Engineering ya china bila zabuni kutangazwa , Mkataba Ulisainiwa Tarehee 7.7.2022 kisiri bila kushuudiwa na Bodi ya AUWSA, Meneja Mradi Eng Mkawe na Menejimenti ya AUWSA kama utaratibu unavyotaka

Eng Rujomba hakupata Ridhaa ya Tender Board ya AUWSA kusaini Mkataba na wafadhili wa Mradi mkubwa wa Maji.

Arusha Bank ya Maendeleo ya Afrika ( AFDB) ilishatoa maelekezo kwa mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji AUWSA kuwa.

Wasitumie mfumo
Wa single source bali zabuni itangazwe apatikane
Mkandarasi mwenye uwezo lakini Eng Rujomba amekaidi kwa madai kuwa Kuna 10% ya kwake na Viongozi wa Wizara ya Maji.

PPRA Mwezi Novemba 2021 walitoa maelekezo zabuni zote zenye thamani inayozidi 5Milion itangazwe kupitia TANEPS,

Hata hivyo, Bank ya maendeleo Afrika (AFDB) wamegoma kutoa kibali ( No Objection ) ya kusaini Mkataba bila zabuni kutangazwa,

Maswali ya Msingi kwa nini zabuni haikutangazwa? Engineer Rujomba ametumia vigezo gani kuipatia zabuni kampuni ya sinohydro mkataba wenye Fedha nyingi kiasi hiki thamani ya TZS 36.3 bilion ?Kwanini mradi umesainiwa bila kushuudiwa na Wajumbe wa bodi ya AUWSA? kwanini Mradi umesainiwa bila kushuudiwa na Meneja wa Mradi na Menejimenti ya AUWSA? Kwanini mradi umesainiwa kisiri? Kwanini ENG Rujomba amekaidi
Maelekezo ya wafadhili Bank ya AFDB,

Ufisadi huu unafanyika AUWSA katika kipindi cha miezi Mitatau baada ya Kuvunjwa kwa Mkataba wa kifisadi wa Tzs 2.5 Bilion wa Ujenzi wa mfumo wa uondoaji Majitaka wa A to Z. Cha kushangaza walioshiriki kusaini huu mktaba wapo huru wanatamba kuiweka PCCB na wizara ya Maji mfukoni.

Waziri Mkuu , DG wa TAKuKuRu na CAG fanyeni uchunguzi wa mkataba wa Construction of water blending system for FLOURIDE reduction wa AUWSA na Sinohydro muokoe hizi pesa za wananchi maana mwisho wa siku watakaoumia ni wananchi amba ni walipa kodi na wahusika walioshiriki kusaini huu mkataba wachukuliwe hatua za kisheria.
 
Mkataba kati ya Sinohyro na AUWSA ulisainiwa tarehe 9 Oktoba,2018 na alianza Ujenzi rasmi tarehe 09 Disemba, 2018 na Muda wa Ujenzi wa mradi ulikuwa ni miaka miwili(2) yaani miezi 24. Sinohyro alitakiwa kukabidhi mradi tarehe 08 Disemba,2020 lakini kutokana na Usimamizi mbovu wa kula rushwa wa Mkurugenzi wa AUWSA hakuweza kukamilisha Mradi.

Sinohydro aliomba kuongezewa muda wa miezi nane (8)hadi agosti,2021 akashindwa kukamilisha mradi kwa kuwa usimamizi mbovu wa Kula rushwa wa Mkurugenzi AUWSA.

Sinohydro akaomba kuongezewa muda wa miezi wa miezi minne (4) hadi Disemba, 2021. Akashindwa kukamilisha mradi kwa kuwa na usimamizi mbovu wa Mkurugenzi AUWSA.

Sinohydro akaomba kuongezewa muda wa miezi saba hadi 07 Julai,2022. Mkandarasi akashindwa tena kukamilisha mradi na kukabidhi mradi ili Wananchi wa Jiji la Arusha waanze kutumia maji yaliyo safi na salama ambayo hayana fluoride.

Kazi ambazo sinohydro hajakamilisha ni
Ujenzi wa Visima Ishirini (20) vya Majimoto- Hai ambavyo maji hayana madini ya fluoride.
Ujenzi miundombinu ya Mabomba kutoka kwenye visima 20 hadi PS1: CHEMKA.
Ujenzi wa mashine za kusuma maji kutoka PS1-CHEMKA kwenda PS2-Mbuguni Kwa sasa maji yanasukumwa kutoka visima kumi (10) Mbuguni ambavyo vina fluoride zaidi ya 6mg/l. Wananchi wanakunywa maji yanayosukumwa kutoka PS2 hadi Themi.

Katika Mkataba kati ya AUWSA na Sinohyro unaruhusu Variation-Addendum Sub-Clause 13.1.3 any additional work, plant, Materials or Service necessary for the Permanet works, including Any associatedTests on Completion, boreholes and other testing and exploratory work kipengele kinataka Mkandarasi aongezewe kazi mpya endapo bila Mkandarasi kuongezewa kazi mpya hataweza kukamilisha kazi ya awali na pia hataweza kufanya majaribio ya kazi ya awali kwa kuwa zitakuwa zinategemeana. Kwa kifungu hiki Sinohydro alikuwa hana sifa za kupata Addendum ya Construction of De-fluoridation system at Seedfarm kwa kuwa tayari kashindwa kumaliza kazi ya awali kwa wakati.

Sababu za Mkurugenzi wa AUWSA kumpatia variations(Addendum) ya Construction of De-fluoridation system at Seedfarm kampuni ya Sinohydro ni kama hizi:

Kubadilisha gharama za ujenzi kutoka Tshs 20 Bil. hadi Tshs 36.3 Bil kinyume na Engineering Estimate ili aweze kupata rushwa kutoka kwa Mkandarasi. Zaidi ya Tshs 16. 3 Bil zinakuwa zimeenda kwenye matumbo ya watu, Serikali inakuwa imepata hasara

Kumuokoa Mkandarasi na Delay Damages kinyume na Sub-Clause 8.7.1 ya Mkataba ambavyo Mkandarasi alitakiwa kukamilisha kazi tarehe 07 Julai,2022 na utekelezaji wa mradi umefikia 78% na Particular Condition ya mkataba sub-clause 8.7.1 & 14.15.1 (b)-0.1% of the Contract Price per day and Maximum amount of delay deamages -8.7.1- 10% of the final contract price . Kulingana na kazi ambazo hajafanya anatakiwa kwa siku akatwe Tshs 100 Mil(100,000,000) na kama hatakuwa hajamaliza kazi ndani ya siku 100 anatakiwa awe amekatwa Tshs 10 Bil. (10,000,000,000).

Kumuongezea Muda kijanja Mkandarasi bila Mkandarasi kuomba kuongezewa muda na wala Consultant kupitia nyongeza ya Muda ili Mkandarasi aweze kuongezewa muda wa kukamilisha kazi zake za awali kinyume na mkataba sub- clause 8.2.1 cha kukamilisha kazi ndani ya muda wa Mkataba.

Mkataba wa Addendum kati ya AUWSA na Sinohydro umeisababishia Serikali hasara ya Tshs 26.3 bil na hii bila kuweka gharama za athari za Wanachi kutumia maji ambayo yana fluoride kwa sababu za kuchelewesha mradi. Makubaliano ya aide Memoire- special supervision mission kati 13-17 Juni,2022 yalisema kwamba rejea kipengele 3.24 &25

3.24 Construction of De-Fluoridation system at SeedFarm: The consultant has finalized the preparation of designs and tender documents for the construction of the De-Fluoridation System at SeedFarm. The bidding documents were submitted on 8 February 2022 for Bank’s review and consideration for “no objection”. During the review, the AUWSA came with an option of intending assign the construction work to the contractor (M/S Sinohydro Corporation Ltd) who is on site implementing the contract of the New Water System. The Bank advised the AUWSA to come up with clear justification including work rates and completion time of the proposed option.

3.25 The proposed option was discussed during the mission and agreed that; The AUWSA will prepare the justification together with contractor’s offer and share with the Bank for review and consideration for “no objection” by 24 June 2022. In case the justification won’t be accepted or the contractor on site refuse to accept the additional works, the AUWSA will proceed with the procurement procedures which will shorten the process of engaging a new contractor. The mission agreed that AUWSA will share the bidding documents together with the specific procurement note by 30 June 2022 for the Bank review and consideration for no objection.

Mkurugenzi wa AUWSA hakutaka kufuata hata maelekezo ya AfBD akasaini Addendum bila kupata No Objection ya bank ambavyo yeye mwenyewe alisaini hayo makubaliano. Bank hawajatoa no Objection kwa kuwa rate za BoQ za Addendum zimepanda kwa 82% kutoka kwenye zile rate za awali na Hakuna Engineering Justification.

02- Mkataba wa Ujenzi wa mabwawa ya kutibu majitaka Mkandarasi alitakiwa kufanya marekebisho kipindi cha Defects Liability kama Sub-Clause 11.1 inavyoelekeza, kipindi cha DLP ili kurekebisho Plastic Membrane ambayo yalikuwa yanajaa upepo na kuelea juu ya maji, lakini Mkurugenzi AUWSA alituma Watumishi wa AUWSA kutoboa na kuweka mawe ili kuyakandamiza kuyazuia yasielee. Kazi hii ilitakiwa kufanywa marekebisho na Mkandarasi kwa sababu ilikuwa ndani ya DLP na hata hivyo kutobolewa ni kinyume na Mkataba ila yote haya ni sababu za Mkurugenzi wa AUWSA kuchukua rushwa. Kwa sasa Makaratasi hayo hayana kazi na Serikali imepata hasara zaidi Tshs 2.8 Bil, taarifa hii ni ya kwel, tunaomba Serikali iunde tume na kuwauliza Watumishi wa Kitengo cha Majitaka na hata pia Wananchi wanaoishi karibu na bwawa hili. Serikali kupoteza Tshs 2.8 Bil ni gharama kubwa sana kwa walipa kodi.

03- Mkataba wa AUWSA na Tumaini Engineer Wenye thamani ya Tshs 2.5 Bil kujenga mtandao wa majitaka kutoka A to Z ni Wakifisadi na haukufuata taratibu za manunuzi.

Mfano wa ufisadi kwenye Mkataba unakifungu cha kuchimba na kufukia bomba Tshs 358,500,000 umbali wa kuchimba =8500m maana yake 1m inachimbwa Tshs 42,176 badala ya T.shs 12,000/=

Mkataba kutopitishwa na Bodi ya Zabuni (Tender Board) ya AUWSA kinyume na Sheria ya Manunuzi PPA,2011 section 35(1),(2) & (3)

Zabuni kutofuata Sheria ya Manunuzi (The Public Procurement (Amendment) Regulation,2016- section 91- Method of tendering for Non Consultancy Services.

Tumaini Engineer hadi Mkataba unavunjwa alikuwa tayari kalipwa zaidi Tshs 200,000,000 Mkurugenzi AUWSA na Tumaini Engineer wanatakiwa warudishe hizi Fedha kwa kuwa mkataba ulikuwa batili
 
Aweso ni fisadi , hizi taarifa za Ufisadi AUWSA anazo ameshindwa kuchukua hatua.

Akiongea Jukwaani unaweza ukadhani ni Hustaz safi kumbe ni fisadi Mkubwa.
 
Makonde water supply wanaongoza kwa kubambikia wateja madeni.
Watanzania jifunzeni kusoma meter reading za Maji ili kuepuka hilo tatizo!! Litter 1000 za maji ni sawa na unit moja tu ya maji! na unit moja ya maji ni sawa na Ndoo 50 za litter 20!!
 
Back
Top Bottom