Pre GE2025 Aweso: Rais ametoa maelekezo ni marufuku kumkatia maji mwananchi wa Mwanga, Same kipindi cha sikukuu na wikiendi!

Pre GE2025 Aweso: Rais ametoa maelekezo ni marufuku kumkatia maji mwananchi wa Mwanga, Same kipindi cha sikukuu na wikiendi!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu,

Kwahiyo huduma ya maji tunapewa kama hisani, yaani tunabembeleza kupatiwa huduma bora na stahiki!

Kwamba kupata maji siku za sikukuu na weekend ni mpaka maelekezo yatoke kwa Rais?:BearLaugh::KEKLaugh:

Kwahivyo huo mradi hautakuwa unajitosheleza, maji yatakuwa yanakatika kama kawaida?

Kupata mijadala ya uchaguzi mikoa yote Tanzania soma hapa Pre GE2025 - Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Mtuambie ukweli tuna maji kiasi gani tujiandae kisaikolojia!

Miaka 60+ plus bado tunaongelea mambo ya kumtua 'mama' ndoo, aroo CCM mnasehemu yenu mahususi kule kwa shetani wanamsemaga (kama yupo kweli).



Aweso amesema amepokea maelekezo kutoka kwa Rais Samia akisema ni marufuku hasa kwa watendaji wa huduma ya maji kuwa ni marufuku kwa wananchi wa Mwanga, Same kukatiwa maji vipindi vya sikukuu pamoja na weekend, waache wananchi wainjoy huduma ya maji safi!



Kuua soo Rais Samia amekuja kusema maji yatakuwa yanapatikana kila siku, eti hivyo ndivyo alivyoambiwa kama haitakuwa hivyo aambiwe ili ashughulike na Waziri!:BearLaugh::KEKLaugh: Sasa Aweso Wizara ya Maji ni Rais gani aliyekupa maelekezo wananchi wasikatiwe maji siku za sikukuu na weekend wakati Rais kaambiwa maji yanatoka 24/7?
Pia soma LIVE - Rais Samia azindua Mradi wa Maji Same-Mwanga-Korogwe Machi 9, 2025
 
Tangu lini maji yanakatwa siku za weekend au siku za sikukuu??
Kweli siasa ni tatizo kubwa sana!
 
Tangu lini maji yanakatwa siku za weekend au siku za sikukuu??
Kweli siasa ni tatizo kubwa sana!
Hapa nilipo maji hayajatoka toka juzi! Ulikuwa unamaanisha nini? Kuna tatizo kubwa ambalo halisemwi... mvua isiponyesha watavuliwa nguo
 
Serikalini wanaofanya kazi vizuri ni wachache sana, tena walio katika nafasi za utendaji. Wengi wamebaki na uchawa na kumtaja taja mama kila sehemu pamoja na kuvaa makofia yenye jina lake na picha yake.
Yaani kila sehemu piga kelele kwa mama Samia🤦‍♂️🤦‍♂️🤦‍♂️
 
Hapa nilipo maji hayajatoka toka juzi! Ulikuwa unamaanisha nini? Kuna tatizo kubwa ambalo halisemwi... mvua isiponyesha watavuliwa nguo
Niko Arusha leo, kuna mvua nyingi sana inapiga mchana huu. Huenda ukawa mwanzo wa masika.
 
Kwa hiyo maji hayakatwi kwa amri ya Rais? Sio kwamba Wananchi wanapaswa kupata maji muda wote???

Kweli sisi ni wendawazimu!
 
Kuua soo Rais Samia amekuja kusema maji yatakuwa yanapatikana kila siku, eti hivyo ndivyo alivyoambiwa kama haitakuwa hivyo aambiwe ili ashughulike na Waziri!:BearLaugh::KEKLaugh: Sasa Aweso @Wizara ya Maji ni Rais gani aliyekupa maelekezo wananchi wasikatiwe maji siku za sikukuu na weekend wakati Rais kaambiwa maji yanatoka 24/7?
Nchi ya kipumbavu mno inayoongozwa na matamko Tu Yaani mtu atakavyojiskia ndio atakavyotamka.

Suala la kukata Maji lipo kisheria na sio utashi WA MTU
 
Maji ni huduma,ila huku kwetu huduma hiyo imekuwa siasa!

Chadema ingechukua mwanga na same,wananchi wangekuwa walishapata maji tangu 2022.

Penye CCM pekee,maendeleo huwa yanachelewa sana!
Kondoa, mpwapwa,mwanga, chunya, Tabora,singida, huko kwote hakuna maji 😭
 
Yaani kila sehemu piga kelele kwa mama Samia🤦‍♂️🤦‍♂️🤦‍♂️
Unaweza kufikiri tupo kwenye kampeni tangu mwaka juzi.

Tupo katika kipindi cha ajabu sana, kila mteule na asie mteule ni chawa.
 
Back
Top Bottom