AY kuachia ngoma aliyomshirikisha Sean Kingston, kuiachia kimataifa

Joined
Sep 11, 2014
Posts
34
Reaction score
23
Msanii AY anatarajia kuachia nyimbo mbili za kimataifa mwezi November mwaka huu. Miongoni mwa nyimbo hizo ni pamoja na ule aliomshirikisha Sean Kingston.

926569_1457488691204165_749843811_n.jpg

Akiongea na kituo cha redio cha Nuru FM cha Iringa hivi karibuni, AY alisema miezi ya hivi karibuni amekuwa akiachia nyimbo kwaajili ya soko la ndani ukiwemo ‘Asante' na wimbo mwingine atakaoutoa hivi karibuni. Alidai kuwa baada ya nyimbo hizo ndipo atakaporejea tena kwenye nyimbo kwaajili ya soko la kimataifa.

Katika hatua nyingine AY amekiambia kituo hicho kuwa yeye na Diamond watawekeza kufanya video ya wimbo mpya wa Chidi Benz, ‘Mpaka Kuchee' walioshirikishwa.

"Watu wategemee video nzuri ya Chidi Benz," alisema.

Chanzo: Bongo5
 
Jamaa yangu huyu sijui ana nyota ya chumvi (chuzi likinoga inasifiwa nazi). Kaanza kitambo kupiga kazi za kimataifa lakini utashangaa sifa zinakwenda kwa wengine!! Namkubali sana
 
wapo weng wa hv kuna rama d, nk
 
Jamaa yangu huyu sijui ana nyota ya chumvi (chuzi likinoga inasifiwa nazi). Kaanza kitambo kupiga kazi za kimataifa lakini utashangaa sifa zinakwenda kwa wengine!! Namkubali sana

Hata nyimbo zake hazina mvuto sema anajitahidi kujitangaza nje ya mipaka.

Huwezi ku-win soko la nje wakati la ndani unachemka.

Ay alikua ni wa zamani enzi za NI RAHA TU, na EAST COAST TEAM.
 
Nyie ndio hamjui jamaa anatengeneza pesa nw kimataifa na anaaset za kutosha, ategemei magaseti ya udaku wala claudz fm, nitofaut na domo yy anajisifia sana afu maisha yake ya kawaida, na ipo siku domo ata achia video anajisaidia chooni
 
mkuu hii ni forum ila umeonyesha hisia za waz kabisa ni jins gan humkubali/husapoti kazi za nasib! pole sana ila kiukweli nimecheka kwa ulichikiandika mwishoni
 
No mm ninamkubali mtu yule anayejituma bt sio yule anayeenda kwa matukio ya uongo na kutuchukulia pess zetu
 
Sean Kingston wenyewe kalost, nyi bado mnaongelea collabo yake, labda tutasikiliza huku huku Iringa.
 
Hata nyimbo zake hazina mvuto sema anajitahidi kujitangaza nje ya mipaka.

Huwezi ku-win soko la nje wakati la ndani unachemka.

Ay alikua ni wa zamani enzi za NI RAHA TU, na EAST COAST TEAM.

Kweli nabii hakubaliki nyumbani....
 
Eeeee AY nae angeacha tu mziki akafanya mengine zaidi
 
Mwenzako anapiga bao vibaya halafu unasema ache??? Kweli nimeamini domo anamisukule yake humu, na wewe ukiwa mmoja wapo!
 
Hapa domo kaingiajee,yaan aimbege basi nyimbo zitushike masikioo
 
Sio kila nyimbo lazima zishike masikio yako. Kuna watu nawajua wao na msondo toka enzi hizo, wewe msondo unawaelewa???
 
Hata nyimbo zake hazina mvuto sema anajitahidi kujitangaza nje ya mipaka.

Huwezi ku-win soko la nje wakati la ndani unachemka.

Ay alikua ni wa zamani enzi za NI RAHA TU, na EAST COAST TEAM.

Jamaa kuimba hata mi najitahidi nimuelewe nashindwa lakini utaftaj wa masoko kwa huu mziki asilimia zote nampa
 
Nyie ndio hamjui jamaa anatengeneza pesa nw kimataifa na anaaset za kutosha, ategemei magaseti ya udaku wala claudz fm, nitofaut na domo yy anajisifia sana afu maisha yake ya kawaida, na ipo siku domo ata achia video anajisaidia chooni

weka picha hapo kwenye red
 
Back
Top Bottom