AY: Simsimamii tena Feza Kessy kimuziki

AY: Simsimamii tena Feza Kessy kimuziki

Money Stunna

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2011
Posts
13,053
Reaction score
6,304
AY amesema kampuni yake ya Unity Entertainment haimsimamii tena aliyekuwa mwakilishi wa Tanzania kwenye shindano la Big Brother Africa The Chase, Feza Kessy.

AY amekiambia kipindi cha Mambo Mseto cha Radio Citizen jana kuwa hajawahi kukutana na Feza tangu arejee kutoka kwenye shindano hilo.

“Tangu ameenda Big Brother na akarudi hatujawahi kukutana face to face,” alisema AY.

“Kulikuwa na vitu kidogo ambavyo viko nje ya kikawaida kama unafanya kazi na artist vinatakiwa vifanyike. Kwahiyo tukaona labda alikuwa anatafuta tu opportunity fulani ya kukamilisha mambo fulani. Katika policy zetu za kampuni ni kuwa hatufanyi kazi kwa njia hiyo, kwahiyo tuliamua kumweka pembeni.”

AY amesema tayari alishaongea na Feza na kumtakia kila lakheri kwenye kila jambo atakalolifanya.

“Hata yeye mwenyewe tu nilimwambia namtakia kila lakheri, cha msingi atumie hiyo opportunity aliyoipata sasa hivi ili kufanya mambo mengine kama washiriki wengine wanavyoenda katika Big Brother.”
 
Mmh hata jina lenyewe hana,sasa anajifany super star kisa kaonekana africa nzima bba,wakat uku ukijulikana bangala,tandika ndo mapngo mzima unapeta
 
huyo feza kwanza hajui kuimba kabisa ni mmoja ya watu wanao lewa sifa na umaarufu.
 
sasa sijui ataenda tena kwa AY maana alivyotoka mjengoni akamkacha na kukata mawasiliano akajiona star haya sasa kimenuka kwa huyo boyfriend mtu Botswana
 
Back
Top Bottom