makaveli10
JF-Expert Member
- Mar 27, 2013
- 31,583
- 92,670
Takribani miezi 10 ama 11 hivi nilikuwa sijagusa mpira, siku hiyo mwili wangu unatamani mpira kuliko chochote, hata ule mchezo wa mguu bara mguu pwani siutamani kama ambavyo nimeamka na tamaa ya kucheza mpira, akili yangu haiwazi mengine kikamilifu ni mpira tu, kila mara najiona kama uwanjani, nafanya vitu vyangu.
Hatimaye jioni ikafika nikachukua viatu vyangu, mie huyo mdogo mdogo uwanjani, njianj nikakutana na jamaa zangu wawili watatu na kunitania
Jamaa "mkongwe naona unaenda kufanya vitu vyako, tunakuja huko kuona burudani"
Mimi: burudani wapi mtaalamu, viungo vyenyewe vibovu, naenda KUZIPASHA SHAHAWA zangu.
Tukacheka, kila mmoja akaenda na njia yake.
Kufika mazoezini watu, wakanilaki kwa furaha, "fundi, fundi, fundi. Miezi 10 si midogo, nikaona sura ngeni kadhaa,
Madogo wakaanza kunitania, leo umekuja, umekutana na fundi mwenzio, haya ubishi wetu leo unaisha, wengine, aahh, huyu kajizeekea, wengine mara hivi mara vile,
Nikamuuliza dogo mmoja wanaongelea nini hawa, mmoja akaniambia kuna jamaa hapa, wanaijeria miongoni mwao kuna huyo fundi, watu wakasema kaziba pengo lako uwanjani, burudani yako yote inapatikana kwake, ndio kukawa kumegawanyika pande 2, wengine wanakubali, wengine wanasema kwenye ubora wako hajafikia,nikatabasamu nikavaa viatu vyangu, mdogo mdogo uwanjani.. Dogo mmoja akaniambia maestro, leo unachezea timu yangu.
Baada ya kupasha pasha, mpira ukawekwa kati, tukaanza kukipiga, piga sana mali dk kama 45 hivi nishapiga pasi zangu kama 50 hivi, nishafanya dribbling zangu za kibabe kadhaa, mmoja akaniita, mkongwe inatosha, naomba sub, uliyofanya yanatosha.. Nami pumzi zilikuwa zishaanza kukata, nikajisemea ngoja nami nikae nje, kumuona vizuri huyu mnaijeria anayeitwa fundi, aisee ni fundi kweli kweli, anajua sana boli, kuna mambo tunatofautiana, ila bado anakaa kwenye kundi la watu wanaojua boli.kabla ya mazoezi kuisha nikajiondokea zangu..
Kesho yake nikaenda tena ila nilijikuta nimewahi, wakati niko bize na simu, akaja jamaa mmoja akakaa pembeni yangu, akanisalimu, kuinua kichwa ndio yule mnaijeria, piga stori kadhaa, akaniambia anatamani angeniona miaka 10 nyuma nilikuwaje, naonekana naujua sana mpira, nikampa historia yangu kiufupi, wazazi hawakutaka nikomae na mpira ila nikomae na school, lakini isivyo bahati zaidi nilipokuwa najiiba kwenda kucheza, nikaishia kupata majeraha mabaya sana, goti na nyama za paja.. Hivyo mpirani sina historia kubwa ya kutamba, hapo ndio ikawa mwanzo wa urafiki wetu na huyu fundi, nikaja kumjua zaidi baadae kadri tulivyozidi kuzoeana.
Jamaa anaitw ayobami junior, wenzake wanamuita BAGGIO, ni mnaijeria aliyepata kucheza kano pillars, kwara united na shooting stars, kacheza u23, alishindwa kucheza CHAN sababu ya kutokuelewana na manager wa timu.
YouTube ana video nyingi sana, nyingine mashabiki wanalalamika kwanini kaachwa timu ya taifa ya wachezaji wa ndani.
Jamaa ni fundi mnoo, kosa alilofanya ni kuja kichwa kichwa, ila naamini dirisha hili dogo anaweza kupata timu...
Kilichomponza ni ile hamu ya kucheza nje ya ligi yao, viongozi wa timu yake shooting stars, hawaachi kumpigia simu arudi, ila mwenyewe anakuambia alishajiapiza mkataba ukiisha yeye na ligi ya naijeria ndio wamemalizana, hataki kabisa kucheza ligi ya kwao, bahati mbaya zaidi akakutana na wakala kanjanja, mgeni kwenye game, bongo hana connection ya kutosha, hivyo anataabika kupata timu.
Siku 1 kaja home tunatizama game ya Dodoma jiji sijui na pamba wale, ghafla namuona mtu kainuka kwa furaha kubwa, kaenda mpaka kwenye tv, namuuliza vipi akanionesha mchezaji wa Dodoma jiji, akaniambia huyu ni ematah, nimecheza nae ligi ya nyumbani, hawa mie nikicheza wao wanapiva salute, akaniambia inshaallah ni dalili njema kwake, kidogo akamuona jamaa anaitwa obata, akaniambia wamecheza timu moja.
Akaanza kusaka namba zao, akapata ya john noble, wote hawaamini kama yupo bongo, noble akamwambia the only mistake kafanya ni kuja Bongo bila timu, ni ngumu timu za huku kumthamini, ila asijali atacheza kwa kiwango chake, ila hatoipata thamani yake kwa haraka, wenzake kina ematah wamekuja bongo tayari wana connection, wamesha sign pre contract.
Kama jamaa atapata timu dirisha dogo na asizuzuke na wadada wa mjini basi katika ligi yetu kuna burudani imeongezeka.