Ayoub Rioba: Kuna watu wanazungumza Mkapa alikuwa hapendi waandishi, hakupenda wavivu na wakosoaji bila maarifa

Ayoub Rioba: Kuna watu wanazungumza Mkapa alikuwa hapendi waandishi, hakupenda wavivu na wakosoaji bila maarifa

Casuist

JF-Expert Member
Joined
Jul 23, 2014
Posts
1,189
Reaction score
2,970
Mkurugenzi wa TBC anamuongelea Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, marehemu Benjamin Mkapa, katika sekta ya habari anasema alikuwa mtendaji mahiri aliyependa umakini kitu ambacho TBC wamekuwa wakisisitiza mpaka sasa kitu ambacho Mkapa alikisimamia wakati akiwa mhariri.

Pia ameongelea Mkapa akiwa Rais, amesema kuna watu wanazungumza kuwa Mkapa alikuwa hapendi waandishi wa habari kitu ambacho sio kweli kwani alikuwa hapendi waandishi wa habari wavivu, wasio na umakini kwani unaweza kumkuta muandishi wa habari anaandika anakosoa tu lakini yeye mwenyewe hana maarifa au hajui kinachoendelea kiasi impe uhalali wa kukosoa wengine.

Amesema kukosoa ni jambo zuri lakini mwingine anakosoa huku lugha yake haina ufasaha vinginevyo Mkapa alikuwa anapenda uje na hoja zako hakuna haja ya kutukanana.
 
Huyo jamaa sidhani kama ni mwandishi wa habari. Hivyo hana uhalali wa kukanusha kilichosemwa na mwandishi wa habari ambaye alikuwa mwandishi wa habari wakati yeye bado anafungwa nepi za vitenge
 
Back
Top Bottom