Jaji Mfawidhi
JF-Expert Member
- Feb 20, 2016
- 17,434
- 27,177
ANAANDIKA AYOU RIOBA , MSTAAFU TBC ANAYEKULA MAFAO KWA MRIJA:-
MDA ALIVYOMJIBU MSTAAFU ANAYEKULA MAFAO YAKE :-
Ziara ya Rais SSH Urusi ni muhimu sana, hasa tukizingatia historia ya mataifa yetu!
Ninafahamu fika kwamba ndugu zetu mabeberu watachukia. Tanzania na Urusi zina historia kubwa kimahusiano.
Tuna Watanzania wengi waliosomeshwa Urusi na wanazungumza Kirusi.
Rais Vladmir Putin ana historia ya kufundisha wanamapinduzi wa Afrika kipindi tunatafuta uhuru wa nchi za Afrika!
Urusi ina utamaduni na historia ya kusaidia mapambano ya Afrika dhidi ya ubeberu wa nchi za magharibi
Wanaofuatilia historia yetu wanajua hili. Hongera Rais SSH kwa ziara hiyo muhimu. Hongera Rais Putin kwa kumwalika Rais wetu!

1. Mwanazuoni mwenzangu, Dkt. Ayub Rioba, matumizi yako ya neno “mabeberu” yanaonekana kuwa ya kimajukwaa na kisiasa zaidi kuliko ya dhati ya kitaaluma (Empty political rhetorics). Hili ndilo ambalo wengi wangelitafsiri kama kutokuwa mwaminifu katika mjadala wa kitaaluma (academic dishonesty). Kama wasomi, tunayo wajibu wa kuchambua hali halisi kwa uaminifu na ukweli, badala ya kutegemea simulizi za kisiasa zilizopitwa na wakati kuelezea changamoto za sasa.
2. Nchi yetu kwa sasa ipo katika njia panda. Uhuru wa kutoa maoni, uhuru wa kujieleza, na haki ya watu kuwa na mitazamo tofauti vinaonekana kuwa katika mazingira ya shinikizo kubwa. Demokrasia imeathirika na misingi ya kikatiba imekuwa ikikiukwa mara kwa mara. Katiba yetu iko wazi kwamba madaraka yote ya dola yanatoka kwa wananchi. Je, inawezekanaje mtu kudai uhalali wa uongozi wa umma ikiwa uchaguzi unaonekana kuporwa au matokeo yake hayaakisi matakwa halisi ya wananchi?
3. Leo hii, wananchi wengi wanaishi katika hali ya wasiwasi na kutokuwa na uhakika wa kesho. Imani ya umma kwa taasisi mbalimbali imepungua, huku kukiwa na hofu kuhusu usalama wa watu binafsi na ulinzi wa haki za kiraia. Rushwa imeonekana kuongezeka na kuwa ya wazi zaidi, ilhali mifumo ya uwajibikaji inaonekana kudhoofika. Utakatishaji wa fedha haramu, mtiririko haramu wa fedha, pamoja na biashara ya dawa za kulevya vinaendelea kuwa changamoto kubwa kwa taifa. Kukithiri matumizi mabaya ya pesa za umma , safari za nje kwa watumishi wa umma na kupoteza rasimali za Nchi kwa Wageni .
4. Tafiti mbalimbali pia zimeonyesha mwenendo unaotia wasiwasi katika jamii, ikiwemo ongezeko kubwa la ushiriki wa vijana na watu wazima katika michezo ya kamari. Zaidi ya asilimia 67% ya Watanzania watu wazima wanacheza kamari utafiti wa hivi karibuni umeonyesha. Wakati huohuo, umasikini wa kipato na ugumu wa maisha unaendelea kuwa tatizo kubwa kwa familia nyingi nchini. Haya ni matatizo ya ndani siyo Mabeberu rafiki yangu Dkt. Ayub Rioba
5. Haya ndiyo matatizo yetu halisi. Si matatizo yanayosababishwa na kile kinachoitwa “mabeberu” pekee. Ndiyo maana inashangaza kuona mwanazuoni mbobezi kama wewe ukiendelea kueneza simulizi za kisiasa zilizoasisiwa katika enzi za mapambano dhidi ya ukoloni za miaka ya 1940 na 1950, huku ukipuuzia changamoto za uongozi na utawala zinazolikabili Bara la Afrika leo.
6. Watanzania wanakumbuka mchango na mafanikio ya viongozi wa Afrika wanaowaona kuwa na maono na uwezo wa kuleta mabadiliko, akiwemo Shujaa wa Afrika , Daktari, Rais John Pombe Magufuli. Vilevile, Waafrika wengi wanafuatilia na kujadili mitindo ya uongozi wa viongozi kama Ibrahim Traoré. Mijadala hii inaakisi kiu ya Waafrika ya kupata uongozi wenye uwajibikaji, ufanisi na maono ya maendeleo.
7. Changamoto kuu ya Afrika si suala la ubeberu pekee; bali ni tatizo endelevu la uongozi na utawala bora. Haya si maoni yangu binafsi tu. Yanakumbusha hoja maarufu ya mwandishi na mwanafikra mashuhuri wa Nigeria, Chinua Achebe, aliyesema kuwa tatizo kubwa la Afrika ni kushindwa kwa uongozi bora.
MWISHO: Iwapo Afrika inataka kufikia maendeleo endelevu, ustawi wa kiuchumi na demokrasia ya kweli, ni lazima tuwe tayari kukabiliana kwa uaminifu, ujasiri na ukweli na mapungufu yetu ya ndani katika uongozi na utawala, badala ya kulaumu kila changamoto inayotukabili kwa nguvu za nje.