Manula alikuwa Bora wakati wake.
Tatizo la manula analazimisha acheze yeye tu.
Hata kama hayuko fiti kiutimamu wa mwili.
Manula alikuwa na magolikipa wengi tu pale Simba lakini kila Mechi anacheza yeye hadi akina Kakolanya wakaamua waondoke Simba.
Hata Mechi za ndondo utamkuta Manula Yuko golini.
Katoka majeruhi na kabla ya kupona sawasawa analazimisha acheze yeye ili akina Salim na Ayoub waanze kuchoma mahindi.
Kaanza na Yanga kapigwa 5 Bado anataka apangwe yeye tu.
Manula angaruhusu na wenzake wacheze angeendelea kufanya vizuri kwenye gemu.
Na sio kutaka wanzake wabakie kuchoma mahindi.
Matokeo mabovu ya hivi karibuni kwa Manula yanatokana na tabia yake ya kutaka acheze yeye tu kama Yuko fiti.
Tumemwona Diara ni kipa Bora kabisa lakini anaruhusu na wenzake wacheze hata kwa kusema yeye hajisikii vizuri ili na wenzake wacheze pia, na tunaona makipa wote wa Yanga wanacheza na kuonesha vipaji vyao.
Abadilike la si sivyo huo ndio mwisho wake.
Kwakuwa Mungu anataka na wenzake wapate ridhiki zao pia.