Ayub Rioba: Anayesema TBC tunaripoti zaidi serikali kuliko umma atuletee utafiti

Ayub Rioba: Anayesema TBC tunaripoti zaidi serikali kuliko umma atuletee utafiti

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC), Dkt. Ayub Rioba, ametetea utendaji wa chombo hicho cha habari cha umma dhidi ya ukosoaji kuwa kinairipoti zaidi serikali kuliko wananchi, akieleza kuwa serikali iliyowekwa madarakani na umma inao wajibu wa kuzungumza na kuwajibika kwa wananchi wake kupitia taasisi hizo, huku akiwataka wakosoaji kutoa utafiti wa kisayansi unaothibitisha kuwa TBC inaipendelea serikali kuliko maslahi ya umma badala ya kutoa kauli zisizo na msingi.

"Unajua mimi nawashangaa sana watu. Kwa mfano, nyinyi mmechagua serikali mmeiweka madarakani, alafu sasa inawajibikaje kwenu? Si ni lazima wazungumze? Na katika kuzungumza lazima waje kwenye taasisi kama zetu. Na chombo chetu sisi ni cha umma, na anayesema kwamba tunaripoti zaidi serikali kuliko umma atuletee utafiti, maana haya mambo yanakwenda kwa utafiti."

Soma pia Mkurugenzi wa TBC Ayub Rioba: Rais na CCM wataonekana sana kwenye habari za TBC kwa sababu watu wengi wanataka kujua wanafanya nini

 
Back
Top Bottom