Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC), Dkt. Ayub Rioba, amefunguka kuhusu changamoto za uripoti wa habari za vyama vya upinzani na kuweka wazi kuwa chama cha CHADEMA kilikuwa kimeamua kuisusia TBC bila yeye kufahamu mwanzoni.
Akizungumza kwenye mahojiano yaliyorushwa na Nijuze Julai 26, 2026, Dkt. Rioba ameeleza kuwa licha ya jitihada za kuwaalika viongozi wa upinzani kwenye vipindi, wawakilishi wa CHADEMA waligoma kushiriki kutokana na misuguano ya kimaamuzi ya nyuma, ikiwemo matukio yaliyopelekea TBC kusitisha kwa muda uripoti wa matukio yao ili kulinda usalama wa wanahabari wake.
Dkt. Rioba ameongeza kuwa mgogoro huo ulihitimishwa baadaye kupitia juhudi za usuluhishi zilizowezesha kukutana na aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, na kurejesha ushirikiano.
Aidha amefafanua kuwa TBC haikuwa na uadui na chama chochote cha siasa na kwamba waliendelea kuripoti habari za vyama vya ushindani na hata kumkaribisha aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA (Bara), Benson Kigaila, kwenye vipindi vyao, huku akisisitiza kuwa uendeshaji wa vyombo vya habari vya umma katika muktadha wa uongozi barani Afrika unakabiliwa na changamoto nyingi zinazohitaji utulivu badala ya hisia.