Azam boresheni kitengo cha matangazo ya mpira

Azam boresheni kitengo cha matangazo ya mpira

Rweye

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2011
Posts
17,057
Reaction score
7,611
Mnafanya vizuri lakini kuna baadhi ya maeneo mnapwaya sana. Eneo la matangazo ya mpira mnakosa watu wa kamera wenye viwango vya kiushindani ijapo mnasifika kwa kuwa na vyombo/mitambo ya kisasa na studio ya haja kweli kweli

Pamoja na hilo, mnakosa watangazaji wa maana katika michezo mingi, natolea mifano kutoka kwa wale wanaohudumu pale kaitaba U20. Kutangaza mpira kama si fani basi kitakuwa kipaji, tafuteni watu sahihi kwa jambo sahihi. Ikiwezekana nendeni Star TV mkawahamishe watu kule wako wazuri sana katika hii idara ya matangazo, nendeni EFM n.k mkatafute vifaa vya maana vya kuturushia na kutuyangazia mpira, mpira ni radha, mpira ni kipaji.
 
Mtumieni C. Hillary atawasaidia sana katika hii idara
 
Ningependa Kuona Mnaongeza Camera usawa wa Linesmen kwa ajili ya kunasa Off-sides otherwise Mnafanya Vizuri...
 
Pia, kwenye hii michezo ya U20 pale Dar na Kagera basi tengenezeni mkeka walau mtuoneshe nani ni nani na yupi yuko wapi, mnashindwa nini wakati vitu mnavyo jamani?

Tengenezeni chati kama wanavyofanya wenzenu wa nje, onesheni Idadi ya michezo, Magoli, Nafasi n.k. Ukiangalia mnavyofanya sahivi ni bure kabisa, mechi inaanza inafika mwisho hatuoneshi msimamo wa leo ukoje, nani kapanda nani kashuka na nani yuko juu/chini, mtu unaishia kuangalia tu na kama hukutizama jana basi hutaelewa yupi kakaa wapi na kamshusha nani ....tunawasihi muwe flexible na mujitajidi kuyachukua yale mazuri tunayojitahidi kushauri, tunaamini haya hayahitaji hisani ya US na yako ndani ya uwezo wenu na mnayaweza.
 
Mnafanya vizuri lakini kuna baadhi ya maeneo mnapwaya sana. Eneo la matangazo ya mpira mnakosa watu wa kamera wenye viwango vya kiushindani ijapo mnasifika kwa kuwa na vyombo/mitambo ya kisasa na studio ya haja kweli kweli

Pamoja na hilo, mnakosa watangazaji wa maana katika michezo mingi, natolea mifano kutoka kwa wale wanaohudumu pale kaitaba U20. Kutangaza mpira kama si fani basi kitakuwa kipaji, tafuteni watu sahihi kwa jambo sahihi. Ikiwezekana nendeni Star TV mkawahamishe watu kule wako wazuri sana katika hii idara ya matangazo, nendeni EFM n.k mkatafute vifaa vya maana vya kuturushia na kutuyangazia mpira, mpira ni radha, mpira ni kipaji.

Mkuu kuna ' tatizo ' kubwa sana na la ' msingi ' mno linaloikumba Azam / Uhai Media Group hasa kutokana na kuwapata ' Watangazaji wake na hili limesemwa sana ila bahati mbaya ' wahusika ' masikio yao wameweka ' nta ' Na tatizo hilo hilo lipo pia katika Kampuni ya Simu ya Zantel. Bila ' unafiki ' wala kuzunguka wala kuogopa kulisemea tatizo lenyewe ni ' udini ' uliokithiri hapo hadi imeshakuwa ' kero '. Mwaka huu huu tu kuna Watangazaji mahiri kabisa hadi wapiga picha waliachishwa ' Kazi ' hapo lakini nakupa ' jukumu ' dogo sana fanya ' utafiti ' wako kati ya hao waliopunguzwa wengi wao wako upande ya Yesu Kristo au Mtume Mohamed? Ukipata jawabu utajua nini nilichokisema hapa otherwise naomba niishie tu hapa Mkuu.
 
Back
Top Bottom