Azam Complex wamewezaje Uwanja taifa ishindikane

Azam Complex wamewezaje Uwanja taifa ishindikane

pwilo

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2015
Posts
10,913
Reaction score
13,876
Habari za jioni wadau,

Mungu ni mwema sana kwa kutupa nafasi nyingine ya kuiona siku ya leo iliyosindikizwa na mechi ya kibabe kati ya simba na Azam mchezo ambao umemalizika kwa sare na wote walikuwa wanastahili point moja.

Sio leo tu hata mechi iliyopita waliyocheza azam yalionekana maandishi ambayo yanaonyesha wadhamini wa team na wa ligi lakini ikiwa inaonyesha automatic kama ulaya kule sio mabango kama yale ya taifa ambayo mchezaji akijichanganya likimgonga la kichwa tunamkosa.

Hivi kwa uwanja ule wa taifa wenye hadhi ya international standard unashindwa kufanya wanachofanya azam yaani pale taifa kila kitu ni cha hovyo pitch haitunzwi vyoo havitunzwi mpaka hili la azam linashindakana licha ya hela zote mnazikusanya inasikitisha kwa kweli.

Wataalam mtuambie inawezakanaje azam taifa ishindikane.
 
Nenda kaiangalie barabara ya Kuelekea Fumba unakofanyika mradi wa nyumba za Bakhresa ndio utajua kwanini serikali inashindwa kujenga barabara za ubora kama ule wakati jamaa kaonyesha mfano.

Bei ya Ile Ngalawa iliitwa MV kivikoni iliyofichwa Kwa walinzi Bei yake ilikua kubwa kuliko speed boat mpya za Azam.

Tatizo uzalendo uko midomoni tu, ndani kabisa hatuna hata chembe ya Uzalendo.

Wakati hayo yote yanaendelea, mahakama ya ufisadi Haina wateja.
 
Back
Top Bottom