Azam FC imewatimua makocha wake wote raia wa Hispania

Hakuna Kocha aliyepewa muda na Azam kama Stewart Hall.

Kwanza aliikimbia ligi ya Bongo. Kaona aende Kenya ambapo hakuna Yanga na Simba.

Hawezi kurudishwa.. Naona kocha mwenye uzoefu na soka la Kiafrika akiingia pale.
Kwangu Mimi Kocha mzoefu ambae anafaa azam na miundo mbinu yao ni...Micho ( Kocha mkuu wa Uganda)
 
Kwangu Mimi Kocha mzoefu ambae anafaa azam na miundo mbinu yao ni...Micho ( Kocha mkuu wa Uganda)
Kuna Makocha 13 ktk list ya Azam na Katika wanaotajwa ni kocha wa zamani wa TP Mazembe, Lamine N'Diaye na PLUIJM, Kigezo kikubwa kinachoangaliwa kwa Mujibu wa CEO wao ni Uzoefu na Mafanikio katika Mashindano ya CAF. Azam wameona kuna Umuhimu wa Kutafuta Kocha Msaidizi Mzawa anayeijua Ligi Kuu, Hapa anatajwa KALI ONGALA.... Tusubiri
 
OK kwa hao sawa je babu ataondoka yanga?..N'Diaye km Omog watashindwana tu,ttz azam uongozi unajua sana na upambe mwingi
Plujim mafanikio CAF ni kucheza Makundi Mara mbili
 
Viongozi wa timu ya Azam ni wasaka tonge tu. Wanaota ndoto za CAF pasi na kuwa na wachezaji wanaofundishika. Walipomuajiri P. Omog waliota hivo na timu iliposhindwa wakamtimua, ng'ombe hawezi nenepa siku ya mnada. Kocha lazima apewe muda wa kutosha na ndio maana Pep Gadiola pale Man City anaendelea japo alikuwa bingwa kwao na Ujerumani.
 
Kwangu Mimi Kocha mzoefu ambae anafaa azam na miundo mbinu yao ni...Micho ( Kocha mkuu wa Uganda)
Sie hatuwezekaniki hata aje Mourinho hapa, atakwama tu. Tunataka sifa kubwa bila kuihangaikia.
 
Azam bado inaendeshwa kiswahili tulishasema hakuna walichofanya cha maana zaidi ya kujenga uwanja wa Chamazi bado wanaendesha timu kama Toto African au Majimaji
 
Sasa ameajiriwa kufanya nini ?
 
Azam bado inaendeshwa kiswahili tulishasema hakuna walichofanya cha maana zaidi ya kujenga uwanja wa Chamazi bado wanaendesha timu kama Toto African au Majimaji
Kuna Umuhimu wa Azam Kuwa na KURUGENZI YA UFUNDI
 
Azam bado inaendeshwa kiswahili tulishasema hakuna walichofanya cha maana zaidi ya kujenga uwanja wa Chamazi bado wanaendesha timu kama Toto African au Majimaji
Kwanini hukusema kama Yanga na Simba? Maana timu hizi ndizo chanzo cha kutokukua au kufanya vizuri kwa soka letu hapa nchini Tanzania.
 
Kwanini hukusema kama Yanga na Simba? Maana timu hizi ndizo chanzo cha kutokukua au kufanya vizuri kwa soka letu hapa nchini Tanzania.
Kwa mtazamo wangu viongozi wa Simba/Yanga wanapata upinzani mkubwa kuliko wanaopata Azam.Azam hakuna uchaguzi wa kuchagua viongozi,Azam fedha ipo tayari tofauti na Simba/Yanga
 
Unafikiri ni yapi Majukumu ya Saad Kawemba pale?
Saad Kawemba ni CEO wa Azam FC kazi yake ni kuhakikisha Azam FC inapata mafanikio ndani na nje ya uwanja. Kama CEO wa kampuni na kampuni haifanyi vizuri wa-kulaumiwa ni wewe watendaji wote wa kampuni wako chini yako.

1.Unafikiri hao makocha wa Spain waliajiriwa bila approval ya CEO?

2.Mlitegemea makocha wa Spain wanakuja kufundisha wachezaji wazee kina Bocco,Nyoni,Morris watapata mafanikio?

3.Azam iliwaacha Kipre Cheche,Kavumbangu,Amme Ally hawakusajili replacement wanamtegemea Bocco

4.Kwa nini Azam walimfukuza Joseph Omog kocha aliyewapa ubingwa kwa mara ya kwanza ?
 
Kwangu Mimi Kocha mzoefu ambae anafaa azam na miundo mbinu yao ni...Micho ( Kocha mkuu wa Uganda)
Sie hatuwezekaniki hata aje Mourinho hapa, atakwama tu. Tunataka sifa kubwa bila kuihangaikia.
Azam bado inaendeshwa kiswahili tulishasema hakuna walichofanya cha maana zaidi ya kujenga uwanja wa Chamazi bado wanaendesha timu kama Toto African au Majimaji
Dah! Inasikitisha mno. Wengi tulitegemea kufarijika kisoka kwa kuanzishwa timu hii lakini walewale waliovurunda Simba, Yanga na TFF ndo wamechukuliwa kuiongoza ndo maana wanaona ili kuendelea kumpiga mpunga mzee Bakhresa ni kufukuza makocha tu. Pep Gadiola kaingoza Barcelona kwa mafanikio makubwa mno, akaenda Bayen Munich nako akapata mafanikio vilevile ndipo matajiri wa Man City wakamchukua. Tazama Pep kaingia Man6 kabla ya benchi jipya la Azam lakini mpaka sasa yupo na timu haina tegemeo la ubingwa labda msimu ujao. Wenye akili nyingi sana pale Azam wametimua benchi tayari basi wao wageuke makocha!!!!!!
 
CEO na kurugenzi nzima ya timu wanapashwa kufukuzwa kwani wameona njia ya kula pesa ya mzee ni kufukuza benchi la ufundi tu. Omog alianza kutupa matumaini ya timu kufanya vizuri na angeachwa asajiri wachezaji wake sasa hivi timu ingekuwa pazuri, lakini kwa kuwa wanataka Yanga na Simba tu ndo wabadilishane ubingwa kila msimu wao wananufaika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…