Azam FC imewatimua makocha wake wote raia wa Hispania

Azam FC imewatimua makocha wake wote raia wa Hispania

Hii timu sijui inamkosi gani..!? uwekezaji wote lakini matokeo ni butu
 
Tulishaliona tangu mwanzo hawa Waispania watachemsha tu hapa
 
Uongozi wa Klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati AZAM FC Leo Limesimamisha Benchi zima la ufundi la Timu hiyo linaloongozwa na Kocha mkuu Mhispania Zeben Hernandez kutokana na Mwenendo mbovu wa Timu
source AZAM TWO

My Take: Ni jambo zuri Kwani kwa Uwekezaji ule Haiwezekani Wapinzani wetu wawe Stendi, Majimaji, Mbao nk.
Nafikiri sasa Watumie Mechi za Mapinduzi kama Pre-Season kwa ajili ya FA ili kumantain Uwakilishi wa Kimataifa, Ligi kuu kwa sasa ni kama Tumechelewa
Good comment big up mkuu
 
Hii ni habari nzuri sana kwa mustakbali wa azam FC.Haiwezekani ufundishe kwa kupitia mtafsiri na mafunzo yako yapokewe kama unavyokusudia.

Ila ubaya ni timing ya kuwapiga stop.Kwanini wameachwa baada ya kufanya usajili wa dirisha dogo?Wangeachana na hao makocha mara tu baada ya mzunguko wa kwanza tayari walishaonekana hawana jipya.Usajili wa durisha dogo ungefanywa na kocha mpya
 
Nafikiri Azam FC leadership hawajajua wanachokitaka, in my view ni kama they are not focused. Nilitegemea Azam FC ingekuwa timu kubwa hapa nchini kuliko hata Yanga na Simba kutokana na uwekezaji wake. Looking at players wanaowasajiri, hawaendani na jina na investment kubwa waliyofanya mpaka sasa. Binafsi simuamini CEO wao I don't know Sad, he is not fit for the job.
 
nimeshangaa kwanini wamewachelewesha kwani nahisi lingehitajika hili kufanyika mapema kulingana na hali yao yakiushindani
 
M nafikiri mkulu wa azam atimue wale Jamaa wanaojiita viongozi wa timu hawa wanafocus kupiga hela tu.
 
Kwa mawazo yangu naona azam haitokuja pata kocha kama stewart hall jamaa ni bonge la kocha yule.
 
Uongozi wa Klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati AZAM FC Leo Limesimamisha Benchi zima la ufundi la Timu hiyo linaloongozwa na Kocha mkuu Mhispania Zeben Hernandez kutokana na Mwenendo mbovu wa Timu
source AZAM TWO

My Take: Ni jambo zuri Kwani kwa Uwekezaji ule Haiwezekani Wapinzani wetu wawe Stendi, Majimaji, Mbao nk.
Nafikiri sasa Watumie Mechi za Mapinduzi kama Pre-Season kwa ajili ya FA ili kumantain Uwakilishi wa Kimataifa, Ligi kuu kwa sasa ni kama Tumechelewa

=====

Azam FC imemtimua Kocha wake Mkuu, Zeben Hernandez Zeben na makocha wengine raia wa Hispania, wametimuliwa kazi leo baada ya Azam FC kwenda mwendo wa kusuasua.

Azam FC iko katika nafasi ya nne ikiwa na pointi 27 baada ya kucheza mechi 17.

Katika mechi 17 za Ligi Kuu Bara, Azam FC imechinda mechi saba, imepoteza nne na sare sita, hali ambayo wazi inaonekana kutoufurahisha uongozi wa Azam FC hata kidogo.
Wamechelewa sana kuchukua uamuzi huo. Wale hawakuwa makocha bali waganga njaa tu.

Azam FC wamchukue Pluijim au Micho wa The Craines
 
Back
Top Bottom