PROSPER 05
JF-Expert Member
- Oct 14, 2013
- 226
- 217
Mabadiliko ya ratiba mpya ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) yaliyotolewa muda mchache uliopita(leo Jumatatu 4/9/2017) na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) yanaonyesha kuwa mechi zote za Azam FC za nyumbani dhidi ya Simba na Yanga zitafanyika kwa mara ya kwanza ndani ya Uwanja wa Azam Complex.
Azam Chamazi Complex ni Moja ya Viwanja Bora kabisa na ni kiwanja Pekee Afrika Mashariki na Kati ambacho kilipewa kibali na Shirikisho la Soka Africa (CAF) mnamo tarehe 31 Januari 2014 kuchezea mashindano ya kimataifa yanayoandaliwa na CAF.
Uwanja wa Azam Complex una vipimo vya mita 110 kwa mita 71 sehemu ya kuchezea, pia una milango mine ya kieletroniki na uwezo wa kuchukua zaidi ya mashabiki 7,000 kwa wakati mmoja.
Kwa maana hiyo, Kuanzia mechi ya Azam FC ya Jumamosi hii dhidi ya Simba, itafanyika ndani ya uwanja huo kuanzia saa 1.00 usiku.
Mashabiki wa Azam Fc Tunaishukuru TFF kwa kutupa haki yetu hii muhimu tuliyokuwa tukistahili muda mrefu.
Viva Tff, Viva Karia, Viva Azam Fc....