Azam FC kucheza mechi zake za nyumbani dhidi ya Simba SC na Yanga SC katika uwanja wa Azam Complex

Azam FC kucheza mechi zake za nyumbani dhidi ya Simba SC na Yanga SC katika uwanja wa Azam Complex

PROSPER 05

JF-Expert Member
Joined
Oct 14, 2013
Posts
226
Reaction score
217
azam complex.jpg

Mabadiliko ya ratiba mpya ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) yaliyotolewa muda mchache uliopita(leo Jumatatu 4/9/2017) na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) yanaonyesha kuwa mechi zote za Azam FC za nyumbani dhidi ya Simba na Yanga zitafanyika kwa mara ya kwanza ndani ya Uwanja wa Azam Complex.

Azam Chamazi Complex ni Moja ya Viwanja Bora kabisa na ni kiwanja Pekee Afrika Mashariki na Kati ambacho kilipewa kibali na Shirikisho la Soka Africa (CAF) mnamo tarehe 31 Januari 2014 kuchezea mashindano ya kimataifa yanayoandaliwa na CAF.

Uwanja wa Azam Complex una vipimo vya mita 110 kwa mita 71 sehemu ya kuchezea, pia una milango mine ya kieletroniki na uwezo wa kuchukua zaidi ya mashabiki 7,000 kwa wakati mmoja.

Kwa maana hiyo, Kuanzia mechi ya Azam FC ya Jumamosi hii dhidi ya Simba, itafanyika ndani ya uwanja huo kuanzia saa 1.00 usiku.

Mashabiki wa Azam Fc Tunaishukuru TFF kwa kutupa haki yetu hii muhimu tuliyokuwa tukistahili muda mrefu.

Viva Tff, Viva Karia, Viva Azam Fc....
 
Kweli kwa mara ya kwanza TFF imefanya maamuzi ya kimpira... Azam walikuwa wanabaniwa kwa fitina na tamaa za kupata fedha nyingi bila kuheshimu sheria za soka.... Bravo TFF mpya kwa kuruhusu chama langu kutumia uwanja wake wa nyumbani kwa mechi za vibomba wa midomoni.....
 
Baada ya danadana ya muda mrefu hatimaye Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF) limeamua michezo ya Simba na Yanga ambayo itahusisha Azam FC itachezea kwenye Uwanja wa Azam Complex maarufu kwa jina la Uwanja wa Chamaza.

Maamuzi hayo ni yale ya kuiwezesha Azam FC kuwa nyumbani baada ya awali timu hiyo kutopewa haki ya kucheza uwanja wa nyumbani kutokana na kilichodaiwa kuwanja wao kuwa mdogo na hivyo kutokidhi mahitaji ya kucheza dhidi ya Simba na Yanga uwanjani hapo.

Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas amesema kuwa maamuzi hayo yamefikiwa ili kuipa Azam FC haki yake katika kuutumia uwanja huo ambao unachukua idadi ya mashabiki 7,000 waliokaa kwenye siti.

Amesema kuwa kitakachofanyika ni kuwa tiketi zitakazouzwa ni zitakazotosha kwa idadi ya siti na hazitauzwa zaidi ya idadi halisi ya siti zilizopo uwanjani, hivyo wale watakaokosa watatakiwa kutosogea uwanjani kwa kuwa ulinzi utakuwa mkubwa.

Mchezo ujao wa Azam FC na Simba utakaochezwa uwanjani hapo, utachezwa saa moja usiku ili kupisha mchezo wa mapema wa siku hiyo katika Ligi Kuu Bara kati ya Prisons na Majimaji utakaochezwa saa kumi jioni.

Chanzo: Salehe Jembe
 
Huu uamuzi hauna tija zaidi ya kumfurahisha mdhamini.Hapa kuna mgongano wa kimaslahi yakitimia huko mbele Tusitafute mchawi.Nina uhakika siku moja lazima pageuke Darfur.Tff hamtakwepa Liability.Ni sawa na mwenye gari bovu akamkabidhi dereva gari hilo bovu abebe abiria halafu lipate ajali liuwe watu,mwenye gari analo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mapato wanagawana au timu mwenyeji anachukua yote? Kama ni kugawana Azam timu ngeni itaumia hasa Simaba na Yanga.
 
Mashabiki wengi wa azam ni wanaotoka zenji, na wauza ice cream
 
Nimefurahi sana kwa maamuzi hayo, nakumbuka nilishamshauri malinzi suala hili akasema wanaoamua viwanja ni timu na si tff
 
Mapato wanagawana au timu mwenyeji anachukua yote? Kama ni kugawana Azam timu ngeni itaumia hasa Simaba na Yanga.
vyovyote itakavyo kuwa hapo hakuna cha kuumia wala nn kwa Adam.
 
Mapato wanagawana au timu mwenyeji anachukua yote? Kama ni kugawana Azam timu ngeni itaumia hasa Simaba na Yanga.
Mapato ni ya Tff, Timu mwenyeji na wamiliki wa Uwanja.... bila kusahau kodi
 
Mashabiki wengi wa azam ni wanaotoka zenji, na wauza ice cream
Mashabiki wengi wa Simba na Yanga ni wale Waliorithi kutoka kwa Baba au Kaka Yaani wamependa Timu kwanza kisha wakapenda Mpira. LAKINI Mashabiki wengi wa AZAM ni wale wanaopenda Mpira Kwanza Kisha wakapenda Timu inayojua Maendeleo na mahitaji ya Mpira wa kisasa (AZAM FC).
 
Huu uamuzi hauna tija zaidi ya kumfurahisha mdhamini.Hapa kuna mgongano wa kimaslahi yakitimia huko mbele Tusitafute mchawi.Nina uhakika siku moja lazima pageuke Darfur.Tff hamtakwepa Liability.Ni sawa na mwenye gari bovu akamkabidhi dereva gari hilo bovu abebe abiria halafu lipate ajali liuwe watu,mwenye gari analo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Acha imani potofu we

Manchester united na ukubwa wake inaweza kwenda Wigan inayochukua watu wasiozid 25,000

Achen kufikiria kizaman dunia imebadilika

mchana toch ,usiku magogo tufanyaje?
 
Mtakaokosa nafasi kuna screen nje mtaangalia

sent from my iPhone 7 nimeinunua SAPNA pale Posta mtaa SAMORA
 
Back
Top Bottom